Sukari ikiwekwa kwenye kidonda huponya haraka kidonda na kuondoa maumivu.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Tofauti na watu wanavyofikiri kuwa chumvi ikiwekwa kwenye kidonda husaidia kuponya kidonda haraka na kukisafisha kisikaliwe na bacteria, lakini tafiti na uzoefu unaonyesha sukari ina nguvu ya kuponya kidonda na kuzuia bakteria kwa kasi zaidi ya chumvi.

Mtu anapopata kidonda bakteria kutoka nje hujikusanya na kuweka makazi kwenye kidonda na kuanza kushambuliana na seli za mwili ambazo hujitahidi kukikausha, kuua bakteria na kukifunga kile kidonda.

Sukari ya vibonge bonge inapowekwa kwenye kidonda na kufungwa na kitambaa safi hufyonza maji maji yote kwenye kidonda kwa njia ya osmosis, majimaji ambayo bakteria wananayatumia ili kuweza ku survive, hivyo kupelekea bakteria wanaoshambulia kidonda kufa hata kabla ya kushambuliwa na mifumo ya ulinzi ya mwili.

Ikumbukwe kuwa bacteria hawa hawawezi kuishi kwenye mazingira yenye ukavu.

Tayari madaktari wa Hospitali ya Selly Oak iliyoko Birmingham nchini Uingereza wanatumia njia hii ya sukari katika kutibu vidonda na majeraha ya dharura kwa haraka.

Hii ni njia ambayo askari wa Kimisri huitumia vitani wakati wa mapigano kama njia ya dharura iwapo askari amejeruhiwa kwenye mapigano na hakuna msaada wa haraka wa kitabibu.

Tofauti na chumvi ambayo ikiwekwa kwenye kidonda huleta uchungu, sukari haina uchungu inapowekwa kwenye kidonda, hali inayosaidia pia kupunguza maumivu kwa mtu aliye na jeraha au kidonda.

Dr. Mary H. McGrath, mkuu wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya George Washington University Medical Center iliyoko Washington amethibitisha hili katika tafiti zake na kwa sasa anatumia sukari kama njia ya kuponya majeraha kwa haraka.

Kwa mazingira haya ya kwetu ambapo kujikata ni kitu cha kawaida ni bora kutumia sukari kuliko chumvi.
 
Bado napata shaka na infection prevention control,vp pathophysiology ya kuzuia bacteria imekaaje...
Mwaga nondo mkuu tuelewe zaidi.
 
alternative ya sukari ni asali... hii ndo kiboko na rahisi kutumia!!! ndani ya siku chache kidonda kinakuwa kishaanza kufunga.
 
Ni kweli kabisa. Mimi nimeitumia tangu miaka ya tisini. Niliifahamu baada ya kutibiwa jeraha na bibi yangu. Tokea hapo nimekuwa naitumia kujitibu na kuwatibu wengine kwa mafanikio makubwa. Pia miaka kama minne imepita BBC WORLD SERVICE(english) waliwahi kutangaza kuwa madaktari wamegundua tiba ya sukari kutibu majeraha. USIPUUZE ETI KWA KUWA NI ELIMU YA BURE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…