SUB-CONSCIOUS MIND KATIKA UCHAWI

SUB-CONSCIOUS MIND KATIKA UCHAWI

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Karibu Binti na mwana wa mama Afrika.

Mwanzoni nilieleza kama ufahamu wa juu wa mtu, Mungu aliufanya kuwa ngumu mtu kuuongoza kwa sababu maalumu.

Moja ya sababu ni kutodhurika na uchawi.

Nilishasema kila kitu unachokistahiri ili kumudu kuishi hapa duniani Mungu alikupa, hivyo hutokuja kusikia Mungu kaleta jambo/ kitu kipya kwako.

Hawa wanaosema Mungu anatupigania, si kwamba Mungu kashusha malaika kama wasemavyo, bali, Wanakuwa na uwezo mkubwa kiimani ili kukabiliana na nguvu za kiroho zisizoonekana.

Kama kuna nguvu mbaya kiroho zisizoonekana, pia Kuna nguvu nzuri kukinga hizo nguvu mbaya zisimdhuru mtu.
Ifahamike kuwa Kila mtu na kila kitu hufanyika Kwa Imani (neno, wazo).
Hivyo ili mtu kukudhuru anatumia Imani, pia wewe kujilinda utatumia Imani pia.

TOFAUTI YAKO NA WACHAWI.

Biblia inasema Imani bila matendo imekufa.
Neno hilo linamaanisha, Ili Imani ilete maana au izae matunda ni lazima iendane na matendo.

Nilisema Subconscious ni ufahamu wa juu wa mtu kimaandiko ni roho au moyo.
Yale unayoamini maishani ndiyo hujaa moyoni kisha moyo au Subconscious huumba, uhalisia au jambo halisi.

Kuna wakati unaweza kuwa na hofu juu ya kutokea jambo fulani, heidha ugonjwa, au kupatwa na tukio fulani.
mfano ukasingizia kuumwa kichwa ili usiende shule na kweli kichwa kikaanza kuuma.
Ukahisi mtu fulani atakuja kukudai na baada ya Muda anakuja.
Unahisi mtu fulani atafanya kitu fulani na inakuwa hivyo.

Matukio kama hayo huwa ni imani, ila hutokea kulingana na kiwango cha imani yako.
Ikiwa na maana ukiamini kidogo Subconscious yako itaumba tukio kidogo, ukiamini sana inaumba sana.
Ukiamini sana kutokewa na mabaya, yakitokea usimlaumu Mungu wewe ndiye muumbaji mkuu.

Kwa mfano huo, inamaana Mungu hahusiki kukulinda na Madhara yoyote ya kiroho, sababu kazi hiyo kakuwekea katika Subconscious mind, uamini ikulinde au usiamini hudhurike.

Wanasayansi, walimu, watumishi wa Mungu, waganga, madaktari, wachawi, wauzaji, wanunuzi na wote wanacheza na Subconscious ya mtu.
Sababu ndiko kwenye kujenga na kuharibu mpangilio wa uumbaji.

Uchawi ni sayansi au utendaji uliopitiliza, ambaye anafanya huo utendaji huitwa mchawi.
ushirikina ni nguvu ya imani kuhusiana na Uchawi kwa njia hasi.

Anayetumia uchawi kuleta mabadiliko chanya, huitwa sayansi.
ila anayetumia uchawi kuleta mabadiliko hasi, huitwa ushirikina.

Uchawi ni kutumia nguvu isiyoonekana ya kitu ili kuleta matokeo au mabadiliko halisi.
Ukijua kutenda mchanganyiko wa nguvu za vitu fulani hutengeneza Bomu (Radi), kimbunga, kinga, dawa, virusi na magonjwa.
Hivyo uchawi ni uleule, ila mazingira ndiyo hufanya huyu kuitwa mchawi, mganga, doctor, n.k.

Imani ni kuamini hili lina nguvu fulani, na Kuifanya hiyo nguvu kuleta matokeo ( matendo).
Ukijua kutenda, mchanganyiko wa vitu fulani unaweza kutengeneza nguvu ya kulinda, kuharibu, kudhuru au kunufaisha.
Na hapa ndipo kuna tofauti ya mchawi na asiye mchawi.

Mchawi anaamini na kutenda, asiye mchawi anaamini tu hawezi kutenda.

Siri ambayo wengi hawaijui.

Matendo ni zoezi la kuiimarisha Subconscious mind, ili ipate uwezo wa kuumba.
ikiwa na maana usipoilisha matendo, uwezo wake unapungua na kufa.

Ndiyo maana ya imani bila matendo imekufa.

Sababu matendo hustawisha Subconscious, ina maana chenye nguvu ni Subconscious na ndicho huwindwa sana na Wachawi pia.
Huwezi kulogeka kama Subconscious yako haiamini Uchawi.

Nakuhakikishia, watu wanaologwa au kudhurika na uchawi, ni wale wanaoamini sana uchawi, sababu nimesema Uumbaji hufanywa na Subconscious.

Asiyeamini ushirikina anaweza kuathirika, lakini halogeki kabisa iwe ni muumini wa dini au imani fulani au si muumini au hana imani yoyote ya kidini, sababu Subconscious haina dini, elimu wala taifa.
Ujue usijue itafanya kazi kama kawaida yake.

Unapoona umeamka na kunyolewa nywele, umelazwa nje ya nyumba, kipande cha nguo kimekatwa na kubebwa, kuona alama, au dalili ya kuonyesha kuna tukio la kichawi umefanyiwa.

Fahamu hujalogwa na aliyefanya hivyo, hana uwezo wa kukuloga.
Anakutisha ili kuiathiri Subconscious yako, itoke katika kuamini unachoamini na kurudi kuamini katika uchawi.

Ataathiri kwa kukuonesha, ndiyo maana tukio lolote kati ya niliyotaja, huwekwa wazi ili uone/ lionekane.
Nywele atakunyoa mbele, nguo atakata ile ambayo unapendelea kuvaa au iliyo rahisi kuiona.

Kurejea katika maandiko, Uchawi wa Wamisri ulimuathiri Musa kuona kamba ni nyoka.
baada ya Mungu kumwelewesha, naye alitumia njia hiyo pia nao waliona fimbo imekuwa nyoka na kumeza zile nyingine.

Sina maana wanaoenda kwa waganga wanalogeka, ila uchawi na uganga unazidiana viwango.

Ushauri.

Kama utapenda kujilinda kupitia Waganga, basi upate mganga bora kuliko wachawi wote, ila akitokea mchawi kuliko mganga wako jua Umeisha, sasa unampata wapi mganga bora kuliko wachawi wote?.

Kama huwezi kumpata mganga bora, ni bora usijaribu hata kusogea katika imani hizo kupata kinga ya aina yoyote.
Utakuwa umeruhusu mwanya wa kulogeka.

Tuwe pamoja.
Sisi ni Afrika tu u1.
 
Back
Top Bottom