JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Ndugu zangu tunapata taarifa nyingi toka kila pande ya nchi yetu pendwa ya Tanzania,Leo nimepata taarifa kuwa huko Sumbawanga MANISPAA madereva bajaji wamekaa kikao na kupandisha gharama za usafiri hususani bajaji kutoka Tshs 600 hadi 800 mpaka elfu 1000 kwa baadhi ya maeneo,ilhali gharama za mafuta zinashuka kila siku.
Nimejaribu kutafakari hivi chombo rasmi kinachopanga nauli za usafiri wa umma kinafanya kazi gani hadi madereva BAJAJI na viongozi wao wanachukua mamlaka mikononi na kupandisha gharama kiholela kabisa na kuongeza ukali wa maisha ya watanzania wa MANISPAA ya sumbawanga na Tanzania kwa ujumla.Mkoa una viongozi na mkuu wa mkoa ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwl.Julius kambarage Nyerere ndugu yetu Makongoro Nyerere yawezekana hana taarifa hizi za kikundi cha wahuni waliokaa na kujigeuza SUMATRA.
Nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa Sheria ninaomba mamlaka husika fuatilieni huko Sumbawanga MANISPAA mtaigundua hiyo Sumatra mpya iliyozuka naamini mtachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria,Tukumbuke gharama za mafuta zinaposhuka watanzania hawapaswi kuendelea kuteseka bila sababu zozote za msingi.Mamlaka husika fuatilia.