Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir Mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir

Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir Mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SULEIMAN ABDULRAHMAN SULEIMAN TAKADIR MJUKUU WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR
Mchana leo nimepokea simu aliyenipigia akajitambulisha kuwa yeye ni Mzanzibari anapiga simu kutoka Zanzibar na jina lake ni Suleiman Abdulrahman Suleiman Takadir, mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Nilidhani ni mtu ananifanyia maskhara.

Hapana.

Hakuwa ananitania.

Suleiman Abdulrahman ni mjukuu khalis wa Sheikh Suleiman "Makarios" Takadir mmoja wa masheikh waliokuwa mstari wa mbele wakati wa kuunda TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyekuwa akifungua mikutano ya TANU ya mwanzo Mnazi Mmoja kwa dua kwa kusoma Surat Fatha kisha atamtambulisha Julius Nyerere kwa wana TANU na wananchi kwa jumla.

Nilipata mshtuko.
Nimekutana na Nyota Jaha mchana kweupe.

Baada ya salamu baina yetu ni kamuuliza Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir, "Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabila gani?"

"Mshirazi."

"Una maana Sheikh Suleiman Takadir alikuwa Mzanzibari?"

"Naam babu yangu alitoka Zanzibar akaja Bagamoyo akamuoa bibi yangu mwanamke wa Kizaramo bint Mgeni kisha akahamia Dar-es-Salaam."

Nilishusha pumzi.
Mimi sikuwa na nguvu ya kudadisi zaidi.

Mzigo niliotwisha ulikuwa mzito.

Nikawa kimya nikimsikiliza yeye na shukurani zake kwangu kwa kuhifadhi historia ya babu yake ambae yeye hakumdiriki kwani yeye alizaliwa mwaka wa 1960 na Sheikh Suleiman Takadir alifariki mwaka wa 1958.

Akanambia kasoma makala zangu nyingi na kutazama video zangu.

Mwaka wa 1990 Suleiman Abdulrahman bin Suleiman Takadir akiwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Diamond Jubilee kutoka Mkoa Mjini Maghrib, Zanzibar Rais Ali Hassan Mwinyi alimshika mkono na kumjulisha kwa Julius Nyerere.

Mwalimu alipoambiwa na Rais Mwinyi kuwa huyu kijana ni mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir, Mwalimu aliomba kukiona kitambulisho chake.

Hakika jina la kijana mbele yake katika kitambulisho cha mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM lilimdhihirishia ukweli.

"Wewe usije ukawa kama babu yako," Mwalimu Nyerere alimwambia Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir.

Huu ndiyo ulikuwa usia wa Mwalimu Nyerere kwa kijana Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir, Mjumbe wa CCM kutoka Zanzibar.

Mwaka wa 1990 Suleiman Abdulrahman alikuwa na umri wa miaka 30 umri ambao Julius Nyerere alikuwanao alipojuana na Sheikh Suleiman Takadir.

Sheikh Suleiman Takadir alifukuzwa TANU mwaka wa 1958.

Historia na sababu ya Sheikh Suleiman Takadir kufukuzwa chama sasa inafahamika kwani nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Halikadhalika iko video nzima ya mkasa huu.

Suleiman Abdulrahman amenieleza kuwa baba yake Abdulrahman Suleiman Takadir alizaliwa mwaka wa 1922 na kamweleza kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa TANU na Afro Shirazi.

"Sisi hatukupata kuwa Hizbu," Suleiman Abdulrahman kanifahamisha.

Hii huenda ndiyo sababu ya yeye kuwa karibu sana na Rais Mwinyi na kupata fursa ile ya kuonana na Mwalimu Nyerere na kujulishwa kwake.

Inaelekea Rais Mwinyi aliona umuhimu wa kuwakutanisha wanachama hawa wawili wa CCM kutoka pande mbili za muungano na kutoka pia vizazi viwili vinavyopokezana kijiti.

Babu yake Suleiman Abdulrahman, Sheikh Suleiman Takadir alipigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya Sheikh Takadir alifutwa katika historia ya TANU.

Juu ya hilo historia pia haikumjua kuwa Sheikh Suleiman Takadir hakuwa Mtanganyika bali Mzanzibari.

Naangalia picha ya hawa Suleiman wawili.
Naona jinsi sura zao zilivyoshahabiana kati ya babu na mjukuu.


1727800531149.png

Suleiman Abdulrahman bin Sheikh Suleiman Takadir​

1727800625759.jpeg
 
Mh hao washirazi ni watu wa namna gani kwa sababu kuna wengine weusi sana wapo kama watu wa bara tu lakini wengine weupe na wana singa lakini wote wanajiita washirazi
 
SULEIMAN ABDULRAHMAN SULEIMAN TAKADIR MJUKUU WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR
Mchana leo nimepokea simu aliyenipigia akajitambulisha kuwa yeye ni Mzanzibari anapiga simu kutoka Zanzibar na jina lake ni Suleiman Abdulrahman Suleiman Takadir, mjukuu wa Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Juu ya hilo historia pia haikumjua kuwa Sheikh Suleiman Takadir hakuwa Mtanganyika bali Mzanzibari.
Mkuu Alama, Maalim Mohamed Said, asante kwa bandiko hili na historia hii.
P
 
Back
Top Bottom