kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapojuu na vigumu kuzuilika, dawa yamajimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia, Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakulana kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli zamwili hudunda na kwenda mbalibila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwilini kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo kirusi hudakwa na melittinna kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipandevilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana nakirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana gandalote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu yakimaumbile ya virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi.
Tatizo katika tiba ya kuzuia uwezo wa kirusi kujidurufisha ni kuwa maambukizi yanakuwapo na hayakomi mwilini, hivyo hayazuii maambukizi kuwepo mwilini.
Baadhi ya vipande vya virusi vya Ukimwi vimepata uwezo wa kujibadili hivyo kuzuia ufanyaji kazi wa ARVs na hivyo kuendelea kuzaliana na kuvamia seli za mwili.
Mtaalamu huyo anaeleza: Tunashambulia sehemu ya kimaumbile ya kiurithi ya VVU, kinadharia, tunasema hakuna namna yoyote ya kirusi kuweza kujibadili ili kukabiliana na mazingira mapya ya kujihami na mashambulizi ya tiba hii ukilinganisha na mashambulizi ya ARVs kirusi kitahitaji kuwa na ganda la kujikinga lenye ngozi yatando mbili ili kuweza kujibadilisha.
Dk Hood anaamini kuwa sumu yanyuki iliyoshibishwa vijipande vyamelittin ina uwezo wa kitiba wa aina mbili katika kutibu na kuzuia, moja ikiwa kutumika kama maji mazito ya kuweka ukeni (vaginal jelly) ili kuzuia maambukizi ya VVU kuenea .
Tiba ya pili ni kutumika kwa maambukizi ambayo tayari yapo mwilini hasa kwa maambukizi yaliyoleta usugu wa dawa, kinadharia ni kuwa kama sumu ya melittin itadungwa mwilini nakuingia katika mzunguko wa damu inaweza kuviangamiza virusi vya Ukimwi.
Anaeleza Dk Hood kuwa, Kimsingi, vijipande hivi vya tiba vilivyotumika vilianza kufanyiwa majaribio ya kimaabara miaka mingi iiliyopita ikiwa kama zao ladamu bandia ya kutengenezwa maabara.
Hata hivyo, haikufanya vyema katika kubeba na kusambaza hewa ya oksijeni, lakini ikawa ikizunguka katika mzunguko wa damu ikiwa salama mwilini na hivyo ilitupa mwanga wa kuwezakupata mbinu mpya ya kupambana na maambukizi ya aina tofauti.
Melittin inashambulia tando mbili za ngozi laini pasipo kutofautiana, hii inaifanya melittin iwe dawa yenye uwezo wa juu kitiba katika mapambanodhidi ya maambukizi VVU.
Virusi kama Hepatitis B (homa ya ini) na C ambavyo navyo vina ganda la kuwakinga la namna hiinavyo vinakuwa miongoni mwa virusi vinavyoweza kuangamizwana tiba ya melittin.
Pia, majimaji mazito (jelly) ya melittin pia huenda yakalenga mbegu za kiume. Mtafiti Hood anaeleza kuwa inaweza kutumika kama dawa za kuzuia mimba, hivyo kuwa kama njia ya uzazi wa mpango. Hata hivyo, bado hawajalifanyia kazi.
Pia, wanaangalia uwezekano wa wenza wawili ambao mmoja wao aliyeambukizwa VVU pale watakapohitaji kupata mtoto aliye salama, kwani vijipande hivyo vya melittin ni salama kwa mbegu za kiume kwa sababu hiyohiyo ni salama pia kwa seli za ukeni.
Dk Hood anasema bado ni mapema mno kwani mpaka sasamajaribio yote ni ya kimazingira ya kimaabara.
Kwa namna yoyote itakavyokuwa, vijipande hivi vya melittin ni rahisi kuvitengeneza vya kutosha na itakuwa rahisi kuvisambaza kwa ajili ya majaribio ya baadaye kwa binadamu.
Hata hivyo, hiyo itakuwa ni habari njema endapo utafiti huo utafanikiwa na kuleta matokeo mazuri katika vita dhidi ya VVU, pia itakuja kuwa na faida kiuchumi kwa wafugaji wa nyuki nchini wakiwamo wa Tanzania.
Chanzo: Mwananchi