Suluhisho la marumbano haya ya viongozi wa dini ni kura ya ndiyo katiba pendekezwa!!!

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
KURA YA NDIYO kwa Katiba Pendekezwa ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matamko mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini wakionyesha tofauti zao, ni vema wananchi tukaisoma Katiba Pendekezwa na kukielewa, kipengere cha Uhuru wa imani ya dini kinaeleza wazi kabisa masuala ya dini, naamini huu ndio mzizi wa tambo hizi za viongozi wa dini!!! naomba kuwasilisha.

IBARA YA 41-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.

(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali.

(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya utaratibu utakaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.

(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.

(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
 
KURA YA NDIYO kwa Katiba Pendekezwa ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matamko mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini wakionyesha tofauti zao, ni vema wananchi tukaisoma Katiba Pendekezwa na kukielewa, kipengere cha Uhuru wa imani ya dini kinaeleza wazi kabisa masuala ya dini, naamini huu ndio mzizi wa tambo hizi za viongozi wa dini!!! naomba kuwasilisha.

IBARA YA 41-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.

(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali.

(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya utaratibu utakaowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye sheria za nchi.

(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.

(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

(7) Neno “dini” kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

Nzuri hii
 
Back
Top Bottom