SoC02 Suluhisho la ajira kwa wahitimu wa fani za uhandisi

SoC02 Suluhisho la ajira kwa wahitimu wa fani za uhandisi

Stories of Change - 2022 Competition

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Kumaliza tatizo la ajira na kulialia ni lazima uwe mbunifu wa kutumia vyema nafasi na elimu uliyopata kuzalisha kwa namna tofauti.Ni rahisi kutumia ulichosomea kwa utofauti kwa kusoma at least FOUNDITION COURSE/FREE narudia FREE ONLINE SHORT COURSE YA AT LEAST 3 WEEKS MPAKA MIEZI MIWILI utayoambatanisha na ujuzi wako .Bila kupitia hii unaweza kufanya ila isiwe very proffesional***
Kwa miaka ya sasa ukisoma elimu kavu bila kiambatanishi ni sawa na ELIMU YAKO.

Makala hii nimeandika kwa waliosoma kozi za engineering(Mechanical,civil,agricultural nk)

(1)Ushauri na elimu ya kitaalamu:Hii itakuhitaji usome at least i course ya COUNSELLING na COMMUNICATION SKILLS.Ukiacha fani za afya,kilimo na biashara sekta ya uhandisi waliosoma wamelala sana mitandaoni na mitaani kwenye hichi kitengo.'Engineering consultation' zimekuwa zikitolewa na kampuni kubwa tu bila kujua unaweza kutoa ushauri ie kwa wale wa electrical na civil mitaani na mtandaoni.Hutapingana na mimi nikisema watu wa fani za udaktari na biashara wamepata milage kubwa sana mitandaoni,kwenye magazeti na mitaani kwa kutumia kiasi kidogo cah elimu yao kuwaelimisha ambao hawajapitia kwenye fani hizo.Natumai baada ya hii post nitaona page za vijana wengi za kutoa ushauri wa ujenzi nk msiassume watu wanajua bali wengi hawajui na hawajui pakuuliza.Unawez kupata matangazo an endorsement ya kampuni za ujenzi kupitia page yako pia.

(2)Simple Accounting(uhasibu) na manunuzi;Hii itakuhitaji usome at least 2 weeks online short course ya ACCOUNTING .Najua utashangaa mtu wa engeneering na accounts wapi na wapi.
Ila ngoja nkufundishe jambo hizi kozi za uhandisi zinaambatana na mafunzo ya muda mrefu na matumizi ya mahesabu.Hii ni moja ya advantages kama hamjajua.Watu wa aina yenu ni rahisi sana kufit sehemu zinazohitaji matumizi ya mahesabu pia kwenye procurement.Mtu wa namna hii pia ni rahisi kuajiriwa kwenye PROCUREMENT NA ACCOUNTS sector za viwanda na makampuni.

(3)Uuzaji wa vifaa vya ujenzi:Hii inakuhitaji usome at least 12 week online course ya MARKETING(pamoja na DIGITAL MARKETING). Baada ya kukamilisha hii kozi unaweza kuwa free agent wa maduka na kampuni za ujenzi.Utachokuwa unafanya ni kwenda kwa wanunuzi na kuwaelezea matumizi nafaida ya bidhaa "Kwakuwa una ujuzi nazo".Pia kwakuwa unaufahamu navyo itakuwa rahisi kuwapa machagua ukiwapambanulia ubora kwa elimu yako ya uhandisi.Hii sio kwa vifaa vya ujenzi tu mfano kwa wale wa mechanical utadeal na garage,karakana za kuchomea nk.Ukianzisha online store pia itakuwa rahisi kwakuwa kw akila bidhaa utatoa maelezo mazuri yanayovutia ukilinganisha na ambaye hajasomea.Mtu mwenye qualification hizi pia ni rahisi kuajiriwa kama marketing manager wa kampuni za ujenzi na viwanda.

(4)Usimamizi wa ujenzi au ufundi;Baada ya at least 3 weeks free online course ya MANAGEMENT especially HUMAN RESOURCE MANAGEMENT utakuwa na qualification ya either kjiajiri au kuajiriwa kusimamia ujenzi wa nyumba "za kawaida kabisa mitaani".Hata usimamizi wa karakana kwa kuwa una ufahamu na kinachofanyika.
Ngoja nikupe siri amabyo huijui kwenye kila career the highest rank mtu anataka kuwa ni kwenye MANAGEMENT kwahiyo kwa hiyo qualification utapaa moja kwa moja kwenye management bila hata ya kuwa na experience ya muda mrefu au PhD.

Narudia kukwambia nilivyokuandikia havitatimia kama hutoambatanisha na hizo online course nlizokuambia

Asilimia kubwa ya online course ni buree kabisa na nyingine zinalipiwa kuanzia dola 5 mpaka 10 mpaka course kuisha.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom