Suala wanafunzi kufeli mtihani robo tatu ya darasa nani alaumiwe......

Joined
Oct 23, 2012
Posts
6
Reaction score
2
Katika shule niliyohtim mimi inaiyoitwa Nakoza Secondary ni robo ya wanafunzi tu ndo wamefaulu mtihani wa kidato cha pili sekondary ye2 ni ya kata kwa hyo kila m2 anaish kwao....sasa KUTOKANA NA MATOKEO HAYO NANI TUMLAUMU KATI YA HAWA? 1.MWANAFUNZI KUTOJISOMEA 2.MWALIMU 3.MZAZI KUTOMUHMIZA MWANAYE KUJISOMEA............ni hayo wana JF
 
hebu jaribu kugusa chanzo cha tatizo lenyewe...mwanafunz anajiunga sec sch akiwa hajui kusoma vizuri nini unategemea? Kufutwa mtihan wa kidato cha pili kuruhusu mbulula kufanya majaribio kwenye mtihani ambao ndo unaamua hatima ya maisha yao? Unadhani ni kwann wamerudisha mtihani huo? Wamepaona hapo..sasa uje uangalie matokeo ya kidato cha nne ya hawa wanafunz waliolejeshewa mtihan wa form 2 yatakuwa tofaut tu, kitu kingine wanasiasa wanawaharibu wanafunz kiasi cha kuleta siasa hata kwenye masomo,ndo maana wanafnz hawana adabu, na wakishakosa nidham bac hao ni mbulula watarajiwa,angalia shule za seminari hapa bongo zinafanya vizur si kwa sababu wanafunz wanaakil sana au wanawalim walioshushwa toka mbinguni lahasha ni kwa sababu ya nidham,tumefuta viboko unatarajia nn? Toto unaliambia kitu linakaid maksud coz linajua hutalifanya kitu,hivyo mwalim analiacha...lakni mgomee mwalim wa zamani uone moto..ndo maana wanafunz wa zaman walikuwa na uwezo mzur.
 
Serikali ndo wa kwanza kulaumiwa halafu wazazi asilimia 64 ndo wamefeli halafu 35 wamefaulu naibu waziri kadanganya.
 
mwanafunz ni wa kulaumiwa,mwalimu anaweza fanya sehemu yake mwanafunz akabaki kuangalia tamthilia, mzazi nae anweza mpa mwanafunz kila kitu ila mwanafunzi akawa mzembe.BORA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI UMERUDI
 
Kila mtu ana lawama zake hapo,labda nijaribu kuainisha sababu mbalimbali za wanafunzi kufeli kwanza ni utoro uliopindukia hasa kwa shule za kijijini,Pili nature ya wanafunzi wengi wa sasa wana uelewa mdogo na kwenda sekondari walienda kwa alama za chini hivyo wanashindwa kabisa kuelewa masomo hasa ya sayansi,Tatu mwamko mdogo wa elimu kwa jamii hasa kwa shule za kijijini,Nne Wazazi kutofatilia taaluma na nidhamu za watoto wao,Tano baadhi ya wanafunzi wanatokea kwenye mazingira magumu hivyo kushindwa kujisomea kwan wanakosa hata hela ya mshumaa pia kwa watoto wa kike na kiume kiasi hupewa kazi nyingi hadi kukosa muda wa kujisomea,Sita uelewa mdogo wa kiingereza,wanafunzi wengine wanaelewa masomo ila swali likibadilishwa lugha kidogo hawezi kulijibu tena,Saba Mabadiliko ya mitaala bila kuwapeleka walimu semina ili waendane na mitaala,Nane Uhaba wa vitabu vya kiada na ziada,Tisa upungufu wa walimu,kumi wanafunzi wanatembea umbali mrefu hivyo wanafika shule wameshachoka sana,Kumi na moja kutokuwepo kwa chakula mashuleni kunafanya wanafunzi wawe na njaa sana na kushindwa kuelewa vipindi vya mwishoni tatizo hili ni kwa shule za kutwa,kumi na mbili Mchanganyiko wa siasa kwenye elimu,hii inafanya kupelekwa sekondari wanafunzi wenye alama za chini sana,kumi na tatu tatizo la nidhamu kwa wanafunzi pia baadhi yaoi kujihusisha kwenye mapenzi,kumi na nne uzembe wa wanafunzi kujisomea kumi na tano Wanafunzi Kusoma tution za mtaani zinazotoa elimu isiyo bora,kumi na sita Walimu kulipwa mishahara midogo inawakatisha tamaa kufundisha,kumi na saba Kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya shule na wazazi/walezi wa wanafunzi,kumi na nane uhaba wa madarasa,viti meza,maktaba na labaratory
 
Kuna mpango wa siri tena wa kijasusi ambao wazazi wanaporwa watoto wao ili wafugwe kwnye mabanda yanayomilikiwa na serikal si wapewe maarifa bali wandaliwe kukataa uwepo wa MUNGU aliye hai.! Mtoto asiyejua kusoma na kuandika unampeleka sec.ili nini kama si kumpora mzaz na kumbebesha gharama za kumfuga mpumbavu!!?? Serkali inahusika 100% kama sivyo angalia trick yake ya kutumia AKILI ndogo kuongoza AKILI KUBWA.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…