Magane
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 202
- 57
Wanajamii, hali ya mauzo ya sukari ya ndani ni mbaya. Magodown ya kiwanda cha sukari cha kilombero yamejaa na sasa sukari inawekwa nje ikipigwa na jua tuombe mvua za vuli zichelewe kunusuru sukari hiyo. Je, ni kweli waliopewa vibali vya kuagiza sukari toka nje wameagiza zaidi ya ile iliyoruhusiwa na kuipiku sukari yetu ya ndani.Nasikia bei ya sukari kutoka nje bei iko chini ya ile bei ya sukari yetu ya ndani? Tunaomba wakuu wa serikali yetu walitupie macho haraka suala hili kabla wawekezaji hawajakasirika. Madhara yake ni dhahiri wafanyakazi wanaweza kukosa mishahara au kupoteza ajira. Naomba mchango wenu wanajamii.