Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 489
Kwa kipindi kirefu tumekuwa na mifumo ya elimu katika shule zetu isiyokuwa na tija, nasema isiyokuwa na tija kutokana na ukweli kuwa mwanafunzi amekuwa akirundikiwa rundo la masomo hata yale ambayo yeye mwenyewe hana usongo nayo. Kwanini umlazimishe mwanafunzi kusoma masomo kumi wakati yeye anataka mu-specialize katika masomo ambayo yamo ndani ya uwezo na moyoni mwake?!
Ili kupata suluhu ya haya, ifike wakati sasa Serikali itenge shule zinazoendana na combination ya masomo husika. Kama ni shule za Arts, zijulikane, shule za Sayansi zijulikane, vivyo hivyo hata katika categories nyingine zijulikane. Mpango wa namna hii utaiwezesha serikali kujua aina ya wataalamu iliyonao wapo wapi na wanafanya nini, pia itasaidia kuongeza tija katika sekta nzima ya elimu. Hivi kuna ugumu gani kufanya hivyo kama ugumu haupo katika vichwa vyetu ambavyo vimechoka kufikiri?!! Nisome pia: saimon wamiwa katika facebook