Unamanufaa gani kwetu sisi wabongo" je africa kuna nchi inacheza mchezo huu? Pia kuna mashindano yakidunia labda?
Siwezi kuzungumzia manufaa ya taifa zima kwani kila mtu ana raghba zake ambazo pengine ziko tofauti na za mwingine. Kwa hiyo sidhani kama hili ni suala la kuzungumzia au kulijadili katika muktadha wa manufaa ya kitaifa.
Sijui kama kwa Afrika kuna nchi ambayo huu mchezo unachezwa kwenye 'scale' kubwa lakini naamini kuna watu ambao huucheza pengine na marafiki zao.
Kuhusu mashindano ya kidunia, hapana. Hakuna.
Ila ligi ya NFL ina wachezaji na imewahi kuwa na wachezaji wengi tu wa kutoka [waliozaliwa] nchi zingine.
Kuna wachezaji wa kutoka Ujerumani, Denmark, Australia, Kenya, Uganda, Zaire [Congo], Ghana, Nigeria, Sierra Leone, Liberia na kwingineko duniani.
Kwa mfano, Tshimanga Biakabutuka ni mzaliwa wa Zaire aliyewahi kucheza kwenye NFL kupitia timu ya Carolina Panthers kwenye miaka ya 90 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Huyu ndo Tshimanga "Tim" Biakabutuka.
Halafu kuna huyu Mkenya Daniel Adongo ambaye alikuwa ni outside linebacker wa Indianapolis Colts.
Halafu kuna mwingine anaitwa Mathias Kiwanuka. Huyu ana asili ya Uganda na aliwahi kuchezea New York Giants.