JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Imedaiwa Mkuu wa Msafara huo ulikuwa chini ya Makamu Rais wa TOC, Henry Tandau ambaye aliwasili Uwanja wa Ndege, Saa 10:00 Alfajiri, baada ya hapo akaondoka, dakika 20 baadaye Wanariadha hao wakawasili na ndege nyingine, wakakwama kutoka baada ya mabegi yao kuelezwa yamebaki Cairo, Misri.
Nyambui ambaye alikuwa eneo la tukio akatoa msaada wa kukamilisha utaratibu wa kujaza fomu, wakafanikiwa kutoka Saa 12:00 Asubuhi, akasema “Tunafanya makosa kutopokea Mchezaji ambaye hajaleta ushindi, tumpokee hata ambaye ameshiriki na kupambana kuutafuta ushindi, naimani hawahawa ndio watafuzu kushiriki Olimpiki 2028.”