Kila mtu ana lawama zake hapo,labda nijaribu kuainisha sababu mbalimbali za wanafunzi kufeli kwanza ni utoro uliopindukia hasa kwa shule za kijijini,Pili nature ya wanafunzi wengi wa sasa wana uelewa mdogo na kwenda sekondari walienda kwa alama za chini hivyo wanashindwa kabisa kuelewa masomo hasa ya sayansi,Tatu mwamko mdogo wa elimu kwa jamii hasa kwa shule za kijijini,Nne Wazazi kutofatilia taaluma na nidhamu za watoto wao,Tano baadhi ya wanafunzi wanatokea kwenye mazingira magumu hivyo kushindwa kujisomea kwan wanakosa hata hela ya mshumaa pia kwa watoto wa kike na kiume kiasi hupewa kazi nyingi hadi kukosa muda wa kujisomea,Sita uelewa mdogo wa kiingereza,wanafunzi wengine wanaelewa masomo ila swali likibadilishwa lugha kidogo hawezi kulijibu tena,Saba Mabadiliko ya mitaala bila kuwapeleka walimu semina ili waendane na mitaala,Nane Uhaba wa vitabu vya kiada na ziada,Tisa upungufu wa walimu,kumi wanafunzi wanatembea umbali mrefu hivyo wanafika shule wameshachoka sana,Kumi na moja kutokuwepo kwa chakula mashuleni kunafanya wanafunzi wawe na njaa sana na kushindwa kuelewa vipindi vya mwishoni tatizo hili ni kwa shule za kutwa,kumi na mbili Mchanganyiko wa siasa kwenye elimu,hii inafanya kupelekwa sekondari wanafunzi wenye alama za chini sana,kumi na tatu tatizo la nidhamu kwa wanafunzi pia baadhi yaoi kujihusisha kwenye mapenzi,kumi na nne uzembe wa wanafunzi kujisomea kumi na tano Wanafunzi Kusoma tution za mtaani zinazotoa elimu isiyo bora,kumi na sita Walimu kulipwa mishahara midogo inawakatisha tamaa kufundisha,kumi na saba Kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya shule na wazazi/walezi wa wanafunzi,kumi na nane uhaba wa madarasa,viti meza,maktaba na labaratory