Sema wanawake wapunguze njaa kwa kweli. Wikiend ya pasaka bhana nilikua kiwanja fulani hivi na washkaji nimepiga vyombo sasa bill inakuja sina cash nikamwambia muhudumu alete mashine ya kuchanja nilipe kwa kadi sasa kutokana na kuzoeana nae si ile kadi nilivyoitoa akaishika akaondoka nayo sikuchukulia siriaz sana sababu haijui password punde kidogo akarudi na mashine pamoja na kadi sasa kila nikichanja mhamala hausomi bahati nzuri kuna atm karibu nikaenda napo naambiwa kadi imezuiwa sio kesi nikalipa bill kwa mpesa. Ilivyofika jumanne nikaenda bank kuuliza kulikoni kadi yangu inasumbua, nikaambiwa ilizuiwa na system kwa sababu niliingiza password tofauti mara nyingi sana, moja kwa moja nikajua yule muhudumu aliendoka na kadi alitaka kunipiga alijaribu kufanya muhamala kwa siri kilichomkwamisha hakua anajua password kwaiyo akawa anabahatisha bahatisha. Basi pale benki wakanilekebishia shida yangu kadi ikawa fresh nikasepa. Wanawake sasa hivi sio wadangaji tu wamekua matapeli kabisa.