Suala la uraia limefafanuliwa vema kwenye katiba inayopendekezwa

Suala la uraia limefafanuliwa vema kwenye katiba inayopendekezwa

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
SUALA LA URAIA LIMEFAFANULIWA VEMA KWENYE KATIBA INAYOPENDEKEZWA KAMA IFUATAVYO;


(a) Uraia katika Jamhuri ya Muungano.

( IBARA YA 70-71).
Suala la uraia limetamkwa kwenye Katiba Inayopendekezwa. Katiba Inayopendekezwa imebainisha aina za uraia katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuwa ni uraia wa kuzaliwa na uraia wa kuandikishwa.


b) Hadhi maalum ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania.

(IBARA YA 72).
Katiba Inayopendekezwa inatoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye alikoma kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, kuwa na hadhi maalum atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano. Hii itawafanya watu wenye sifa hizo kupata stahili na fursa ambazo ni tofauti na zile za wageni wawapo ndani ya nchi ya asili yao.


TUISOME KATIBA HII NA KUIELEWA VEMA NA MWISHO WA SIKU TUFANYE MAAMUZI SAHIHI YENYE UZALENDO KWA NCHI YETU.
 
Back
Top Bottom