Sumu ya NGE ni sumu ghali kuliko zote hapa duniani

Sumu ya NGE ni sumu ghali kuliko zote hapa duniani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642

https://www.udakuspecially.com/


Inadaiwa kuwa sumu ya nge ndio sumu ya gharama zaidi Duniani ikiuzwa kwa Dola za Kimarekani milioni 39 kwa galoni moja, sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 90. Galoni moja ni takriban lita 4.5

Sumu ya nge inaweza kumsababishia maumivu makubwa mwanadamu ikiwa ataumwa na mdudu huyu, lakini wanasayansi wamegundua na wanaendelea kutafiti, sumu hii inasadikiwa kutibu saratani ya matiti na magonjwa mengi sugu
Sumu ya nge ina Chlorotoxins ambayo hutumika kutibu saratani, Kaliotoxins hutumika kutibu matatizo ya mgongo. Kaliotoxin imeshajaribiwa kwa panya mwenye matatizo ya mgongo na ikafanikiwa

Bei imekuwa hiyo kwa kuwa kuna ugumu katika upatikanaji wa sumu hiyo, kutokana na wadudu hao kuzalisha sumu kidogo sana wanapokamuliwa, nge mmoja hutoa Mililita 2 akikamuliwa mara moja
Mimi nimeishia hapo tunagawana Michongo hoja hapa tujue namna ya ufugaji wake na soko lake kama una rafiki yako Mchina hebu muulize.
 
Back
Top Bottom