Sudan kusini yazidiwa kete olimpiki yakubali kichapo kutoka kwa Marekani

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Timu ya kikapu ya Marekani imeibuka na ushindi wa pointi 103 - 86 dhidi ya Sudan Kusini katika mechi ya Olimpiki iliyomalizika muda mfupi uliopita huko Ufaransa.

Sudan imeshindwa kufua dafu mbele ya Marekani yenye mastaa kama Kevin Durant, LeBron James, Anthony Edwards, Devin Booker and Derrick White, Steph Curry na wengine.

Katika mechi hiyo Sudan Kusini imefanikiwa kushinda raundi ya tatu na pointi 21 kwa 18 huku raundi zingine tatu Marekani ikiibuka kidedea.

Ushindi wa Marekani katika mechi za kundi C umeipa nafasi ya kusonga hatua inayofuatia ikiwa kileleni na pointi 4 ikifuatiwa na Serbia yenye pointi 3 na Sudan Kusini yenye pointi 3 kila timu ikicheza mechi mbili, Puerto Rico inashikilia mkia kwenye kundi hilo baada ya kupoteza mechi zake zote mbil
 
Nifaida ya Sudan kusini kuwa na pro wa kutosha wanao cheza kwenye Ligi zenye ushindani.
 
Back
Top Bottom