Sumaye Achinja mbuzi na kufanya sherehe baada ya Lowassa kujiuzulu

Status
Not open for further replies.

Kama haya ni kweli basi mara moja angeweza kugundua kuwa Richmond ni kampuni hewa,vinginevyo nazidi kuamini pasi shaka kuwa Richmond ni yeye na yeye ni Richmond
Kwa hiyo hata kama alikuwa mtendaji vizuri vipi,kwa ufisadi huu uliopelekea kupotea mabilioni ya shilingi na kuua watanzania wengi kimwili,kiroho na kiuchumi tayari amepoteza sifa zozote nyingine nzuri,anachostahili sasa ni lupango tu na muflisi.
 
Nina uhakika JK ataisifu Jambo forums wakati akitangaza baraza la Mawaziri.labda aone aibu ila ndio ukweli.Waandishi wote hata Mwanahalisi wanatoa Nws Hapa.

JF ndio kikomo cha ufisadi.

Sumaye alikuwa na usongo wa aina gani ?
 






Kwa ufuatiliaji na msimamo Tulwai ni kichuguu na Ngoyai ni Mlima;miaka kumi ya "bora kiongozi" ni alama ya aibu si ushujaa. Shida ni hii ya uharamia na vamiavamia ya Ngoyai. Sijasoma ripoti ya Mwakyembe kwa kina hivyo nasita kusema wazi endapo kuna mahali inapomtaja moja kwa moja Ngoyai kuhusika/kupewa chochote (pamoja na kunyimwa haki ya kusikilizwa), lakini nadhani Tulwai ukimuundia Nusu-mwakyembe tu, atahamia morogoro si kibaha tu...hili la EPA laja. Hivi kweli wananchi tulioliwa miaka kadhaa ya uwaziri mkuu wake, wanajifunza nini wanapomuona "Zero" anachinja mbuzi?!kushangilia yeye alikula salama? Ya EPA na TICTS nayo hayamuhusu? Ya DEEP GREEN na Mwananchi Gold pia si yeye alikuwa Waziri Mkuu? ZERO anadhani aliyeshikwa na mfupa ndiye aliyekula nyama,..kwa haki kutendeka tulwai naye atuambie zile nyama zilivyoenda chini yake...
 
Wanasiasa wote wanachotaka ni madaraka ili wapate kutunyonya vizuri, huyu Sumaye hana jipya bahati yake tu hatukushtuka.
 

Kama ni kweli basi amepoteza muda wake bure! Yeye SUmaye ni Fisadi tu kama EL tofauti ni kuwa yeye alikuwa Waziri Mkuu wakati wa Utawala wa BWM ambao uliwakumbatia na kuwasafishia njia mafisadi.

Ni vema ajue naye pia atakinywea kikombe hicho hicho ikiwa JK atakuwa ana nia ya kweli ya kupambana na wote walioitafuna Sangara wetu (nchi yetu) na kutuachia mapanki!
 
Kama SUmaye angekluwa mchafu mithili ya Lowassa,Je angeweza kubaki mpaka hivi sasa?Tumuache apumzike kwa Amani.Ni bora Lowassa kang'oa sababu amedhihilisha malipo ni hapa Duniani
 
mi nimeona nisome hii habari ya 2008 leo 2016 .... nimesoma kimya kimya
 
mi nimeona nisome hii habari ya 2008 leo 2016 .... nimesoma kimya kimya
 
Funzo tunalopata hapa ni kuweka akina ya Maneno, Chadema walipomshikia Bango Lowassa hawakuwaza kuwa ipo siku atapeperusha bendera ya chama chao kwenye Urais. Hata huyu January Makamba waweke akiba ya maneno hatujui 2025 itakuaje?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…