Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
SULUHISHO LA MGAO WA UMEME, ITAKAYOPUNGUZA GHARAMA NA MGAO
Tatizo la umeme Tanzania limekuwa na viswahili vingi kutoka kwa Mamlaka na ni changamoto kubwa inayokwamisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ukosefu wa miundombinu ya kutosha ni moja ya sababu kuu, tumekuwa tukitegema vyanzo vichache kwa miaka mingi, ambapo gridi ya taifa haifiki maeneo mengi ya vijijini na hata baadhi ya sehemu za mijini. Upatikanaji wa nishati ni wa kusuasua kutokana na kutegemea vyanzo vya umeme visivyoaminika kama maji na gesi asilia, ambavyo huathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na matatizo ya kiufundi.
Tatizo lingine ni gharama kubwa za uzalishaji na usambazaji wa umeme, zinazopelekea bei ya umeme kuwa juu kwa watumiaji wa kawaida na viwanda. Pia, wizi wa umeme na uharibifu wa miundombinu ni changamoto kubwa, zinazoongeza hasara kwa shirika la umeme (TANESCO) na kupunguza ufanisi wa huduma hiyo katika mikoa mingi nchini.
Matatizo haya yameathiri sekta mbalimbali kama vile Usafirishaji, Biashara, viwanda, elimu, na afya, ambapo shughuli nyingi hushindwa kufanyika ipasavyo bila umeme wa uhakika, Bidhaa kuaribika masokoni, Dawa kuharibika, na mengine mengi. Serikali na wadau Tunapaswa Kuongeza Jitihada ili kupata Mbinu nyine Mbadala za kutatua tatizo hili la umeme nchini.
VYANZO MBADALA VYA UMEME
-Kuvuna Umeme Wa Jua
-Umeme wa upepo
1. UVUNAJI WA UMEME WA JUA
Umeme wa jua ni aina ya nishati mbadala inayozalishwa kutoka kwenye mionzi ya jua kwa kutumia teknolojia maalum. Mchakato wa kuzalisha umeme wa jua unajumuisha hatua zifuatazo:
- Solar Thermal Systems: Hizi hutumia nishati ya jua kupasha moto kimiminika (kama maji au mafuta) ili kuzalisha mvuke ambao huendesha mitambo ya kuzalisha umeme. Mfumo huu unaitwa Concentrated Solar Power (CSP).
- Photovoltaic Cells (PV Cells): Hizi ni seli zinazobadilisha mwanga wa jua moja kwa moja kuwa umeme wa moja kwa moja (DC) kupitia mchakato unaoitwa photovoltaic effect. Paneli za jua (solar panels) hutengenezwa kwa kutumia seli hizi.
Chanzo: Picha ya Mtandaoni (verogy.com)
Gharama
za kuweka eneo la kuvuna umeme wa jua zinaweza kutofautiana kulingana na ukubwa wa mradi husika wa uzalishaji wa umeme wa jua, teknolojia inayotumika katika mradi huo, eneo la kijografia la ujenzi, na vigezo vingine vingi. Hata hivyo, hapa kuna makadirio ya jumla ya gharama kwa mradi wa kawaida wa Kuzalisha Umeme wa Jua:
Gharama za Awali
- Uchunguzi na Upembuzi Yakinifu: Hapa kuna gharama za awali zinazojumuisha uchambuzi wa eneo, mipango ya mradi, na ruhusa/Vibali. Gharama hizi zinaweza kuwa kati ya $10,000(TZS 23M) hadi $50,000(TZS 131M).
- Ununuzi wa Paneli za Sola: Paneli za sola ndizo Kiini na gharama kuu katika mradi. Gharama za paneli za sola kwa kawaida ni kati ya $0.30(TSZ 720) hadi $0.50(TZS 1,300) kwa watt. Hivyo, kwa shamba lenye uwezo wa megawati 1 (1 MW), gharama za paneli pekee zinaweza kuwa kati ya $300,000 hadi $500,000.
- Vifaa vya Msaidizi: Hii ni pamoja na inverters, miundo ya kusimika paneli, na vifaa vya uunganishaji. Gharama za vifaa hivi zinaweza kuwa kati ya $0.10 hadi $0.20 kwa watt. Kwa shamba lenye uwezo wa megawati 1, hii inaweza kugharimu kati ya $100,000 hadi $200,000.
- Ufungaji na Kazi za Ujenzi: Gharama za ufungaji na ujenzi zinaweza kuwa kati ya $0.10 hadi $0.30 kwa watt, ikijumuisha gharama za kazi za usanikishaji na miundombinu ya umeme. Hii inaweza kuwa kati ya $100,000 hadi $300,000 kwa shamba lenye uwezo wa megawati 1.
“Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania.” Chanzo: BBC
2. UMEME WA UPEPO
Umeme wa upepo ni aina ya nishati mbadala inayozalishwa kwa kutumia nguvu ya upepo kuzungusha mitambo maalum (turbines) ambayo huzalisha umeme. Turbines za upepo hupandwa kwenye maeneo yenye upepo mkali na wa kudumu kama vile maeneo ya pwani na juu ya milima.
Kwa Tanzania Tuna maeneo mengi yenye upepo mwingi n awa kudumu ambayo yaweza Kutusaidia Katika swala zima la Kumaliza tatizo la umeme na Gharama kubwa za umeme kwa wananchi wa Tanzania na Zanzibar
Turbines zinaweza Kutofautiana Gharama na ukubwa na uzalishaji wake lakini kwa gharama za kawaidi ni kama ifuatavyo:
- Makadirio ya Bei kwa Turbine za Kawaida
- Turbine ya 1 MW: $1 milioni hadi $1.5 milioni
- Turbine ya 2 MW: $2 milioni hadi $3 milioni
- Turbine ya 3 MW: $3 milioni hadi $4.5 milioni
Chanzo: Picha za mtandaoni (thyssenkrupp.com)
Tunaweza maliza Tatizo la umeme kwa Kutumia Vyanzo vingi ili kuepuka vile vyanzo vya asili kama Maji Pindi vipatwapo na tatizo au Mabadiliko ya Tabia Nchi
Upvote
8