Sukari ya ndani yakosa soko

Magane

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
202
Reaction score
57
Wanajamii, hali ya mauzo ya sukari ya ndani ni mbaya. Magodown ya kiwanda cha sukari cha kilombero yamejaa na sasa sukari inawekwa nje ikipigwa na jua tuombe mvua za vuli zichelewe kunusuru sukari hiyo. Je, ni kweli waliopewa vibali vya kuagiza sukari toka nje wameagiza zaidi ya ile iliyoruhusiwa na kuipiku sukari yetu ya ndani.Nasikia bei ya sukari kutoka nje bei iko chini ya ile bei ya sukari yetu ya ndani? Tunaomba wakuu wa serikali yetu walitupie macho haraka suala hili kabla wawekezaji hawajakasirika. Madhara yake ni dhahiri wafanyakazi wanaweza kukosa mishahara au kupoteza ajira. Naomba mchango wenu wanajamii.
 
Sababu zinaweza kuwa nyingi, moja ikiwa ni hiyo ya bidhaa kutoka nje kwa jumla kuwa zonakuwa bei rahisi kuliko bidhaa za ndani. Sababu inayoweza kufanya bei za ndani kuwa kubwa ni pamoja na kodi wanazotozwa wazalishaji na teknolojia ya uzalishaji, yaani kutumia nguvu kubwa ya uzalishaji kwa kutoa bidhaa chache na za viwango vya chini.

Katika ulimwengu huu wa ushindani, huwezi kumlazimisha mfanyabiashara na mlaji anunue bidhaa ghali za ndani wakati kitu hicho hichi kikitoka nje kinakuwa cha bei nafuu. Mfano ni saruji.

Kwa hivyo, kwa maoni yangu, suluhisho sio tu kwa serikali kuzuwia vibali vya uagizaji bali, bali kuwapunguzia kodi wazalishaji, kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa uhakika na miundo mbnu na kwa upande wa wazalishaji kutumia teknolojia ya kisasa na kutoa kuwalipa mishahara mizuri wafanyakazi wao ili kuwapa moyo wa kufanyakazi badala ya utegeaji, wizi na hujuma viwandani.
 
Safi sana,
Washushe basi bei ili soko lake lipande.
 
ni kweli bongo sukari bei, mie mwenyewe huwa naagiza malawiii kilo buku moja, nikichukua kilo25 zinanisogezea siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…