Nimefuatilia yanayoendelea Lindi na Mtwara na hoja za Serikali pamoja na wadau mbalimbali nikagundua serikali inataka kupingana na ukweli tu bila sababu. Nimeshindwa kuelewa maana ya kauli ya serikali kwamba mali zinazogundulika sehemu yoyote ya nchi hii ni mali za Watanzania wote. Hao Watanzania wote maana yake nini na ni akina nani hao Watanzania wote!!?? Maana sijaona namna madini, misitu, pembe za ndovu zilivyotunufaisha hasa mimi binafsi zaidi ya kila siku kusikia tuhuma za ujangili, ufisadi, mikataba mibovu n.k na ubaya wanaotajwa katika tuhuma na kashfa zote hizi ni kikundi kilekile cha watu au hicho ndio kinakula halafu Watanzania wote tunashiba??. Sera ya Majimbo ndio suluhisho. Natamani Wasukuma, Wachaga, Watu wa nyanda za juu kusini, Kanda ya ziwa, Arusha na wote ambao rasilimali zao zinavunwa na hiki kikundi kinachojiita Watanzania wote tuamke na kuwashika mkono na ikibidi tuipake mikono yao kwenye mchanga ili wasiendelee kula tena la sivyo wtamaliza kila kitu maana hawashibi. Hawa ni madalali wan chi yetu na ndio maana wanapeana tu vyeo kwenye Chama na Serikali ili wawe na kinga na kujihakikishia usalama. Tuamke Watanzania. Wanapoonewa wa Mtwara tuwaunge mkono maana kesho itakuwa zamu ya watu wa Bahi, na Watanzania wengine kwa niaba ya Watanzania wote.