Sufi/sufu inapatikana kwa wingi mkoa gani?

Means 600Tsh/kg.
Kuipata hiyo kilo moja si nusu mfuko wa debe 6 sasa?
Muambie jamaa huyo wa Botswana kwa bei hiyo hapana,tuvunjike bure kama sio vifo miti yenyewe kama mibuyu uchumaji wake mgumu sana aisee
 
Sufi inatokana na matunda ya miti ya misufi Tanga ipo mingi, sufu ni manyoa ya kondoo wanapatikana Kitulo Njombe.
 
Kitu imekuchanganya ni kusikia hizo LAKI SITA kwa tani, sijui kama unaelewa kuwa TANI 1 ni Kilo 1000…. kwamba KILO 1 ya SUFI/SUFU ni Tsh 600/-!

Kwa bei hiyo hata PAMBA tu hapati bwashee.!
Wewe haujui tofauti ya sufi na sufu, hauwezi kusema sufi au sufu! Ungeuliza kwanza.
 
Miaka ya zamani kabla ya sponji magodoro na mito(siyo ya maji) vilitengenezwa kwa kutumia sufi, mkonge(katani) na manyoa ya kuku.
 
Nimewasiliana nae muda huu kuhusu bei kulinganisha na ugumu wa upatkanaji amenijib kwamba ngoja afanye calculation then kesho atajibu khs kuongeza kiwango cha bei.
Yes ongea nae aongeze bei watu tuingie mzigoni.
 
Means 600Tsh/kg.
Kuipata hiyo kilo moja si nusu mfuko wa debe 6 sasa?
Muambie jamaa huyo wa Botswana kwa bei hiyo hapana,tuvunjike bure kama sio vifo miti yenyewe kama mibuyu uchumaji wake mgumu sana aisee
Tayari amenipigia leo anasema ishu ya kuongeza pesa sio shida,shida yake zipatikane tu,Anasema alitaja kiwango hicho akijua kwamba kwa Tanzania inapatikana kirahisi ila baada ya kumwambia mambo ni tofauti Anasema kwa huu mwanzo anaweza kununua kwa 1,0501,000 kwa ton lakini ameuliza hivi.
1:Tone 1 mtu anaweza akaipata kwa muda gani
2:Miezi gani hiyo sufi ndiyo inakuwa nyingi
3:Huko inakopatikana gari/roli inafika?

Ukiwa tayar nichek inbox nikuunganishe na muhusika.
 
Biashara kichaa hio achana nayo.
Utapoteza bure muda na nguvu zako.
 
Hiyo tani 140 ya December nafikiri mtamaliza sufi yote ya afrika mashariki [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…