benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha 'madudu' ya ubadhirifu wa fedha kwenye maeneo mbalimbali, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ameibuka akisema Bunge linapaswa kuwa kali katika kuisimamia na kuishauri Serikali.
Sumaye aliyekuwa Waziri Mkuu kwa muongo mmoja kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 katika utawala wa Awamu ya Tatu amesema kwa kawaida hakuna Serikali ya demokrasia inayokataa ushauri wa Bunge.
"Haya mambo yanapojitokeza mara kwa mara lazima tukubali kuna tatizo mahali fulani, kubwa kabisa ni Serikali lakini Bunge nalo halifuatili," alisema.
Sumaye anatoa kauli hiyo ikiwa ni takribani wiki mbili zimepita tangu Ripo-ti za CAG Charles Kichere kwa mwaka 2021/22 zilizowasilishwa bungeni jijini Dodoma.
Katika mahojiano kati ya Sumaye na televisheni ya mtandaoni ya Dar 24, yalijikita katika masuala mbalimbali yanayomhusu Sumaye na ripoti za CAG, alisema;
"Bunge lina kazi kubwa na linatakiwa liwe na ukali zaidi, ndiyo maana tunapenda Bunge lenye vyama mbalimbali kwa sababu ni afya kwa nchi.
"Hiki kitu watu hawakielewi, watu wanafikiri ukiwa na Bunge la chama kimoja, ndio njema, hapana. Ukiwa na Bunge la chama kimoja ndani ya mfumo wa vyama vingi ni tatizo," alisema.
Ripoti za CAG alizokuwa anajadili Sumaye zimeonyesha ubadhirifu kati-ka taasisi na mamlaka za Serikali, hali ambayo imewaibua wadau wakitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Tayari Rais Samia Suluhu Hassan, amekwishaanza kuchukua hatua kwa kutengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) na kuivunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mbali na hilo, Rais Samia ametoa maagizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
DK Moses Kusiluka kuhakikisha makatibu wakuu na watendaji wakuu wote wa taasisi za Serikali wanapitia kwa kina taarifa ya CAG, wajibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote.
Bunge la sasa ambalo lilitokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, lina wabunge wengi wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), zaidi ya asilimia 90 huku upinzani wakiwa wachache tofauti na mabunge yaliyopita na wengine hawatambuliwi na vyama vyao.
Aprili 12 mwaka huu, Spika Tulia Ack-son alisema wabunge wanaruhusiwa kuijadili ripoti hiyo kwa namna wanavyoona inafaa lakini watambue kuwa Serikali haitalazimika kujibu kwa kuwa Kamati za Bunge Mashirika ya Umma (PAC) na ile ya Serikali za mitaa (LAAC) itapitia taarifa hiyo na itawasilishwa bungeni.