Joshua Deus
Member
- Jul 16, 2021
- 50
- 21
Umaskini ni hali ya kukosa kumudu mahitaji ya msingi kwa binadamu,mfano Chakula,mavazi na malazi.
Janga hili kwa sehemu kubwa bado Lina ikumba bara la Africa,Mwalimu Nyerere,alisema "taifa lina adui watatu ambao wanapaswa kuwatokomeza ambao ni Ujinga,maradhi,na umaskini".Kwa kiasi kikubwa ujinga kwa taifa hili umepigwa vita,watu wengi leo wamesoma na wanajua kusoma na kuandika hata Kama sio elimu ya juu,lakini imefika hatua wasomi ni wengi na ajira serikalini na sekta binafsi zimekua chache,hivyo kundi kubwa kubaki bila ajira,tumesikia viongozi wa kiserikali wakiwatupia mzigo wahitimu wa kwenda kujiajiri wenyewe.
Chanzo picha(blog ya taifa ya CMM)
Zifuatazo ni njia za kutatua Changamoto ya ajira kwa wahitimu wasio na ajira,
Kuwapa Mafunzo ya kibiashara au huduma kulingana na fani zao,
Wahitimu wengi wamekua wakifundishwa masomo kwa nadharia na kutokujua uhalisia wa soko la fani au taaluma anayo somea baada ya kuhitimu akipata nafasi ya kuajiriwa hukutana nayomaelekezo kuhusu utendaji kazi,na ni Mara nyingi unaweza kukuta muhitimu kasoma kilimo Ila hajishughulishi na utaalamu aliosomea unakuta labda Ni mtoa huduma za kifedha,na aliye somea Mambo ya fedha na benki,anakua mkulima,serikali iunde mfumo ambao utasaidia taaluma hizi wanazo soma wahitimu zilete tija kwa Taifa.
Mikopo isiyo na mashariti na riba,
Unaweza kushangaa kwanini nimesema hivi,Ila ki uhalisia kijana aliye hitimu Hana fedha ambayo inaweza kuwa Kama dhamana,wengi hawana Mali wanayoimili ili wapate mikopo ambayo itawafanya wajiajiri kulingana na taaluma zao,usipo weka vizuizi vigumu vya mikopo hii itasaidia kuokoa jahazi hili linalo zama.
Kuwahamasisha waunde vikundi vidogo vidogo kulingana taaluma zao,
Vikundi hivi vitawafanya waweze kuwajibika kufanya kazi kwa ushirikiano wakianzisha mradi wao kulingana na taaluma zao na kitu wanacho kifanya kilete tija kwa Taifa na kuwaingizia kipato hivyo kupunguza idadi ya wasio na ajira.
Kuunda mfumo ambao unafatilia wahitimu wote,
Mfumo huu uwe unahusika kufahamu Nani anafanya nin baada ya kuhitimu masomo yake,hili kuona wangapi wanapaswa kutengezewa mazingira ya ajira au kazi itasaidia taifa kua na nguvu kazi inayo wajibika na sio idadi ya watu.wasio wajibika.
Kuunda sheria mpya kuhusu masuala ya ajira
Serikali inapaswa.kutambua kila mwaka idadi ya wahitimu inaongezeka,ili kumudu idadi hii inapaswa kufany mchakato ambao utaweka ukomo mzuri wa ajira za serikalini ilikutoa nafasi kwa watu wengine muda mrefu kwa watu wale wale utafanya watu wasikie tu walicho soma ma sio kukitendea kazi.
Mifumo ya elimu kuendana na mabadiriko ya sayansi na Teknolojia,
Elimu yetu ikiwa itaendana na jinsi dunia inavyo kwenda,huenda ikatoa nafasi nyingi za ajira miongoni mwa hitimu wanahitimu elimu ya juu na Kati kila na Mafunzo ya ufundi stadi kila mwaka.
Kuanzisha mjadala wa kitaifa w kila mwaka kuhusu masuala ya ajira,
Kuanzishwa kwa mjadala huu kulete chachu ya kufanya tathimini na hatua zilizo.chukuliwa kilamwaka lukabiliana na janga hili la ajira.
Hatua hizi zisipochukuliwa Kuna athari zifuatazo.
Kuongezeka kwa magenge ya uhalifu,
Serikali isipochukua hatua watu wengi watatumia njia haramu ili kujipatia pesa ili amudu mahitaji yake,na familia yake.
Kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya,
Mtu asilo kua na kitu kinacho mshughulisha huenda ikamchochea kua na msongo wa mawazo ambao utapelekea aingie katika matumizi ya dawa za kulevya.
Kushamiri kwa biashara haramu ya ngono,
Wengi wanadhani madada poa wengi,wanapenda kufanya hiyo kazi wanafanya wengi wao Ni sehemu ya kujipatia ridhiki,serikali ikichukua mikakati madhubuti kuhusu ajira na kuwawezesha vijana kujiajiri huenda ikawa Suluhu ya Jambo hili hivyo kupunguza magonjwa zinaa.
Wahenga walisema"usipoziba ufa utajenga ukuta,bado hatuja chelewa Sana ikiwa viongozi wa umma watachukua hatua madhubuti mapema janga la ukosefu wa ajira kwa wahitimu huenda likabaki historia katika Taifa hili

Upvote
4