KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Mtangazaji mashuhuri wa muziki wa dansi, Sunday Mwakanosya, anayefahamika kwa kazi zake kupitia Chanel Ten na Magic FM, amefariki dunia leo alasiri.
Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wanafamilia, Sunday Mwakanosya aliugua kwa siku chache kabla ya kufariki katika Hospitali ya Mloganzila. Habari za kifo chake zimethibitishwa, na msiba uko nyumbani kwao eneo la Ukonga Mzambarauni, Dar es Salaam.
Inasemekana kuwa Mwakanosya alianza kuugua ghafla mnamo Disemba 25, siku ya Krismasi, na alikimbizwa katika Hospitali ya Rabininsia, Tegeta. Hata hivyo, hali yake ilizidi kuwa mbaya na akahamishiwa Hospitali ya Mloganzila, ambako alifariki dunia.
Sunday Mwakanosya atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani, hususan kwa kuutangaza na kuukuza muziki wa dansi nchini Tanzania. Kazi zake ziliwavutia mashabiki wengi, huku sauti yake na utangazaji wake wa kipekee ukiwa sehemu ya maisha ya wapenzi wa muziki wa dansi.
Pumzika kwa amani, Sunday Mwakanosya.