Pre GE2025 Sumbawanga: Serikali ipo mbioni kuanza ujenzi wa daraja la Ilembo lenye urefu wa mita 60 kwa bilioni 1.3

Pre GE2025 Sumbawanga: Serikali ipo mbioni kuanza ujenzi wa daraja la Ilembo lenye urefu wa mita 60 kwa bilioni 1.3

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali imesema ipo mbioni kuanza ujenzi wa daraja la Ilembo lenye urefu wa mita 60 litakalogharimu kiasi cha Shilingi Bil.1.3 hadi kukamilika kwake lililopo Kata ya Mpui, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Wenyeviti, Makatibu na Mabalozi wa CCM wa Kata ya Mpui, ikiwa ni ziara yake ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo hilo.

Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Sangu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha inajenga daraja hilo ili kusaidia wananchi kupata huduma za kijamii, kibiashara na uwekezaji katika kipindi chote cha mwaka.
1740992207786.png
 
Back
Top Bottom