Sudan: Idadi ya waliouawa tangu Jeshi kuchukua Madaraka wafikia 39 baada ya wengine 15 kuuawa jana

Sudan: Idadi ya waliouawa tangu Jeshi kuchukua Madaraka wafikia 39 baada ya wengine 15 kuuawa jana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Vikosi vya usalama nchini Sudan wamewauwa waandamanaji 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa baada ya kutumia risasi za moto kuyakabili makundi ya watu waliokusanyika kupinga hatua ya jeshi kunyakua madaraka.

Duru kutoka nchini Sudan zinasema waandamanaji wote 15 waliouwawa ni kutoka wilaya za kaskazini mwa mji mkuu Khartoum, ambazo zimeshuhudia ghadhabu kubwa ya umma unaopinga utawala wa kijeshi.

Muungano wa madaktari nchini Sudan umesema vifo hivyo vinafanya idadi ya waliouwawa tangu kuzuka wimbi la kupinga utawala wa kijeshi kufikia watu 39.

Muungano huo umesema wengi ya waliopoteza maisha jana walikuwa na majeraha ya risasi kwenye shingo au viungo vingine vya mwili.

Madai ya kutumika risasi za moto yameelezwa pia na waandamanaji wenyewe ikiwemo mmoja aliyetambulishwa na shirika la habari la AFP kwa jina la Soha aliyesema ameshuhudia kwa macho yake mwenyewe mtu akipigwa risasi na polisi mjini Khartoum
 
Back
Top Bottom