Sumaye ndani ya Uingereza!

Status
Not open for further replies.

Hapana, Mkuu. Bila kupiga kelele hizo sheria hazitobadilishwa. Ni muhimu kulalamika kwa kadri ya uwezo. Pengine wahusika wataona aibu na kuanza kuwaonea huruma wananchi wao.

Madiba alipokwaa urais bunge lake likampitishia mshahara wa ajabu sana. Mzee hakusema kitu. Lakini alipoamka Desmond Tutu na kusema mshahara ule haukustahili katika nchi kama ile, bai Madiba akaukataa na kuelekeza upunguzwe!

Hawa wenzetu nao wakisema kuwa hawataki kwenda nje kwa check-up ( hawalazimiki kwenda huko) basi hao wanaojipendekeza itabidi wabadilishe haya mafao dhalimu!

Amandla.........

Fundi Utumbo a.k.a Uwiano Usio Maalum
 

Sawa mkuu nakubaliana na wewe. Ila unatakiwa kujua Tanzania hatuna viongozi kama Mandela. Ingekua kupiga tu makelele wana sikia tusha pigia makelele mangapi? Huyo mandela alivyo punguziwa mshahara si ilibidi hiyo sheria irekebishwe ili mshahara ipinguzwe? Kutaka wakatae privileges walizo nazo ni kuji danganya, watu wangapi duniani hukataa privileges walizo nazo ndani ya sheria? Hata mshahara kwa raisi siyo lazima ila maraisi wangapi haswa nchi kama za kwetu hukataa kulipwa? Isipo badilishwa sheria leo tutam lalamikia Sumaye, kesho akienda Mkapa tuta lalamika, kesho kutwa Kawawa na Mwinyi tutaendelea kulalamika. Ukweli unabaki hizo haki wanazo ndani ya sheria na kukataa au kukubali na maamuzi binafsi, utam lazimisha mtu kukataa mafao yake? Cha kufanya ni kuondoa hayo mafao kabisa kwenye sheria na kumlalamikia kiongozi mmoja mmoja badala ya sheria yenyewe haita tufikisha popote.
 

Hakuwa na clearance wasiliana na mambo ya nje.siruhusiwi kutoa document ya safari yake hapa JF nipe email nitakutumia.ninazo hadi za utumishi.

naomba tumia dakika mbili kutizama picha ya Mama aliyekuwa akitafuta riziki yake kwa kuuza nyanya Kariakoo iko kwa michuzi blog amevuliwa nguo na kuachwa uchi na mgambo wa jiji kwa kuvunja sheria.wewe unayemtetea Sumaye kwa kuvunja sheria umeona wenzake wanavyoadhibiwa? imenitoa machozi.mama kama yule akiuza nyanya ndio anapata riziki yake,mama kama yule akitoa sadaka yake kanisani au msikiti ni jasho lake.

unajua kuwa Sumaye anaweza kushitakiwa kwa fojari?amedai anaumwa ili akatibiwe kumbe yuko FIT.ni sawa na mtu anayekwenda hospital kuchukua cheti cha daktari akiwa haumwi ili asiende kazini kwa wiki mbili na huku akichukua mshahara kama kawaida ndio ufisadi huo.
 

Sasa, Mkuu, kama unaona kulalamika ni kugumu basi hizo sheria unategemea zitabadilishwa vipi? Hizo sheria zitabadilishwaje bila sisi kuonyesha kukerwa nazo? Hatuwezi kukaa na kungoja atokee Desmond Tutu wetu au Madiba wetu. Bandu bandu humaliza gogo. Hivi hivi vijikelele vyetu iko siku vitasikilizwa. Kama sio na wanaofaidi basi na hao wanaopeleka kwenye ulaji. Dr. Slaa ameanza nae kwa kulalamikia mafao na mishahara wanayolipwa waheshimiwa hawa. Basi nasi tumuunge mkono kwa kupiga kelele. Iko siku watatusikia. Tukikaa kimya, hiyo siku haitakuja fika.

Amandla..........

Fundi Utumbo a.k.a Uwiano Usio Maalum
 
kanda2,

..maadamu una access na watu wenye document za safari za viongozi nje, tuletee taarifa za gharama za safari za Kikwete nje ya nchi.
 

Lakini bado sijaelewa unasema Sumaye kaenda kutibiwa au kwenye check-up? Mimi simtetei Sumaye kwa lolote ndugu yangu. Najua mateso ya watu wa kawaida. Ila nilicho kua napinga ni hoja zako za mwanzo ambapo nili kuuliza maswali mpaka sasa hauja yajibu. Ndiyo maana nikasema tatizo si Sumaye tatizo ni sheria. Na kama kavunja sheria hiyo ya clearance basi ni wajibu wa wahusika kum shugulikia. Wote tuko upande mmoja ambayo ni vita dhidi ya ufisadi, tofauti yetu ni approach zetu. Mimi naona sheria ndiyo tatizo na ndiyo ninayo taka ishugulikiwe lakini jua tupo upande mmoja. Maswali niliyo kuuliza mimi ni maswali ambayo katika kutetea nchi lazima utaulizwa na lazima ujibu. For every attack there is a counter attack. Sasa ndugu yangu kama nimekuuliza maswali yale machache ambayo mpaka sasa hauja jibu vizuri na kuishia kusema tu mimi namtetea Sumaye hauoni hatuta fika? Mambo haya ni ya hoja na lazima mtu uwe tayari kutetea hoja zako na jua hoja zako zita pigwa maswali. Naonea huruma wananchi wa kawaida ila najua hawa viongozi kuwa lalamikia hatuta fika popote, najua mapambano yana takiwa kuwa kwenye sheria na nadhani hapo ndipo tofauti zetu za kiitikadi zilipo. Kamwe siangalii mtu bali naangalia hoja zinazo tolea na yeye au dhidi ya mtu/kitu fulani. Kwangu mimi hoja zako zilikua weak kutetea unacho pigania ndiyo maana nikakuuliza maswali na kama unavyoona mengi ukashindwa kujibu. INdiyo maana post ya mwisho nikasema mimi siogopi kukiri kosa iwapo utanionyesha kwa hoja zako kuwa nime kosa. Ila tupo upande mmoja mkuu, dhidi ya ufisadi, tofauti ni views zetu tu. na kuhusu email yangu unaweza kuni pm mkuu.
 

Sawa mkuu nime kuelewa. Tupo pamoja.
 
kanda2,

..maadamu una access na watu wenye document za safari za viongozi nje, tuletee taarifa za gharama za safari za Kikwete nje ya nchi.


Joka Kuu umenena. Let's hope that Kanda2 atamwaga hizo taarifa za gharama za safari za Kikwete nje ya nchi.

Kanda2, you surely can understand that many opinions, though against leaders' over-spending, are sceptical of your singling-out only Sumaye?

Please we are waiting for expenses of JK's trips abroad.


Jingine:
Kuna gharama kubwa zinakuja, wabunge wameanza kutaka kuongezewa mishahara, wanadai hizo sh milioni 6 hadi 7 kwa mwezi haziwatoshi. Eti wanadai wanatumia gharama kubwa 'kuwasaidia' wapiga kura wao majimboni. Uhuni tu, hiyo ni hiari yao, siyo lazima, ni kama rushwa tu.

Ni kweli kwa hilo tuanzishe kampeni kumuunga mkono Dk. Slaa kwa kuwalaani wabunge wanaompinga. Wengi wataona aibu kumpinga hadharani, na matokeo yake wengine watamuunga mkono kwa aibu, na tukipiga kelele saea bili kuchoka mishahara yoa itabaki milioni 7 tu!

Si mmeona pressure ndani ya House of Commons ya UK kuhusu malipo ya wabunge wa UK na pia suala la Ghurka soldiers? People pressure imefanya Govt ikubali matakwa ya wananchi kwa yote hayo mawili.

Halafu si Bunge hili ndio lilitaka kujipandishia mishahara mara tu lilipoingia madarakani? Pressure ilisaidia mishahara ya wabunge wetu isipande. Tuanzishe tena hii.

Wazee wa research tufanye mambo.
 
Last edited:

Kweli kabisa hata mimi nina skepticism because most of his post zinaonyesha kuwa ni something personal against Sumaye rather than the cause. If you having something concrete you know tueleweshe hapa jamvini.
 
Hivi hizi entitlements ni za viongozi tu. Nilikwenda JKT wakati wanakaribia kusimamisha mafunzo kwa wanafunzi.

Na kule nilipewa kitabu ambacho kilitoa orodha ya vitu vyote ninavyotakiwa kupewa nikiwa jeshini, entitlements zangu.

Asubuhi nilitakiwa kunywa chai na nusu mkate wenye siagi. Lakini nilikuwa nawepa chai tupu.

Nilitakiwa kupewa pair mbilimbili za mavazi. Lakini mpaka naondoka sikuweza kujua jinsi soksi za kijeshi zinavyofanana.

Nilitakiwa chandarua, lakini mpaka naondoka sikuwahi kupata chandarua.

Kwa ujumla nilipata chini ya 10% ya entitlements zangu. Na bado nilitakiwa nisigome.

Mkitaka kuzungumza entitlements, hata wafanyakazi wastaafu wa jumuia ya Afrika mashariki walikuwa na entitlements.

Hivyo tunapozungumza entitlements za viongozi wetu ni lazima tufikiri kwa sababu hata wafanyakazi wa serikali wana-entitlements zao ambazo zimeandikwa vitabuni na hazitekelezwi.

Nikiwaletea gharama za vidonge vya TB na ukilinganisha mizunguko ya wakubwa wetu, utaona hakuna justification yoyote ya watu kuwa na entitlements medical check ups nje ya nchi.
 
Wakati akina Sumaye wakijirusha huko majuu kwa kodi zetu huku nyumbani hali halisi kwa akina mama wajasiriamali ndio kama hivi.

Huyu dada Veronica kanyang'anywa bidhaa zake na mgambo wa jiji eti anaharibu mji!



Hata kama ni sheria watuambie ni sheria gani inayo wapa mamlaka ya kuwavua kina dada zetu nguo?





Halafu mnatujia na longolongo za "stahiki" kama mtu anaona uovu na anaunyamazia au ananufaika nao nae ni fisadi.
 
- Wakuu hata huko US sasa hivi kuna wananchi wanaoteseka sana na matatizo ya uchumi, huku Obama akitumia dola millioni karibu 60 kwa ajili ya inauguration, taifa ni lazima liwe na waongoza na waongozwa, tunawapa haya yote viongozi wetu wa juu ili kuwaepusha na tamaa ya kuiba mali za umma,

- Ndio maana wakitoka kwenye power kama bado wameiba inahitajika adhabu ya ajabu sana maana huo sasa ni usaliti, otherwise inapendeza sana kuona taifa linavyowathamini viongozi wake, ndio maana Kaunda alipigwa na bumbuwazi kuona wastaafu walivyonawiri na wako pamoja na serikali uwanja wa taifa katika sherehe za kitaifa tena upinzani na CCM, wote hatuwezi kuwa sawa katika maisha wakuu,

- Matatizo ya taifa letu yanafahamika lakini haina maana masiha yanatakiwa kusimama, kwani majuu hakuna masikini wanasikitissha manjiani? Majuzi tu nimesikia NYC serikali ya City imeamua kuwalipisha homeless kwenye shelter walizokuwa wanalala bure, Tanzania tunahitaji new policies ambazo wananchi tunaweza ku-invest in badala ya kuwaamini viongozi kama tunavyfanya sasa, ndio maana unasikia Magufuli ndiye aliyeishindisha CCM Busanda, that is sad!

Respect.

FMES!
 


Mkuu FMES:

Matumizi ya waMarekani na nchi masikini kama vile Tanzania, ni kama vile matumizi ya Cocaine kwa tajiri na masikini.

Tajiri akiwa addicted na matumizi ya cocaine, anazo pesa za kwenda rehab. Na vilevile akikamatwa na vyombo vya sheria, bado anazo pesa za kulipa wakili mzuri na kushinda kesi. Hivyo basi matumizi ya cocaine kwa tajiri sio lazima yaharibu quality ya maisha.

Kwa upande mwingine cocaine kwa masikini inazidisha messy tupu.
 
 
 

- Mkulu Zakumi, sawa sawa tupo pamoja sana hapo!

Respect.

FMEs!
 

picha hii imetoa machozi jana.wakati mama huyo anahangaika apate riziki yake ya halali.SUMAYE ANATUMBUA KODI ZETU KWA KIGEZO CHA HAKI YAKE KISHERIA.

KAACHA KWENDA KANISA LA KAKOBE AU KWA MAMA RWEKATARE HADI READING?ONA AIBU SUMAYE.WATU KAMA SUMAYE WAKO TAYARI TULE MAJANI ILI WANUNUE NDEGE ZAO TUKIULIZA JIBU TUKO ENTITLED KIKATIBA.SUMAYE MTIZAME MAMA HUYU ANAVYOKULA KWA JASHO LAKE.
 

Kikwete, Pinda, Lukuvi na viongozi wengine ambao wana madaraka ya maamuzi kwa sasa hebu mtizameni huyo mama! Hawa ndio wenye uwezo wa kusaidia hapa.

Huyu kanda2 ana issue fulani na Sumaye.

Data za gharama za safari za Vasco da Gama vipi?
 

Kuddo!

Hivi Mzee Mwinyi alipochapwa kofi alikuwa wapi na akifanya nini...???
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…