Sudan yakifuta chama tawala cha Al-Bashir, hii ina maana gani?

Sudan yakifuta chama tawala cha Al-Bashir, hii ina maana gani?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Sheria imepitishwa nchini Sudan ya kuvunja chama cha rais aliyeng'olewa madarakani Omar al-Bashir.

Bwana Bashir alichukua mamlaka 1989 kwa mapinduzi na kuliongoza taifa hilo kwa takriban miongo mitatu, hadi alipoondolewa kwa vuguvugu la maandamano ya upinzani mwezi Aprili.

Mamlaka inayoongoza kipindi cha mpito nchini humo pia imeondoa sheria ya umma ambayo ilitumiwa kudhibiti mienendo ya wanawake.

Hatua zote zimejibu madai muhimu ya vuguvugu la waandamanaji, ambayo yalilenga kuvunja utawala wa rais Bashir.

Sudan kwa sasa inaongozwa na utawala unaojumuisha jeshi na baraza la kiraia pamoja na baraza mawaziri la raia linaloongozwa na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok.

Hii ina maana gani?
Kuvunjwa kwa chama tawala cha Bwana Bashir cha National Congress Party (NCP) inamaanisha kuwa mamlaka zinaweza kuhodhi mali za chama .Sheria imethibitisha kuwa kamati itaundwa kutekeleza hili.

Hii inafanyika ili'' waweze kurejesha utajiri ulioibiwa wa watu wa Sudan ". alisema Bwana Hamdo katika ujumbe wake wa Twitter.

Sheria hiyo pia inasema "hakuna nembo yoyote ya utawala au chama itakayoruhusiwa kuhusika katika shughuli yoyote ya kisiasa kwa miaka 10 ''

Msemaji wa Muungano wa wasomi wa Sudan, kikundi cha waandamanaji kilichompindua rais al-Bashir, ameiambia BBC kuwa huu ulikuwa ni " wakati wa kihistoria".

"Huu ni wakati wa ahueni , kwasababu kila mtu nchini Sudan ameathiriwa vibaya kwa namna moja au nyingine na utawala ," alisema msemaji Samahir Mubarak.

Hata hivyo mchambuzi wa siasa kikanda na Bwana Mohammed Issa, anasema inapotokea hali kama iliyoikumba Sudan kama yaliyotokea sudan ambapo chama tawala kilichokuwa madarakani kinapinduliwa hatua ya kukivunja chama tawala haina maslahi kwa mustakabal wa Sudan.

''Hatua iliyochukuliwa na viongozi wa mpito kujenga utengamano haina maslahi katika kujenga utengamano wa Wasudan. Ilitarajiwa kwamba kungekuwa na ujumuishaji wa makundi yote katika siasa za nchi kwa ajili ya mustakbal.'', ameiambia BBC Bwana Issa kutoka Dar es salaam Tanzania.

Anasema:''kuvunjwa kwa chama cha National Congress (NCP), kinawaacha viongozi na wafuasi wa chama kile na washirika kama vile wafuasi wa kundi la Janjaweed bila uwanja wa kuelezea maoni yao ya kisiasa, na hali hiyo inaweza kuwafanya waelezee hisia zao kwa njia ya vita na uasi''.

Ni sheria gani nyingine zilizobadilishwa?

Sheria tata za umma ambazo zilikiuka vibaya haki za wanawake pia ziliondolewa.

Wanaharakati wanasema chini ya sheria za ukandamizaji, zenye misingi ya ufafanuzi sheria ya Kiisalmu (Sharia) , wanawake walikamatwa kwa kuhuduria mikutano ya binafsi ya chama au kwa kuvaa suluari.

Wahaharakati wa haki za binadamu wanasema maelfu ya wanawake walikamatwa na kupigwa kwa mienendo isiyofaa kila mwaka, na sheria zilitumiwa kiholela.

Mabadiliko yaliyotangazwa na na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok yalitimiza madai muhimu ya waandamanaji
Wairi Mkuu Hamdok alituma ujumbe wa Twitte : " Sheria za umma pamoja na maadili ya umma zilitumiwa kama chombo cha unyonyaji, kuaibisha na ukiukaji wa haki za raia na ukiukaji wa hadhi ya watu.

"Ninatuma ujumbe heshima kwa vijana wa kike na kiume wa nchi yangu ambao wamepitia masaibu ya utekelezwaji wa sheria hizi."

Tarehe 25 Novemba, Sudan ilifanya matembezi ya kwanza ya maadhimisho ya miongo kwa ajili ya Siku ya kimataifa ya kutokomeza ghasia dhidi ya wanawake.

Wanawake walikua mstari wa mbelekatika vuguvugu lililomg'oa madarakani Bwana Bashir.

1575026421641.png
 
Attachments

  • 1575025648533.gif
    1575025648533.gif
    51 bytes · Views: 1
Hii habari natamani iwafikie hao maprofesa na madokta ili wajue athari wanazozisababisha kwa historia.
Ni bora mara mia kuwa chama cha upinzani lakini kikabakia katika historia ya nchi lakini kwa yanayoendelea huenda watakaokuwepo nyakati hizo wakaamua hata kulifuta hilo jina maana kila likionekana litakuwa linaashiria maumivu ya nyakati zilizopita!
 
Aisee Naamini kwa mageuzi hayo ni suala la muda tu Sudan watatupita kimaendeleo tena kwa mbali sana,watanzania sijui tuna nini,yaani uoga umetuzidi mno tumekuwa kama mazezeta aisee,tuamke tuyatoe mafisi ya lumumba.
 
Ina maaana hii ikija tokea Bongoland
Jembe na nyundo watarudisha mali zooote walizojipa serikalini
Eeeeeh bora itokee aiseeee
 
Ina maana kuwa jembe na nyundo lazima siku moja yayeyushwe tutengeneze zana za kisasa za kazi
 
Ule UGALI WA YANGA sina imani nao kabisa!
Aisee Naamini kwa mageuzi hayo ni suala la muda tu Sudan watatupita kimaendeleo tena kwa mbali sana,watanzania sijui tuna nini,yaani uoga umetuzidi mno tumekuwa kama mazezeta aisee,tuamke tuyatoe mafisi ya lumumba.
 
Hii habari natamani iwafikie hao maprofesa na madokta ili wajue athari wanazozisababisha kwa historia.
Ni bora mara mia kuwa chama cha upinzani lakini kikabakia katika historia ya nchi lakini kwa yanayoendelea huenda watakaokuwepo nyakati hizo wakaamua hata kulifuta hilo jina maana kila likionekana litakuwa linaashiria maumivu ya nyakati zilizopita!
Yaani hili ni somo tosha kwa chama kilichopo hapa bongo
 
Aisee Naamini kwa mageuzi hayo ni suala la muda tu Sudan watatupita kimaendeleo tena kwa mbali sana,watanzania sijui tuna nini,yaani uoga umetuzidi mno tumekuwa kama mazezeta aisee,tuamke tuyatoe mafisi ya lumumba.

Kwani kwa taarifa za sasa, Sudan inazidiwa kimaendeleo na Tanzania? Au wewe unasemea South Sudan?
 
Ccm wameiba viwanja vya michezo vyote wataifishe ili vikarabatiwe
 
Back
Top Bottom