Mtambo 1272019
Member
- Jul 29, 2022
- 16
- 15
SULUHU MBADALA YA UKOSEFU WA AJIRA NCHINI TANZANIA
Maana ya ukosefu wa ajira.
Kwa maana ya kawaida na inayoeleweka na wengi. Ukosefu wa ajira humaanisha kitendo au hali ya mtu kukosa au kutokuwa na shughuli(kazi) rasmi ya kumuingizia kipato. Neno “ Ukosefu wa ajira “ imekuwa wimbo wa ulimwengu, na wimbo wa mataifa mengi yanayoendelea ikiwemo Tanzania.
Ukosefu wa ajira umechagizwa haswa na hali ya uwepo wa rasilimali watu wengi,ambao wanataka na wako tayari kufanya kazi,lakini sekta zinazoajiri zikiwa chache ukilinganisha na idadi ya wahitaji wa ajira/kazi husika.
Kutokana na janga hili kukua kwa kasi ,limechagiza uongezekaji wa vitendo wa kiarifu (uwizi,mauaji,uporaji),msongo wa mawazo,usitishwaji wa masomo kwa wanafunzi(morali ya shule kuporomoka),, na ukuaji wa matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya kwa vijana na wahitimu wengi wa elimu ya chuo.
Hivyo basi ,tatizo la ukosefu wa ajira lingefaa kutazamwa kwa jicho la tatu, na kupatiwa suluhu endelevu ya kupunguza tatizo husika kwa kiwango cha juu.
Nini kifanyike kutatua ukosefu wa ajira?
Ningependa kutoa mtazamo wangu juu ya ukosefu wa ajira na kupendekeza mambo kadhaa kufanywa na mtu mmoja mmoja, taasisi binafsi na serikali kiujumla, ambayo yanayoweza kupunguza janga hili baya la ukosefu wa ajira.
Mfumo na mtaala wa elimu urekebishwe/uboreshwe ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira . mfumo na mtaala wa elimu tangu kipindi cha mkoloni hadi sasa umekuwa ukiwaandaa wahitimu kuajiriwa kuliko kujiajiri. Hii imechangiwa sana na masomo mengi kufundishwa kwa nadharia tu, hivyo wanafunzi wengi hujikuta hawana uwezo wa kubadili nadharia husika kwenda kwa vitendo. Kwa mfano mtu anasoma masomo ya kilimo,uchumi,sayansi n. lakini baaada ya kuhitimu shule hana uwezo wa kulima,kubuni mawazo bora ya kilimo na kuyatendea kazi, aliyesomea uchumi. Pia hana hata uwezo wa kuanzisha biashara ,au kuibua wazo bora la kibiashara au hata kuweza kutoa suluhu kadhaa za biashara husika.
Vilevile, lazima kila daraja la elimu(shule ya msingi,sekondari na chuo) lijitosheleze kimaarifa na kiujuzi ili mwanafunzi akiishia daraja fulani aweze kutumia maarifa n aujuzi husika katika maisha yake halisi. Hivyo kama taifa tujitathmini katika hili, elimu apatayo mwanafunzi lazima iweze kumsuka(kumuandaa) vyema ili aweze kukabiliana na changamoto za kimaisha, sambamba na kuweza kutumia maarifa na ujuzi aliopata akiwa shuleni/vyuoni kubadili maisha yake .hii itapunguza idadi ya wahitimu wanaowaza na kusubiri kujiajiri, badala yake watajiingiza kwenye sekta binasi na kufanya makubwa.
Vipaji (taranta) vya watoto vitunzwe na viendelezwe. Nielewavyo ni kuwa kila binadamu amezaliwa na kipaji (taranta) yake. Lakini mfumo wa maisha,na mfumo wa elimu umechangia kwa ukubwa kuua vipaji vya watoto wengi kuliko kuviendeleza. Yaani wazazi,jamii na serikali zimewafanya watoto na wananchi wengi kudharau na kupuuza sana vipaji wa watoto wengi.
Jambo hili ningependekeza litazamwe kwa kina kwani dunia ya sasa kipaji kina uwezo wa kufanya mabadiliko makubwa kuliko ifikiriwavyo. Kwa mfano, jaribu kufikiri watu maarufu kama Diamond platnum, Ali Kiba, Hasheem Thabit,Mbwana Samata, ,Harmonize, na wengine wengi, wangelikuwa wapi kama wasingalikuwa na kuendelezwa vipaji vyao, fikiri pia hao watu wameajiri watu wangapi?. Hivyo basi, wazazi,jamii na serikali lazima ibadili mtazamo wake juu ya vipaji. Vipaji ni tunu, vitunzwe na viendelezwe.
Kozi (somo) la ujasiriamali liwe la lazima katika ngazi zote za elimu. Miaka ya sasa, elimu ya ujasiriamali inatolewa na baadhi ya vyuo vya kati na juu, na ni somo la hiyari kwa baadhi ya vyuo. Lakini shule nyingi na vyuo vingi havitoi elimu hii katika nchi yetu. Lakini pia, elimu ya ujasiriamali imekuwa ikitolewa kwa ukubwa na taasisi/asasi binafsi kwa malipo,hivyo basi kuna ulazima wa wizara ya elimu,sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na serikali kufikiri juu ya ulazima wa somo /elimu ya ujasiriamali kiuwa ya lazima na itolewe bila malipo. Hii itachangia wahitimu wengi kuwa na “mindset” ya kiubunifu hata baada ya kuhitimu masomo yao.
Somo la stadi za kazi lifufuliwe na liboreshwe kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kwa miaka mingi sasa, somo la stadi za kazi limepuuzwa na kupewa hadhi ya chini katika elimu ya mwanafunzi.vilevile ni somo ambalo mwanafunzi ameamuliwa kutojibia mtihani wa taifa wa darasa la saba. Lakini ukweli ni kuwa , somo hili lina umuhimu mkubwa katika kukuza na kunoa uwezo wa kujitegemea na ubunifu wa mambo au vitu mbalimbali.
Kipindi tupo shule ya msingi, tulijifunza kutengeneza vyungu, ususi,ujenzi(ufundi washi), na kutengeneza vitu mbalimbali kuendana na mazingira yetu, ingawaje somo hili lilikuwa bado halijapewa kipaumbele na lilifundishwa kimazoea tu pasipo walimu wabobevu katika fani husika. Hivyo ningependekeza, somo la stadi za kazi lirudishwe mashuleni,liboreshwe kuendana na dunia ya sasa,lipewe kipaumbele, liwe la lazima na l;ihusike kwenye mitihani wa taifa(darasa la nne na saba), na mwisho, walimu wenye mafunzo ya ufundi wahusishwe katika somo hili ili kuleta tija. Endapo ufundishwaji wa somo hili utachukuliwa kwa umakini, na utasimamiwa na walimu wenye mafunzo toshelevu, naamini kuwa linaweza kuleta matokeo chanya na kuwa sehemu ya suluhu ya ukosefu wa ajira, kwani wahitimu wanaweza kujiendeleza kwenye fani husika, na kutumia maarifa na ujuzi walioupata katika somo husika kwa kwenda kujitegemea.
Kwa kumalizia ,ningependekeza vijana, jamii na serikali kuwa na hali ya uthubutu hii kwasababu ya kuwa yote uyaonayo ulimwenguni, yamechochewa na hali ya uthubutu ya watu kadha. Vijana lazima tuondokane na uoga wa kufanya mambo mapya(ikiwemo na kujiajiri), lakini pia jamii, na serikali kiujumla zinapaswa kuthubutu kufanya mabadiliko chanya katika mifumo yake mbalimbali kwaajili ya manufaa ya kizazi cha leo na kesho. Wanasiasa waache kulinda maslahi yao,kila wasikiapo wazo jipya la kufanya mabadiliko .
RUSHWA NI CHA CHA UKOSEFU WA AJIRA,TUPAMBANE KUITOKOMEZA.
Upvote
1