Suluhisho la Machinga sio kufukuzwa, mji ubomolewe

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣siku nyingine nitajitahidi,
 
Mlezi wa yote Ni ccm tengeneza tatizo tatua tatizo
Uchaguzi bado miaka 3, mwaka wa 4 vurugu za uchaguzi zinaanza. Kelele za machinga hutasikia tena, zaidi ya CCM kupaaza sauti ya kuwatetea wapiga kura wao. CCM wangewajua machinga, leo wangekuwa wanafanya biashara zao maeneo rasmi. Ni machinga wachache (na wafanya biashara kwa ujumla) wanaopiga kura.
 
Sio kimya bado sijakuelewa, wamachinga hawataki kukodi fremu wanataka kuwa mbele ya maduka ya watu sasa ukisema ujenge kwenda juu usitegemee kama kuna chinga ataenda juu
Asili ya machinga si kukodi eneo, ni watembeza bidhaa. Wakipata mitaji wanahitimu na kuwa wafanya biashara. Hawa wanaotaka kupanga vitu ni wafanya biashara wakwepa kodi, wafate sheria.
 
Mfumo wa jiji kwa bahati mbaya ni wa hovyo. Hivi kwanini mpaka leo hii, kariakoo peke yake ndio business centre ya kueleweka? Why not Mbezi, Tegeta, Mbagala, Gongo la mboto au Chanika. Kwanini kitu kinachofanana na kariakoo kisiwe goba au bunju?
 
Kwani Machinga Complex wanakopaswa kuwepo na wagombanie vizimba kumejaa??? Ili waje watande kuziba mitaa nazungumzia Kariakoo
 
Unadhani bylaws hakuna? Zipo, na sheria ya nguvu kazi haijafutwa. Tatizo utekelezaji wa sheria nchi hii unakwamishwa na wana siasa.
 
Izo Kodi watakazotozwa wakiwa kwenye hayo majengo ya biashara Bora watenge masoko pembezoni mwa mj na kama katikati ya mji basi kuwe na mgawanyiko
Ujengaji wa majengo kwa sasa utakua too expensive kwa serikali wawahamishe kwa kuwapunguza na kutengeneza market pembezoni ndio waanze KUJENGA vizuri mji kwa biashara.
 
Dada hao Machinga sikio la kufa hata ufanyaje hawawezi fuata sheria...mfano walijengewa Machinga complex pale ikiwa na ghorofa mbona hawataki kwenda?
Hilo jengo hata uwape vizimba bure, hawataingia, wao ni wachuuzi wanao wafuata watu. Ukiwazuia wamachinga kukaa eneo moja ili watawanyike, hawatakufa njaa, itakuwa ni sawa na samaki kumrudisha majini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…