Subaru Impreza Hatchback ni Chaguzi Sahihi??

Jack HD

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
851
Reaction score
1,168
Wakuu habari za weekend,

Sio siri nimejibana sana kununua ndinga nikiamini kwenye kuanza kujenga. Nashkuru nimepata kapango cha kujihifadhi na nimeamua kuvuta ndinga. Kabla sijavuta mchuma niliwafuata jamaa zangu kadhaa kwa ushauri. Vipaumbele vyangu vingiwa Gari yenye gharama ndogo ya mafuta, maintenance na uagizaji. Nilihitaji gari isiyokuwa na engine capacity ya zaidi ya 1500 na owe low mileage, chini ya 80,000KM. Niliposhauriwa IST I was like kila nikigeuka naona everybody owns it, imekaa sana sokoni soon itaondoka na hii gari nataka nikae nayo kwa muda. Wapo walionishauri Allex, Premio lakini mwisho wa Siku I met this friend of mine. Akaniuliza what is your desire. Nikamwambia Subaru Impreza Hatchback zilizoanza kutoka mwaka 2007. Tukaanza kuifanyia assessment. Kwenye ulaji wa mafuta ni 13/16 urban/highway it can go down to 10km/l kukiwa na traffics kubwa. I can use budget ya IST ama Allex kuimport hii gari, utata kidogo ulikuja kwenye maintenance. Cost zilionekana kuwa juu kiasi though tuliambiwa spare zake ni mkataba. Je, Subaru Impreza Hatchback ni chaguzi sahihi? Vp kwenye masuala ya maintenance kuna yoyote mwenye experience na hzi gari akaongelea?? Shukrani!!
 
Subaru yenye cc 1500 huwezi linganisha na Hizo toyota alex/ist yenye cc 1500,subaru inakunywa juu kiasi.

Hio cc 1500 ya impreza isikudanganye mkuu.

Boxer engine zina tabia ya kuunguza head gasget,kwny garage zimeshazikuta zikiwa na shida hizo though sio mara nyingi kiviile.

Khs maintainance watakuja wadau kuelezea.

Though kwangu mimi,i prefer power kuliko mambo ya consumption.
 
Mkuu Power ya hii Impreza iko juu sana kulinganisha na IST. Iko na 6000rpm horse power. Hapa nadhani inakwenda sambamba na crown 2.0L/2.5L
 
Ndio maana nimekwambia ukitaka kununua hio subaru masuala ya consumption usiyafikirie kabisaa,hio inakunywa kama kawa mkuu.
Mkuu Power ya hii Impreza iko juu sana kulinganisha na IST. Iko na 6000rpm horse power. Hapa nadhani inakwenda sambamba na crown 2.0L/2.5L
 
Dadeeki umenikumbusha siku nilikua na jmaa zangu na hiyo imprezza tumetoka mwanza kuja dar..tulitelekeza moro..ina Cc 1500 lakini kanabugia wese hatari
 
Dadeeki umenikumbusha siku nilikua na jmaa zangu na hiyo imprezza tumetoka mwanza kuja dar..tulitelekeza moro..ina Cc 1500 lakini kanabugia wese hatari
Its 1490Cc 1.5S 2WD Impreza 2007, kwa wanaotumia Subaru aina hii wanasema ulaji wake ni juu kiasi ya IST but that is nothing when you compare Subaru & Toyota.
 
He he he he he he! Wabongo tunafurahisha sana.

Kwani ungeanzia tu kuulizia kuhusu Subaru kulikuwa na tatizo?!!! Sasa umeanza kuelezea story za maisha binafsi, mara kujenga. Hivyo vingine ni non of our business.

Binafsi umbo la subaru huwa halinivutii!
 



Kaka najua ushapata ushauri mkubwa kutoka kwa watu ila nachokwambia ni kuwa kama unataka gar ya alinunua babu had mjukuu anatumia chukua subaru regardless kama ni impreza ama legacy ama forester as long as ni non turbo hutajuta


Mi nina legacy ya 2002 yenye cc 2.0 napata 10km/l trip towns highway 13 to 14

Huu ni mwaka wangu wa sita and i have abused this car only God knows how, maana ndo hakahaka
Njia zote nimekapitisha na it had never fails
Me

Kuhusu spare yah zina bei ila ukifunga unasahau hata iwe used. Mi mwenye natembelea used spare na nimebadili shockup once nilipoingiza otherwise ni mabush ambayo nabadili at least once a year au year and a half

Mafuta asikudanganye mtu mimi yangu inakula
Mafuta kama gar yoyote ile ambayo ni non turbo yenye cc 2000 iwe toyota carina ama IST


Kuhusu kuunguza gasket mi nina mwaka wa sita na nina km 165000 sijabadili
Chochote kwenye engine na gar imeingia ikiwa na 100k

Kikubwa matunzo naweka recomended Oil ambayo ni around 150k bei ila
Inakupa 20km mi naibadilisha nikifika 10km oil
Inatoka bado mupya

By the way yangu ni manual

Nina thread humu imezungumzia
Subaru na bei za spare itafute
 
Shukrani sana Fredwash comment yako imenijenga sana na hata thread yako nimeipitia Mzee
 
Wadau nimeagiza Subaru Impreza Hatchback 1.5L 2007 with 79000KM. Kuna Uzi niliousoma humu JF kwamba unapoagiza gari wakati wa pre inspection inakuwa inafanyiwa kabisa na service huko hivyo ukija hakuna haja ya service ni moja kwa moja kuingia barabarani. Je, ni sahihi?so sihitaji kabisa kumwaga oil wala kubadilisha filter ama kufanya general check up?? Nasubiri maoni yenu.
 
Subaru ni gari nzuri sana kwani aina mgonjwa ya mara kwa mara ukilinganisha na Toyota

Kuhusu mafundi wapo wa kutosha, sio kama zamani na spea zinapatikana kila kona na ni OG

Ukiwa barabarani utaenjoy sana ni gari ambayo imetulia barabarani

Kuhusu mafuta, aili kivile mafuta kama watu wanavyokutisha japo inaweze isiwe sawa na ist japo raha ya hii gari ni tofauti na ist

Mwisho wa siku chagua kitu roho inapenda maisha yenyewe mafupi haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…