Elections 2010 Sumaye atajwa kumvaa Kikwete uchaguzi 2010

Elections 2010 Sumaye atajwa kumvaa Kikwete uchaguzi 2010

Msee Lekasio

Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
73
Reaction score
8
LICHA ya kutangaza kutogombea urais mwaka 2010, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye bado anatajwa katika anga za kisiasa baada ya kuelezewa kuwa ni mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kupambana na Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha urais.

Sumaye, ambaye alikuwa waziri mkuu kwa kipindi cha miaka kumi, alijitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kuwania nafasi hiyo mwaka 2005, lakini hakuweza kufua dafu.


Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, alikwenda masomoni nchini Marekani na aliporejea aliweka bayana kwamba elimu yake ya juu zaidi aliyokwenda kuipata haikuwa na uhusiano na urais wa 2010 na mara kwa mara amekuwa akisisitiza kutokuwa na mpango wa kugombea kiti hicho mwaka huu.


Alisema hata utaratibu wa CCM wa kumuachia mshindi wa kiti cha urais kuachiwa aendelee ngwe ya pili, unamzuia kujitokeza kuwania urais.


Lakini, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali zinasema Sumaye ni mmoja wa watu wanaoweza kubadili hali ya kisiasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Oktoba mwaka huuu.


Alipoulizwa jana kwa njia ya simu, alisema: "Nimetoa msimamo wangu mara kwa mara kuhusu jambo hili (la urais), kwa hiyo kama kuna watu wananitaja na kuniona nafaa, mimi nasema bado sijawaona wala kuwasikia."


Sumaye, ambaye alizungumza katika hali inayoashiria kuwa ni mwenye furaha, aliongeza: "Kama wakitokea watu wakiniambia nigombee urais, nitawauliza kwa nini wanataka mimi nigombee; wanafikiri nina kitu gani ambacho naweza kukifanya?"


Alipoulizwa kama kutatokea watu na kumtaka abadili msimamo wake ili aweze kugombea urais, alicheka kisha akajibu: "Aaaa... sasa tatizo hao watu hawajajitokeza na kuniambia hivyo, wangekuwa wapo tayari ningeweza kuwapa jibu baada ya kuwauliza.


"Pia ningeweza kuwa na jibu kwako, lakini siwezi kujibu kitu kwa jambo ambalo sijalipata rasmi wala sijui ni nani anazungumza hivyo, ila wakiniambia siku nitawapa jibu."


Huku akiendelea kucheka Sumaye alihoji : "Au wewe (mwandishi) ndiyo unataka mimi Sumaye nigombee urais? Ninachoweza kusema hadi sasa sijamsikia mtu akitaka nigombee urais. Ila wewe kama ndiyo unasema Sumaye nigombee urais sawa ni maoni yako."


Sumaye alisema anafahamu kuwa hadhi yake ni mali ya umma na umma unaweza kumwomba afanye kitu fulani, lakini bado alisisitiza: "Sijawasikia hao watu wanaonitaja mimi nigombee urais." Sumaye alisema hadi sasa bado yuko CCM na kwamba kama kuna mipango yoyote ni ile inayofuata taratibu za chama.


Waziri mkuu huyo mstaafu alisema kwamba umma ni sehemu kubwa na kwamba hadi sasa hajaelewa genge hasa ambalo linamtaka yeye kugombea nafasi hiyo na mantiki inayokusudiwa.


Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa uamuzi wa kumtaka agombee kiti hicho ni ombi maalumu kutoka kundi maalumu la watu wa kada mbalimbali nchini.


Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, tayari kundi hilo limejipanga vema ikiwa ni pamoja na kufanya hadi utafiti kuhusu asilimia za kura za urais ambazo Sumaye anaweza kuzipata kama ataingia katika kinyang'anyiro hicho kwa kumvaa Rais Kikwete.


Ingawa tafiti mbalimbali ikiwemo za Synovate zinamuonyesha Rais Kikwete kuweza kupata asilimia zaidi ya asilimia 50 katika uchaguzi ujao, vyanzo hivyo vinaonyesha kama Sumaye ataingia anaweza kupata asilimia 40 ya kura za urais huku Kikwete akipata asilimia 52.


Vyanzo hivyo vya habari vilifafanua kwamba Sumaye amekuwa akiandaliwa mipango mbalimbali ambayo kwa sasa imefikia katika hatua ya juu ya kiutekelezaji kumwezesha kutimiza azma hiyo ya kumvaa Kikwete.


Katika taarifa hizo, vyanzo hivyo vinasema Sumaye anaonekana kuwa mtu makini na mwenye maono na ana uzoefu unaoweza kuleta changamoto kubwa za maendeleo kutokana na kukaa madarakani akiwa ni waziri mkuu kwa kipindi kirefu cha miaka 10.


Siku za karibuni Sumaye amekuwa akijitokeza hadharani katika matukio mbalimbali na hata mwishoni mwa mwaka jana alishiriki kikamilifu katika kongamano la hali ya kisiasa nchini lililoandaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere na kufanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.


Katika kongamano hilo Sumaye alikuwa akitaka kusomwa kwa maazimio yaliyotolewa na wananchi bila kuchelewesha, lakini mwenyekiti wa kongamano, Dk Salim Ahmed Salim alishauri ufanyike uhariri kidogo kutokana na maazimio hayo kuwa makali zaidi kwa serikali ya Rais Kikwete.


Kongamano hilo hadi sasa limebaki kuwa tukio kubwa ambalo serikali na CCM iliwaelezea waliohudhuria kwamba ni watu ambao walikuwa na chuki kutokana na kukosa madaraka baada ya uchaguzi wa chama wa mwaka 2005. Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi, kundi hilo la watu mashuhuri wakiwamo viongozi wa dini, wanasheria, wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani wamekwishaweka mkakati maalum wa kumshauri Sumaye kugombea ili agombee uraisi.


Kikwete anaonekana kuwa hata kuwa na mpinzani mwaka huu baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumuacha mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba kuwa mpinzani pekee mwenye nguvu kwenye kinyang’anyiro hicho.


Hii habari ni kutoka gazeti la mwananji
 
Japo wengi wanaona Sumaye hakufanya fisuri alipokuwa wasiri mkuu dhakini mimi naona ni jambo jema kumpa Kikwete upinsani....
 
Ashe bhabhalai...Ashe Naleng!...Ni maneno nsuri sana hii!...mi pia nataka sana hii shauri itokee kwa hii leigwanan!
 
Wote ni walewale tu ni kama kuhama siti ndani ya basi ukifikiri utaepuka pancha na ajali nyingine!
 
Hata kama ikitokea Mh. Benjamini Mkapa akasema anataka kugombea tena sidhani kama litakuwa tatizo kubwa....kinachoni sugua mtima wangu ni kwamba ...WANA LIPI JIPYA???????

Ari,nguvu na kasi mpya ndo hizoooo zimebakiza miezi michache tuzitie kwenye mizani tuone uzito wake, sijui Mtanzania atapata kilo ngapi toka kwenye mizani wa nafsi yake.....huyo Sumaye atakuja na lipi????

Labda, jazba mpya,ukakamavu mpya na kujifunga mkanda....mungu ndo ajuae
 
Sumaye si mpumbavu. Ni kipindi cha uongozi wake na baba yake Mkapa tuliposhuhudia madudu mengi ya ajabu yakifanywa na serikali. Akithubutu tu kumpinga Kikwete, the following morning atakuwa kisutu sambamba na Mramba & co
 
Sumaye si mpumbavu. Ni kipindi cha uongozi wake na baba yake Mkapa tuliposhuhudia madudu mengi ya ajabu yakifanywa na serikali. Akithubutu tu kumpinga Kikwete, the following morning atakuwa kisutu sambamba na Mramba & co

Maasi aliyofanya Sumaye, aliyafanya kwa akili sana na bila kuacha traces zozote. Kwa kifupi ni vigumu sana kumuunganiasha Sumaye na ufisadi (japo alichuma sana wakati akiwa waziri mkuu) uliofanyika. Laiti Kikwete/washirika wake wangekuwa wanayajua madhambi yake....tungesikia mengi
 
wadau naomba mnisaidie hivi kati ya kikwete na Sumaye Yupi Bora zaidi ya mwenzake
 
Wazee wote hawa wanaizingua nchi yetu tu, mtu wakati mwingine unaweza omba dua mbaya tu. Maana ukiangalia sisi wananchi hatuna jinsi ya kujikwamuwa kutoka kwa hii mikoloni.
 
sumaye alikuwa akidhaniwa ubaya kwa ajili ya kuchafuliwa na mtandao...mbona hata ameyashinda magazati yaliyokuwa yakitumiwa na mtandao mahakamani??? tutaona mengi mwaka huu inaonekana kuna watu wengi ndani ya ccm wapo nyuma ya sumaye kimya kimya???

bora sumaye kuliko sakakasi zisizoisha za kikwete.
 
Zote siti ndani ya gari kama jamaa alivyokwisha kusema gari ikipata pancha hatuendi wote! Mr FS amekiwa WM for 10yrs! Things were mambo jamboz business as usual! JK ndio huyu tumeimba wimbo wa ufisadi mpaka umezoeleka masikioni. Mwenzetu mmoja aliwahi toa ushuhuda akasema Mtoto wake wa mdogo alipoulizwa swali yeye anataka kuwa nani atapakapo kuwa mkubwa Mtoto akajibu anataka kuwa fisadi! Thats why Im saying we have sung, and we are still singing and the single had maintained on the chart for 5 yrs!
Supringly the guy hasnt heard the song! What if he had heard the song and is pretending he hadn't heard it!
I gt go!
 
Fred Sumaye ndio waziri mkuu wa kwanza kukamua 10 o'clock ingawa alikuwa na diploma lakini alikuwa anamake sense sasa hawa jamaa kuwalinganisha inakuwa ngumu sana unajua wamehudu nafasi tofauti ingawa huyu alikuwa boss wa mwenzake
 
Bora kwenye nini kwa kuwa natambua kila mmoja anampiku mwenzake katika mambo fulani fulani.Hebu tueleze vizuri unamaanisha nini.
 
Sumaye si mpumbavu. Ni kipindi cha uongozi wake na baba yake Mkapa tuliposhuhudia madudu mengi ya ajabu yakifanywa na serikali. Akithubutu tu kumpinga Kikwete, the following morning atakuwa kisutu sambamba na Mramba & co

Inaelekea wewe hukumpata vizuri Sheikh Yahya Hussein! The following morning atakuwa marehemu siyo Kisutu.:frown:
 
Nadhani katika habari tuliyobandikiwa hakuna mahali popote ambapo Sumaye amesema anataka kugombea isipokuwa wapo watu wanaomtaka agombee. Kwa hiyo kuanza kumpaka na kumshutumu haina maana sana.

Naungana na aliyesema kwamba ni bora Sumaye kwa sababu anao uzoefu na vile vile hatujayaona matope aliyojipaka akiwa Waziri Mkuu. Kujitokeza kwake hadharani na kujiunga na wananchi wenziwe kujadili mustakabali wa Taifa letu kunadhihirisha anavyojali. Uzoefu aliupata katika kipindi cha miaka 10, changamoto za uongozi alizozipitia, utambuzi wa makosa aliyoyafanya na yaliyofanywa na viongozi wenziwe, yote hayo yanaweza kufanya aibuke kuwa Rais mzuri.
 
livingston
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png


Join Date Mon Jun 2008
Posts 1
Thanks 0
Thanked 0 Times in 0 Posts


where have you been all this long!
Rep Power 0
 
Back
Top Bottom