SoC02 Suluhu ya mauaji na ukatili Tanzania

SoC02 Suluhu ya mauaji na ukatili Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Ntaganda boy

Member
Joined
Jan 16, 2016
Posts
90
Reaction score
59
SULUHU LA MAUAJI NA UKATILI TANZANIA

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo kila kukicha kuna tukio jipya la Ukatili au Mauaji au kujiua.

2021 pekee vifo zaidi 470 vya Watanzania chanzo chake ni ukatili na kujuondoa uhai, taarifa waliyochapisha LHRC May 31 2022.

Kuna vitendo zaidi ya 42,414 vya ukatili kwa mwaka 2021. Kumaanisha kuwa kuna ongezeko la idadi ya watu na Watoto wanaofanyiwa ukatili kwani kwa mwaka 2020 visa vya ukatili vilikua takriban 30,000. Tukumbuke si wanawake wala Watoto tu wanaofanyiwa ukatili pekee bali pia na wanaume japokua ukimya katika kutoa taarifa ndio huficha Habari zao na raiti wanaume wakianza kutoa taarifa basi idadi ingekua maradufu ya takwimu zilizopo kwa sasa.

Kuanzia Januari 2022 hadi Julai 2022, kuna zaidi ya matukio 100 yameripotiwa na vyombo vya habari juu ya kuuana au kujiua(kujiondoa uhai). Kuna mikoa inatajwa kama kinara katika Habari hizi, mfano Mwanza, Geita, Iringa, Dar es salaam na hivi karibuni imeripotiwa Kigoma kwa tukio la familia moja kuuliwa na Dodoma kwa visa vya mapenzi. Kwenye vyombo vya Habari hasa Habari za mauaji Jiji la Mwanza na Mkoa wa Geita ni vinara kusikika, hali hii inazua taharuki kwa wakazi wa mikoa hiyo lakini zaidi kwa wageni ambao wanaamini kuwa wakazi wa mikoa hiyo ni wakarimu Zaidi.

Kila Mtanzania anafikilia chanzo na njia ya kuondoa changamoto hizi.

SULUHU

Tendo la ndoa (Kileleni)

Kuna Watanzania wengi sana wanachangamoto katika tendo la ndoa hasa wenye uwezo mdogo wa kufurahishana au kumtoshereza mwingine, hiki ni kiini cha kutoka nje ya ndoa na kusababisha migogoro ya kifamilia au mahusiano na hapa ndio ukatili katika ndoa/mahusiano hutokea. Walio kwenye mahusiano ni vyema kufanya jitihada za kumlizisha mwenza wako ili nawe pia akulizishe.

Ugonjwa wa Haiba (Personality Disorder)
Kuna takribani magonjwa 11 ya haiba na mengi huwafanya watu kufanya vitu bila uhiyari wa kutokujua kama ni kosa au sio kosa. Hapa zaidi ni kwa magonjwa ya haiba yanayokua ndani yake yana sifa za kutaka kuonekana na kusifiwa, mfano "narcissistic disorder na borderline disorder". Hawa watu wanahitaji msaada wa kisaikolojia ili kuwasaidia kuendana na hali zao bila kuleta madhara kwa watu wanaowazunguka.

Malezi (Historia ya kukatiliwa)
Watu wazima wengine walio vinara katika kukatili watu, wana historia mbaya ya kufanyiwa ukatili wakati wakiwa watoto. Kuna tatizo kitaaluma linaitwa "Traumatic Relapse", hali hii humtokea mtu kwa lile tukio alilofanyiwa akiwa mdogo hasa anapokutana nalo au kulishuhudia na kumfanya kurudi katika hali ya kutafuta unafuu wa hali aliyonayo kwa kufanya na yeye ukatili kwa weninge. Wazazi wanapaswa kuwaweka watoto wao katika mazingira salama ili kuwaepusha na ukatili lakini pia na wao kutokufanya ukatili kwa watoto wao.

Magonjwa ya Akili (Mental Illness)
Uwezekano wa mtu mwenye changamoto za Afya ya Akili kufanya ukatili kwa wengine ni 80% sababu uwepo wake kwenye kufanya matukio unakua haupo ila mwili wake ndio unakuwepo. Wagonjwa wengi wa akili wanakua na uwezo mdogo wa kuzimudu fikra na hisia na kuzaa tabia ya ukatili ndani yake. Mfano wa watu wenye magonjwa ya Hasira mlipuko, Hisia mseto na Skizofrenia wanakua na matendo yaliyotawaliwa na hisia na sio uhalisia wao. Jamii inapaswa iamke katika kupata huduma za changamoto za Afya ya Akili ili kuondokana na ukatili.

Elimu
Jamii inapaswa ipatiwe elimu ya kutosha na isiyoisha juu ya ukatili hasa kwa watoto maana wao ndio waathilika wakubwa. Elimu pia juu ya magonjwa ya akili inatakiwa iwe sehemu ya jamii au ikiwezekana waiingize katika mtaala wa kielimu kila mtu aweze kujifunza magonjwa hasa yale yaliyozoeleka ili kusaidia wahanga au kujikinga wao wenyewe.

Imani
Ni muhimu watu wengi kumrudia Mwenyezi Mungu hasa wale wanaofanya mauaji na ukatili kwa kuagizwa na waganga wa kienyeji hasa kwa watoto wachanga au wadogo.


CHANZO CHA MAUAJI NA UKATILI

Katika suala la ukatili na mauaji kuna vyanzo vya aina nyingi kulingana na mazingira mtu anayoishi au hali aliyonayo;

Kuchepuka au mahusiano mengi
Watu wengi sasa wako katika mahusiano yanayowahusisha watu zaidi ya mmoja na kupalekea uaminifu kufa na hali hii hupelekea ukatili hasa kwenye ndoau kwa wapenzi na ndipo mauaji pia huibuka. Kuna watu hata hufanya mauaji kwa watoto kwa kutoamini kuwa ni watoto wao

Uchumi
Sasa hivi kila mmoja anapambana ili kuleta mkate wa siku na wazazi au uliyenaye anapokosa au kazi inapokua haiendi vizuri basi huhamishia ile hali ya kazi katika familia au mahusiano yake, hapa wazazi wengi wanawafanyia watoto wao ukatili kwa kuathiliwa na kazi zaidi na bahati mbaya wanakua hawajui kuwa kazi ndio chanzo cha matendo anayoyafanya.

Maagizo kutoka kwa waganga wa kienyeji
Waganga wanakua chnzo cha kuwafanya watu kufanya mauaji na ukatili hasa wa ubakaji kwa kuamini kile watu wanachokihitaji watakipata kama mali au fedha. Maeneo ya vijijini watoto wengi wanafanyiwa ukatili kwa kigezo cha waganga.

Shule
Shule kuwa na umbali kutoka sehemu wanayoishi watoto ni moja ya chanzo cha watoto kufanyiwa ukatili hasa watoto wa kike. Walimu pia shuleni kwa namna moja ama nyingine huwa chanzo cha watoto kufanyiwa ukatili na walimu wengine ukatili huufanya wao wenyewe na hii hutokea sababu ya nguvu na imani kubwa waliyonayo kwa wanafunzi.

Baadhi ya walimu hutengeneza mazingira ya kuogopwa na wanafunzi huku jamii ikiamini kuwa mwalimu ni mzazi wa pili maana mtoto hutumia muda mwingi kuwa nae na kujifunza mengi kutoka kwake, hali hii inakua ni hatari kwa Watoto hata kama anafanyiwa ukatili na mwenzake ni vigumu yeye kutoa taarifa kwa mwalimu.

#StoryofChange
Asante kwa kusoma uzi huu naimani utakuletea mabadiliko kadhaa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom