Suluhisho ajira kwa Walimu

Suluhisho ajira kwa Walimu

EMACHA

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
771
Reaction score
1,478
Hoja hizi 3 ni hakika haziwezi kubishaniwa:

1. Kwamba, kama nchi bado tunalo tatizo la upungufu wa Walimu katika shule za msingi na sekondari.
2. Kwamba, serikali haiwezi kuajiri kila mhitimu/mtaaluma wakiwemo Walimu.
3. Kwamba, mtaani kuna idadi kubwa ya vijana wasomi (wakiwemo walimu) wasio na ajira

Katika miaka ya karibuni baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Miji/Manispaa/Majiji) wamekuwa wakianzisha ama kufungua shule za msingi za mchepuo wa Kingereza(English Medium Schools); tena pengine kwa kubadilisha shule zilizokuwepo awali. Shule hizi ni za kulipia na kwa muktadha huu ni wazi serikali 'kimtindo' inafanya biashara, mbali na kutoa huduma ya elimu. Si jambo baya!

Nashauri mamlaka husika zione uwezekano wa kuingia ubia na Walimu wasio na ajira ili waweze kutumika kusimamia na kuziendesha shule za aina hiyo. Maana yangu ni kwamba; serikali iendelee kujenga au kuanzisha shule ya aina hiyo (English Medium) na kisha wachukuliwe hao Walimu wasio na ajira ili waweze kuzisimamia na kuziendesha kwa ubia kati yao na serikali.

Kwa mtindo huu tunaweza angalau kupunguza tatizo la ajira za walimu na wakati huo huo wakitoa huduma kwa Watanzania.

Nawasilisha.
 
IMG_0833.jpeg
 
Kwanini hizo course za ualimu ziendelee kuwepo wakati serikali haiwezi kuajiri.

Muulize Mkenda
 
Sisi kama serikali tumeshaamua,tutaajiri mwalimu mkuu pekee,wengine watakuwa wakujitolea na watalipwa na wananchi elfu 30 kwa mwezi
 
Back
Top Bottom