Kocho
Senior Member
- Jun 5, 2013
- 120
- 21
Baada yakufanya utafiti na kuchambua mazingira yaliyosababisha Tanganyika na Zanzibarkuungana, hasa kutokana na mvutano wa ukomunisti na ubepari katika enzi za vitabaridi, ambapo Zanzibar iliitwa Cuba ya Afrika na kuitia hofu kubwaMarekani, huku Tanganyika ikikumbwa na maasi kati ya Januari 20-27, 1964na Zanzibar kufanya mapinduzi Januari 12, 1964; inaeleweka kabisa kwaniniTanganyika iliungana haraka sana na Zanzibar.
Tanganyikailikuwa na miaka miwili na miezi minne tu baada yakupata uhuru Desemba 9, 1961. Zanzibar ilikuwa na miezi mitatu tubaada ya kufanya mapinduzi, na miezi minne tu baada ya uhuruDesemba 10, 1963. Nchi zote mbili hazikuwa shwari na zilikuwa hazijakomaa nakupata utulivu wa kisiasa huku zikisukwasukwa nje ndani. Na kama tunakumbukaAbeid Amani Karume aliwatupia kwenye muungano kwa Mwalimu Nyerere wanamapinduziwaliokuwa na mrengo wa kikomunisti akiwemo Babu, Kasim Hanga, Twala, Salim, nk.
Baada yakuuona muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa upekee, si kwaubora au uhusiano mzuri, bali wa upekee kwa utata wake ambaowengine wamezoea kuita kero za muungano ambazo hazijaisha baadaya miaka takribani 50, naamini utata au kero hizi zitaendelea kuwepo.
Mbaya zaidiimekuwa kama ni uasi kuhoji muungano maana wengine wamekumbwa na adhabu kali yakutengwa au kufukuzwa kwenye serikali na chama. Mwaka 1984 alifukuzwa AboudJumbe aliyechangia sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na chama kimojacha siasa akikubali kufuta ASP Zanzibar waungane na TANU Tanganyika kuunda CCM1977. Baada ya hapo nilitarajia tungepata serikali moja ili kuunganisha kabisanchi mbili zilizoungana kwa mambo machache tu.
Baada yakuona kimahesabu huwezi kuunganisha vitu viwili vikabakia viwili,kitakuwa kitu kimoja kizima au zaidi ya viwili kama ambavyo kwa sasa tunaserikali tatu ingawa tumeeneza kwamba ni mbili wakati kiuhalisia ziko serikalitatu: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mambo ya muungano,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika ambayo inajifichakwenye mambo ya muungano au wengine wamebadili jina kiholela na kuita TanzaniaBara.
Huwezikuwaoza mwanamke na mwanaume ukawa na ndoa mbili. Itakuwa ndoa moja tu.Ukiunganisha maumbo mawili unapata moja au kama yameungana kwa sehemu tuunapata maumbo matatu: kiunganiko (intersection set) na sehemumbili ambazo hazijaunganika. Wengine wanasema moja na moja ni mbili na si tatu,lakini je utabaki vipi na vitu viwili tena endapo umeviunganisha?Hazikujumlishwa nchi mbili bali ziliungana! Kulikuwa na Ujerumani mbili(magharibi na mashariki), baada ya kuungana ni Ujerumani moja tu.
Miaka yotetokea mwaka 1964 baada ya muungano tuna mamlaka za aina tatu. Niseme ukwelikuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba haijaleta muundo wa serikali tatu baliimeutambua na kuuelezea vizuri uliopo. Ninachosema ni kwamba Rais wa Jamhuri yamuungano ana kofia mbili kiserikali ndiye pia Rais wa Tanganyika. NasisitizaTanganyika kwa kuwa hatujawahi kuwa na upande wa muungano unaoitwa TanzaniaBara. Zanzibar iliungana na Tanganyika na si Tanzania Bara, na nyaraka zote zamuungano zinadhihirisha hivyo hadi leo.
Utafitiwangu unabainisha kuwa Tanganyika na Zanzibar hazikufuta hadhi ya kuwa nchiisipokuwa tu katika masuala ya muungano. Kwa miezi kadhaa baada ya kuungana,nchi ya muungano iliendelea kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar hadi pale ambapo mshindi wa kutunga jina moja la muungano (IsmailAkbar) alipounganisha TAN kutoka herufi tatu za mwanzo za Tanganyikana ZAN kutoka herufi tatu za mwanzo za Zanzibar, na kumaliziavifupisho vya majina yake mawili vya I (Ismail) na A (Akbar)na kupata TANZANIA.
Unapotaja TANZANIAunataja mambo ambayo ni ya muungano, yanayobaki yanakuwa ya nchi ya Zanzibarupande mmoja wa muungano na nchi ya Tanganyika kwa upande mwingine. Hadileo hakuna mahali popote ambapo jina Tanganyika lilifutwa rasmi na kuwekwa jinalingine. Na hadi leo Hati ya Muungano ndio mkataba pekee ulio haikuhusiana na muungano wa nchi mbili. Wanaoita Tanganyika kuwa ni Tanzania Barawanakosea sana kwa kuwa hatujawahi kubadili rasmi jina la Tanganyikakuwa Tanzania Bara. Wengine kiholela wanaita Bongo wakatiTanganyika haijawahi kuitwa Bongo ni majina ya mitaani tu!
Hatatungekubaliana kisheria bado tungekosea kuiita Tanganyika Tanzania Bara kwakuwa pwani yote (Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga namaziwa) haiko bara! Aidha visiwa vya Mafia, Songosongo, Koma, Kwale,Ukerewe na vingine haviko bara!
Nisisitizekuwa, hali halisi na muundo halisi wa kiutendaji uliopo sasa tangu Aprili 26,1964 ni wa serikali tatu: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Tanganyika ambayoinajificha kwenye jina la Tanzania au Tanzania Bara. Wengine wanasema serikaliza mitaa ni serikali ya nne! Tunawajibika kwa aina nne za serikali. Ni ukweliusiopingika! Nenda kwenye halmashauri uone waliotuna na kuvimba na mamlaka zao.
Pia kuna watuwalijitungia kienyeji kwa kubadili jina la Zanzibar na kuita TanzaniaVisiwani bila kujua kuwa hata visiwa vya Ukerewe na Mafia ni TanzaniaVisiwani lakini haviko Zanzibar! Na waliendelea kutapatapa tena kwa kuiitaZanzibar Tanzania Zanzibar na wengine wanasema Zenj wakati niZanzibar na ndiyo jina halali na rasmi lililomo kwenye hati ya muungano.Kubadili jina la nchi kunahitaji tamko rasmi la mamlaka iliyopo au kupatamwafaka wa wananchi wote.
LaurentKabila alitamka rasmi kwamba iliyokuwa ikiitwa Zaire itaitwa Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo; iliyokuwa ikiitwa South West Africa ikaitwa Namibia;Abyssinia ikawa Ethiopia, Upper Volta ikawa Burkina Faso, Gold Coast ikawaGhana, na kwingineko kwa tamko rasmi. Jina la nchi haliibuliwi mitaani au bilamamlaka rasmi.
NashukuruWazanzibar daima huita nchi yao kwa jina rasmi la Zanzibar. Nisisitize pia kuwamambo yote yasiyo ya muungano yanashughulikiwa au kusimamiwa na Zanzibar auTanganyika. Kusema masuala yasiyo ya muungano ni ya Tanzania kwa upande waTangayika ni makosa kwa kuwa si ya muungano, maana Tanzania ni kwa ajili yamasuala ya muungano tu ikiwemo Zanzibar! Huenda ndiyo maana kuna malalamikokuwa Tanzania imemezwa na Tanganyika na kuiacha Zanzibar kando.
FikiriaWaziri wa Elimu aliyeko Tanganyika anajiita Waziri wa Tanzania wakati elimu sisuala la muungano! Na hata nyaraka zote za mambo yasiyo ya muungano kwa upandewa Tanganyika zinachukuliwa kama vile ni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kumbe si ya muungano bali ya Tanganyika pekee ingawa wakati mwingine huitwa yaTanzania Bara. Wanaodai tuna serikali mbili, je, ya Tanzania Bara inatokawapi?!
WenzetuZanzibar wanakwenda sawia na unavyosema mkataba almaarufu Hati ya Muungano nawako wazi sana katika kufuata mkataba huo na kuulinda. Ndiyo maana hadi leotuna sikukuu za aina tatu: uhuru wa Tangnyika wa Desemba 9, mapinduziya Zanzibar ya Januari 12 na Muungano wa Aprili 26.
Tanganyikailikuwa na umri wa miaka miwili na miezi minne tu ilipoungana naZanzibar kwa mambo 11 tu (sasa yako 22) tangu ilipopata uhuru Desemba9, 1961. Zanzibar ilikuwa na umri wa miezi minne tu na siku kadhaatangu ilipopata uhuru Desemba 10, 1963, na na umri wa miezi mitatutu tangu ilipofanya mapinduzi Januari 12, 1964, ambayo ndiyo huenziwa.
Leo hiihatuwezi kujigamba kwamba Zanzibar imefaidika na muungano kwa kuwa haikuishimuda mrefu nje ya muungano (miezi mitatu tu) na kuzitumia vizuri fursa zakitaifa na kimataifa. Na Tanganyika pia haikuishi muda mrefu nje ya muungano(miaka miwili tu na miezi minne). Hapo hatuwezi asilani kupata ulinganifuwenye urari kwa kuwa nchi zote zilikuwa bado changa kiasi ambacho hatujuiTanganyika na Zanzibar zingenufaika vipi kama zingedumu miaka 50 zikiwa hurukabisa zenye mamlaka kamili ya kidola (sovereign states).
Kuendeleakudai kuwa Tanzania kuna serikali mbili wakati hali halisi kiutendaji niserikali tatu ni kuwadharau wananchi na uchambuzi huu wa kweli. Mwalimu Nyererealiwahi kusema ukimwambia mtu mzima ukweli unamheshimu, lakini ukimwambia uongounamdharau. Na aliwahi kukiri kuwa haikuwezekana kwa yeye kufanya yote mazurikatika utawala wake wa miaka 23.
Najua mengimazuri aliyofanya Mwalimu na namuenzi, lakini suala la muungano lilimsumbua nakushindwa kupata ufumbuzi wa kweli labda kwa kuwa alitamani kuishia na serikalimoja kama ambavyo alifanikiwa kuwa na chama kimoja nchi nzima. Hata hivyo,Wazanzibar wamekataa katakata kufuta historia ya nchi yao yenye umri mrefukuliko Tanganyika na Tanzania.
Suluhishola Kudumu la Muungano Bora wa Tanganyika na Zanzibar
(b)Kugawanya madeni ya nje kulingana na uwiano halisi wa jinsi yalivyotumikakusaidia nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
(c) Kuratibu balozi za nje ili ziendelee kutumiwa pamoja kiofisi (sharedconsulates) kwa Tanganyika na Zanzibar hadi wakati ambapo uwezo wa kilanchi utaruhusu kuwa na ubalozi wake.
(d)Kuratibu fedha na/au sarafu za aina moja ili ziendelee kutumika kihalali katiya Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha uhusiano na utambulisho wa kihistoria.
Nikiwamwanafunzi wa Mwalimu Nyerere nihitimishe kwa kusema alichokataza ni kufukuzanabaina ya Watanganyika na Wazanzibar. Akaita dhambi kubwa sawa na kula nyama yamtu. Hakukataza maelewano na makubaliano ya amani. Na sitegemei watuwanaokubaliana kwa amani watapigana. Wala si sahihi kulinganisha hilo na Sudanambao walipigana miongo kadhaa wagawane nchi.
Wakati vitavya Uganda na Tanzania vikielekea ukingoni kabisa Mwalimu Nyerere alilaumiwakuwa anataka kuimeza Uganda, wengine wakidiriki kusema kama alivyoimezaZanzibar. Yeye alijibu kuwa lililo la msingi ni kudumuisha amani na nchi jiranina kuwa na uhusiano mwema si kuunganisha nchi. Tubakie majirani wema kamailivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusianomema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi.
Kuna nchinyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani, sembuseZanzibar na Tanganyika! Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi. Naujirani na udugu wa kihistoria upo kwa nchi zote tunazopakana nazo na siTanganyika na Zanzibar pekee.

- Watu wa Tanganyika wenye makazi ya kudumu Zanzibar na Wazanzibar wenye makazi ya kudumu Tanganyika, wapewe uhiari, haki na uraia wa kuendelea kuishi Zanzibar au Tanganyika mtawalia.
- Endapo Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwa na uraia wa nchi moja, basi nchi hizi mbili ziwe na makubaliano maalum ya uraia maalum wa nchi mbili (Duo Exclusive Treaty on Special Dual Citizenship) kwa Watanganyika na Wazanzibar ambao watahiari kuwa na uraia wa nchi mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar pekee.
- Tanganyika na Zanzibar ziwe madola huru kama ilivyokuwa kabla ya muungano na zijiunge katika jumuiya au taasisi mbalimbali za kikanda au kimataifa ikiwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), FIFA, nk.
- Pasiwepo viza ya kusafiria kati ya Tanganyika na Zanzibar isipokuwa vitambulisho vya uraia au hati za kusafiria (passports) zitumike kumtambua Mtanganyika au Mzanzibar.
- Iundwe Tume ya Mahusiano na Ujirani Mwema baina ya Tanganyika na Zanzibar (Commission for Relations and Good Neighbourhood). Tume hii pamoja na mambo yatakayojitokeza, ifanye yafuatayo: