Sumu kuvu inavyosababisha Saratani ya ini

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Mahindi na karanga ni mojawapo ya mazao muhimu ya chakula. Mazao hayo huweza kushambuliwa na fangasi wanaozalisha sumukuvu ambayo huathiri usalama wa chakula.

Sumukuvu ni nini? Sumukuvu ni sumu zinazotokana na aina ya ukungu (fangasi) unaoota zaidi kwenye mazao kama mahindi na karanga.

Jinsi Sumukuvu inavyoweza kumfikia Mlaji huweza kupata sumukuvu endapo atakula chakula kilichochafuliwa na sumu hiyo. Hali kadhalika, mtoto anayenyonya huweza kupata sumukuvu kupitia maziwa ya mama endapo mama anayenyonyesha atakula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu. Aidha, baadhi ya sumukuvu hupatikana katika vyakula vitokanavyo na mifugo kama vile maziwa endapo mifugo italishwa chakula kilichochafuliwa na sumukuvu.

Madhara ya kiafya yatokanayo na sumukuvu Ulaji wa chakula kilichochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu husababisha madhara ya kiafya na hata kifo. Madhara hayo huweza kujitokeza baada ya muda mfupi au mrefu kutegemea kiasi cha sumukuvu kwenye chakula kilicholiwa, muda ambao chakula kilichochafuliwa kimekuwa kikitumika, umri wa mlaji na hali ya afya kwa ujumla.

Madhara yanayotokea ndani ya muda mfupi Hutokea baada ya mtu kula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu kwa kiasi kikubwa. Madhara hayo ni pamoja na kuharibika kwa ini na hata kifo. Dalili zake ni pamoja na:- Maumivu ya tumbo, kutapika, kuvimba tumbo, homa, kuharisha, kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili (mfano viganja, nyayo, macho) na degedege.

Madhara yanayotokea baada ya muda mrefu Madhara haya hutokea endapo mtu atakuwa akila kwa kipindi kirefu chakula chenye kiasi kidogo cha sumukuvu. Madhara hayo ni: Kupungua kwa kingamwili Udumavu kwa watoto

Jinsi ya kudhibiti sumu kuvu kwenye mahindi na karanga Sumukuvu huweza kudhibitiwa kwenye mazao ya mahindi na karanga kabla ya kuvuna na baada ya kuvuna usindikaji.

Jinsi ya kudhibiti sumukuvu kabla na wakati wa kuvuna Panda kwa wakati mbegu zilizothibitishwa na wataalam Tumia viuatilifu vilivyothibitishwa mara uonapo dalili za visumbufu (wadudu, magonjwa) kwenye mazao Vuna mazao kwa wakati Ondoa mazao shambani mara baada ya kuvuna Kumbuka: Kuchelewa kuvuna au kulundika mazao muda mrefu shambani huchochea uzalishaji wa sumukuvu.

Jinsi ya kudhibiti sumukuvu baada ya kuvuna Chambua mahindi na karanga kuondoa taka, rangi na zilizoharibiwa na wadudu. Sumukuvu huweza kutokea wakati mazao yakiwa shambani, baada ya kuvunwa, wakati wa kusafirisha au kuhifadhi. Zinapokuwepo kwenye chakula, sumukuvu hazionekani kwa macho na pia huendelea kubaki kwenye mazao yaliyochafuliwa na sumu hizo hata baada ya chakula kupikwa au kusindikwa. Sumukuvu ambazo zimeripotiwa kuwepo zaidi kwenye vyakula ni aina ya aflotoxin ambayo hupatikana zaidi kwenye mahindi na karanga na aina nyingine ni fumonisin ambayo hupatikana zaidi kwenye mahindi
 
Ahsante sana!
 
Back
Top Bottom