Sumaye apinga SERIKALI TATU



tusishabikie serikali tatu kwa maana ya kulinganisha na mfumo mbovu uliopo, tume inabidi kuungwa mkono kwa jambo zuri na si serikali tatu, serikali moja ndio kitu muhimu saana kwa uchumi wa nchi hii.
serikali tatu, ndege za maraisi watatu, ikulu tatu, cabinet tatu, mabunge matatu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, maspika, hawa watu wakistaafu nini kinatokea! ni kuubaka uchumi wa nchi hii, wananchi wanalipa kodi kwa nguvu zao zote na still watu wachezee pesa. thats non sense. serikali tatu ni upungufu wa fikra na kufikiria kutatua migogoro kwenye katiba. huo ni upungufu wa mawazo chanya kwa nchi yetu na watu wake. Tuwe makini, hakuna barabara za kuunganisha nchi yetu, foleni Dsm zinaua uchumi badala ya kupeleka pesa kule tunataka kuhalalisha ulaji kwenye katiba.
tuwe makini saana katika maoni ya katiba.
serikali tatu ni ubeberu kwa mwananchi mlalahoi
 

HATA HUJUI KUWA KIKWETE NDIYE ALIYESEMA HAJUI KWA NINI NCHI NI MASKINI.
 

RASIMU YA KATIBA inatia moyo'kuhusu serikali tatu gharama si tatizo'labda kuna mengine yanayompa hofu sumaye kwani kitendo cha wizara kupungua hadi 15 pesa nyingi zimekuwa zikitumika kuendesha wizara takribani 45'tusonge mbele kwani wapo wanaopata kigugumizi uwepo wa mgombea binafsi'so kila mtu ataguswa kwa namna yake na katiba hii mpya ikiwa itapita kama rasimu inavyopendekeza
 
Kwa hali iliyopo sasa Tanzania serikali 3 ndiyo suruhisho.
Wenzetu Zanzibar wamepiga kelele karibu miaka yote 49 ya muungano kupinga kero nyingi za muungano.
Katiba sasa inakuja kuimarisha muungano.
Suala la gharama ni suala la kizushi litokalo kwa wale wanaotapatapa wakijua mwanzo wa mwisho ndo huu.

Tangu lini viongozi waandamizi wa Tanzania wanajari gharama za kuendesha Tanzania????
Tangu lini???

Ni wafujaji wakubwa wa mali ya umma, malaya watapanya mali.
Ni wakengeufu wa mioyo, majuha na malimbukeni na akili za KiTeenager.

Wana Criminal minds ambazo kila siku hubuni njia madhubuti za kiharamia za kunyonya uchumi wa nchi kwa faida yao, familia zao na waume zao toka nje waliopo kwa vilemba vya uwekezaji.
Zaidi ya yote viongozi wetu wetu karibu wote hawana uzalendo wala utu, pia hawana shukrani, wamesahau kabisa kwamba bila Mwalimu Julius Nyerere wengi wangekuwa bado wanalala na ng'ombe au wanakula mchunga na ugali wa muhogohuko kwao mashenzini.
Tangu wao na wake zao waukwae uwezo wa kumechisha rangi za magari wanayoendesha na kaptula za ndani, basi wanadhani akili zao na mazoea yao ni SI unit ya uwezo wa kufikiri Tanzania.

Serikali tatu si jibu kamili la matatayizo yetu, lakini ni suruhisho la masuala mengi ya hovyo na ya kujitakia tuliyoyalea kwa karibu miaka 50 sasa.

Hii katiba si ya wazee wahuni waliotufikisha hapa, ni ya vijana,watoto na watu wanao litakia mema Taifa la Tanzania.

Mtoto akililia wembe mpe nyembe mbili.
 
Kuwa na serikali tatu ni upofu wa mawazo. Kwa nini tunalazimisha kukwepa ukweli?Tubaki na Tanganyika yetu tu kwa namna yoyote ile hizi chokochoko za kero za muungano hazitakwisha
 
Ukiona mtu anatetea serikali mbili jua ni MNAFIKI na MZANDIKI!!! Jiulize kwa nini chako chako na changu chetu?

Ndio! Waliona kazi rahisi pale Wazanzibari waliipokuwa wakiendesha mambo yao na Serikali yao, wao wakijitia katika Serikali ya pamoja. Sasa wanaweweseka wazee na vijana (hata Mr six nae analalama) eti ooh! gharama serikali tatu. Tukitaka iwe hivyo naam itakuwa.
 
Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.

chanzo: BBC

Angalizo: Nadhani ana hoja
Huko CHADEMA aliko anaamini serikali ngapi? Ugeugeu na uchumiatumbo ni ugonjwa mbaya sana.
 
SUMAYE huyu HUYU


Sumaye huyu ambaye juzi mashamba yake yamechukuliwa na serikali zaidi ya ekari 200 na kila kitu ndani yake.

Kumbe hata hayo mashamba yamekuwa ni mzigo kwake ameshindwa kuyaendeleza
 
du! comments za Enzi hizo Sumaye akiwa CCM
 
aisee!
 
Mbowe alifanya jambo jema kutuletea Sumaye Chadema
 
Zanzibar inapaswa kuwa Halmashauri Kama ya Longido ty
 
Kabisa...kwanini isiwe serikali moja?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui alizingatia nini Lakini mimi ni mmoja wa wanaopinga serikali 2 na Tatu. Nataka serikali moja. Kama ASP na TANU ziliweza kuunda CCM kwanini naserikali za CCM zisiunde moja? Muungano alioutaka mwalimu ilikuwa kuunganisha nguvu ya mataifa machanga lakini sasa naona ni masilahi ya watu. Serikali moja itapunguza mzigo zaid kwa sababu kule Zanziba kutakuwa ni mikoa tu kama bara hivyo kutakuwa na makambi ya jeshe na secta zingine kama kawaida. Hakutakuwa na serikali ya mapinduzi inayobeba Baraza la wawakilishi, lakini pia msuguano wa nani awe Raisi kutoka upande gani haitakuwepo na viongozi hawatapata nafasi ya kuchochea vitu vingine kama tunavyoona sasa tofauti za mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. yapo mengi. Mimi napenda serikali moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…