Suggest a College/University For My Undergraduate HRM Programme here in BONGO.

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
1,287
Reaction score
486
Hallo wana JF.
Mungu akinipigania Uhai nataka nikapambane na Adui Ujinga kwa Kuongeza Elimu mwakani 2014. Infact baada ya kumaliza Kidato cha Sita 2001, utamu wa kazi ulinifanya nikashindwa kuona umuhimu wa Kugraduate kwanza ndio maana nilikawia kwenda Shule.

Lakini hivi sasa kila nikitembea nasikia kelele/kengele zikisemezana na kunihimiza kichwani kuwa this is your right time for you to go to school.
Na kadri siku zinavyozidi kwenda ndio zinazidi kukua na kunifanya kushindwa kufikiria tena Mambo mengine kama ya Maendeleo.

Mkiwa kama waungwana, kwa wale hasa waliobahatika kupiga hatua mbele na kupambana na huyu adui UJINGA naomba Mnipendekezee Chuo ambacho naweza kupata Shahada yangu ya "HR" bila longo longo kwani vyuo vingine inasadikika kuwa na Longo longo.

Tafadhali naombeni ushauri wenu mkitaja Chuo na Wasifu wake kwa Course husika ya HRM.

Msiache kuniwosia kuwa niepukane na Nn ili niweze kuwa Kinara mwisho wa Course yangu ili niweze kuvuka na kuvunja Record kwenye Familia/Ukoo wangu kwa kupata Shahada ya UZAMILI pia. Umri wangu ni 32yrs, pia niko na Familia at the moment. And I plan to go for a Full time course.

Thanks Wajameni.
 
Nenda Zoom college kipo mkabala na Nmb MbeyA mjini.
 
Mmh! kiukweli ndugu yangu elimu yetu hii ya sasa ya kitanzania imekua kizungumkuti. Kwa mtizamo wangu Sidhani Km kuna chuo bora hapa Tanzania maana hata records zenyewe za vyuo bora ukizichunguza kiuhalisia zaidi utagundua ni za kwny makaratasi hamna uhalisia wowote ule wa hali halisi.
Kikubwa hapa just for angalau ni kupata chuo cha serikali ambapo hapo nadhani chuo wape 25% na 75% iwe ni wee mwnyw kujifua away from what you receive from lecturers.
Hapo namaanisha kucheza vizuri tu na google maana nowdays interviews haziangalii umesoma wapi instead what you knw abt your career.
 
IRDP-Institute of rural development planning kipo dodoma ila kama unapenda kusoma na kujisomea nenda pale nakufundisha wanafanya hivyo ila kama unajiona ni mzembezembe hivi usijaribu maana wao DISCO kama kawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…