The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kundi la vijana wasio na ajira rasmi linaongezeka kwa kasi kubwa sana, kila kukicha wanakuwa wengi leo kuliko jana.
Mzee kikwete alikuja na ufumbuzi eti wa kujenga machinga complex ambayo matokeo yake haijapunguza tatizo hata tone moja.
Namuona rais wa sasa anajaribu kupitia njia ileile eti kujenga soko, ukweli ni kwamba hata ungejenga soko la kuchukua machinga milioni moja sioni kama unaweza kumaliza changamoto ya machinga.
Badala ya kuhangaika na machinga huku mitaani nakushauri serikali kama ipo serious na swala la machinga basi wawekeze nguvu nyingi sana huko wanakotokea hawa vijana. Yaani wawekeze zaidi kwenye kilimo ili kivutie vijana lakini pia wabadili elimu ili ilenge kuzalisha wazalishaji!