Sugu kuja na wimbo mpya atakaoupa namba yake ya gerezani

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye pia ni msanii nguli na mkongwe kwenye game ya hip hop ya bongo, anatarajia kuachia kazi yake mpya hivi karibuni aliyoipa jina la namba yake ya jela, 219.

Sugu anaachia wimbo huo ikiwa zimepita siku 25 tangu alipotoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10, 2018, na kusema kwamba wimbo huo utabeba mambo mbali mbali aliyokutana nayo akiwa jela kama mfungwa.

“Maandalizi na kila kitu kipo poa na soon nitautoa wimbo wangu nilioupa jina la 219, nimeimba mimi mwenyewe na nimezungumzia hali ya nchi, experience yangu niliyoipata gerezani na mambo mengine, ni ngoma nzuri kabisa”, amesema Sugu.

Sugu amesema ameamua kuita jina hilo la namba yake ya ufungwa kwa sababu ni namba inayojulikana nchi nzima.


Mpekuzi
 
Wana HipHop tunausubiri kwa hamu kubwa kabisa!!
 
Huyo tumbo tumbo Kama vp nae atulie tu kwanza zama zake zimekwisha!!.. aimbe mambo ya jela ye amekua ndanda kosovo au nyoshi elisadaat?
 
afanye pia na 219 show series kupitia tv mbalimbali hata za kenya kama watamkubalia,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…