UTANGULIZI
Ongezeko la mahitaji ya taulo za kike limekuwa kubwa kutokana na elimu ya umuhimu wa kutunza afya kwa wasichana na wanawake ambayo imekuwa ikitolewa nchini Tanzania kwa njia mbalimbali. Pamoja na ongezeko hilo la mahitaji ya taulo gharama yake imekuwa ni mwiba kwa watumiaji hasa wale wa kipato cha chini hivyo kupelekea kushindwa kumudu gharama hizo na kuwafanya wasichana na wanawake kutumia njia nyingine za kujisitiri ambazo si salama kwa afya zao pindi wanapokuwa katika siku zao za hedhi. Pia kwa wanafunzi imekuwa ikipelekea kutohudhuria masomo katika kipindi hiki. Aidha tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu binafsi au taasisi zikitoa misaada ya taulo za kike kwenye baadhi ya maeneo jambo ambalo ni zuri na linalenga kupunguza makali ya gharama hizo kwa walengwa. Lakini swali la kujiuliza ni je misaada hii hudumu kwa kipindi cha muda gani kwa walengwa? Hedhi ni kipindi ambacho msichana au mwanamke hupitia kila mwezi na hivyo kama msichana huyu atapokea msaada wa taulo maramoja kwa mwaka, maana yake hili si suluhisho la kuondoa changamoto ya taulo za kike. Hivyo ili kutatua changamoto hii tunahitaji suluhisho la kudumu kwa wasichana na wanawake wote nchini.
SULUHISHO
Ili kutatua changamoto ya taulo za kike nchini, Halimashauri zote nchini zinaweza kutenga bajeti ili kuweka mashine za kuuzia taulo kwa njia ya koini (Automatic Sanitary napkin Vending machine) katika maeneo yote yenye mikusanyiko kama vile Shule, stendi za mabasi, Hosipitali, Katika masoko na maeneo mengine.
Sambamba na kuwepo kwa mashine hizi, pia tunahitaji kuzingatia usafi wa mazingira kwani muhimu sana. Hivyo kutakuwa na ulazima wa kuweka machine zitakazo tumika kutupa taka ili kusaidia katika kutunza mazingira yetu, kwani bila kufanya hivyo uchafuzi wa mazingira utakuwa kwa kiwango kikubwa sana.
UMUHIMU NA FAIDA ZA AUTOMATIC SANITARY NAPKIN VENDING MACHINE
Mradi huu ni muhimu na wenye faida kubwa hasa kwa wasichana na wanawake lakini pia utakuwa na faida kwa Halimashauri zetu kwa kuongeza mapato yake. Faida watakazo pata wasichana na wanawake ni kama zifuatazo:
UTEKELEZAJI
Mapendekezo yangu mradi huu uweze kutekelezwa na Halimashauri kupitia mapato yake ya ndani ili kuharakisha utekelezaji.
Serikali ifute kodi na tozo zote katika material yanayotumika kutengeneza taulo za kike
Pia wasambazaji au msambazaji wa mashine na taulo za kike apatikane zabuni ili kulinda ubora na kuhakikisha ufanisi wa mradi.
USIMAMIZI:
Kama ilivyo miradi mingine mradi huu pia unahitaji usimamizi na ufuatiliaji wa karibu ili kuleta ufanisi mkubwa. Kwakuwa mradi huu utatekelezwa na Halimashauri, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum iweze kusimamia mradi huu ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Endapo mradi huu utaachwa chini ya usimamizi na ufuatiliaji wa halimashauri pekee, ufanisi wake unaweza kuwa ni mdogo sana pengine hata kushindwa kutekeleza kabisa.
LENGO LA WAZO HILI
Pengine naweza kuwa tofauti na mawazo ya walio wengi ya kuwamba taulo za kike zitolewe bure bila malipo. Hili ni wazo zuri na linalengo la kuondoa adha kubwa wanayopitia wasichana na wanawake katika kipindi cha hedhi. Lakini tujiulize je taulo hizi zikitolewa bure bila malipo zitawafikia walengwa? Inawezekana kabisa taulo hizi zikatolewa bure na serikali lakini zisiwafikie walengwa hasa walioko vijijini.
Wazo hili limelenga kutatua changamoto ambazo wanapitia baadhi ya wasichana na wanawake kipindi cha hedhi kwa maeneo yote nchini. Changamoto hizi ni pamoja na upatikanaji wa taulo za kike na bei yake kuwa juu sana. Hivyo Imani yangu kubwa ni kuwa kupitia wazo hili tutaweza kupunguza changamoto hizi.
Pia wazo limelenga kulinda afya za wasichana na wanawake kwani hedhi salama ni njia muhimu ya kupunguza na kuondoa magonjwa yanayosababishwa na hedhi isiyosalama kwa wasichana na wanawake.
MWISHO
Hedhi Salama kwa wasichana na wanawake wote nchini inawezekana.
Ongezeko la mahitaji ya taulo za kike limekuwa kubwa kutokana na elimu ya umuhimu wa kutunza afya kwa wasichana na wanawake ambayo imekuwa ikitolewa nchini Tanzania kwa njia mbalimbali. Pamoja na ongezeko hilo la mahitaji ya taulo gharama yake imekuwa ni mwiba kwa watumiaji hasa wale wa kipato cha chini hivyo kupelekea kushindwa kumudu gharama hizo na kuwafanya wasichana na wanawake kutumia njia nyingine za kujisitiri ambazo si salama kwa afya zao pindi wanapokuwa katika siku zao za hedhi. Pia kwa wanafunzi imekuwa ikipelekea kutohudhuria masomo katika kipindi hiki. Aidha tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu binafsi au taasisi zikitoa misaada ya taulo za kike kwenye baadhi ya maeneo jambo ambalo ni zuri na linalenga kupunguza makali ya gharama hizo kwa walengwa. Lakini swali la kujiuliza ni je misaada hii hudumu kwa kipindi cha muda gani kwa walengwa? Hedhi ni kipindi ambacho msichana au mwanamke hupitia kila mwezi na hivyo kama msichana huyu atapokea msaada wa taulo maramoja kwa mwaka, maana yake hili si suluhisho la kuondoa changamoto ya taulo za kike. Hivyo ili kutatua changamoto hii tunahitaji suluhisho la kudumu kwa wasichana na wanawake wote nchini.
SULUHISHO
Ili kutatua changamoto ya taulo za kike nchini, Halimashauri zote nchini zinaweza kutenga bajeti ili kuweka mashine za kuuzia taulo kwa njia ya koini (Automatic Sanitary napkin Vending machine) katika maeneo yote yenye mikusanyiko kama vile Shule, stendi za mabasi, Hosipitali, Katika masoko na maeneo mengine.
AUTOMATIC SANITARY NAPKIN VENDING MACHINE
Source: Riya INC
Jambo hili litasaidia kurahisisha upatikanaji wa taulo hizi za kike kiurahisi na kwa gharama nafuun kwa wakati wote kwani taulo hizi zinaweza kuuzwa kwa koini ya shilingi miambili (100) za kitanzania tofauti na ilivyo sasa kwani taulo hizi zinauzwa kuanzia shilingi 2000 kwa pakiti katika maeneo mengi nchini. Wanawake wengi nchini hasa wale wenye kipato cha chini huendesha Maisha yao kwa kutegemea kipato cha kila siku hivyo hupata ugumu kumudu mahitaji yote ikiwemo taulo za kike ambazo huuzwa kuanzia shilingi 2000. Lakini kama mpango huu utakuwepo utasaidia kuwawezesha na wao kupata hitaji hili wao pamoja na Watoto wao wa kike.Sambamba na kuwepo kwa mashine hizi, pia tunahitaji kuzingatia usafi wa mazingira kwani muhimu sana. Hivyo kutakuwa na ulazima wa kuweka machine zitakazo tumika kutupa taka ili kusaidia katika kutunza mazingira yetu, kwani bila kufanya hivyo uchafuzi wa mazingira utakuwa kwa kiwango kikubwa sana.
SANITARY NAPKIN DESTROYER
Source: Riya INC
Source: Riya INC
UMUHIMU NA FAIDA ZA AUTOMATIC SANITARY NAPKIN VENDING MACHINE
Mradi huu ni muhimu na wenye faida kubwa hasa kwa wasichana na wanawake lakini pia utakuwa na faida kwa Halimashauri zetu kwa kuongeza mapato yake. Faida watakazo pata wasichana na wanawake ni kama zifuatazo:
- Kurahisisha upatikanaji wa taulo hizi hasa katika maeneo ya mikusanyiko
- Kupata taulo hizi kwa bei ya chini Zaidi
- Kulinda afya za wasichana na wanawake kwa kuwakinga na magonjwa yatokanayo na hedhi zisizo salama.

Upvote
1