Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

 
Ngoja niwatonye wazee kule kijijini wasiuze mahindi yote, maana hawachelewi kubakiza debe mbili tu za kula 🫩😒😒
 
96 mpaka 97 hiyo kipande tulikua tunaishi iliitwa Arusha ila kwa sasa ni manyara , simba na wanyama wengine walisunbua sana kwa baa la njaa mtaani
Hata mawindo mwituni yaliadimika ikabidi wanyama wakimbilie miji ya watu kutafuta chakula
 
Hii kitu hua nasikia wazee wananambia ishatokea miaka ya 90 huko kwa hiyo hii ndo itakuwa super kuliko ile...
1998 hii ilikuwa balaah ikaja kujirudia 2012 , 2022 na kidogo 2024.

Ila 1998 ilikuwa mvua kubwa kuliko kawaida mkoani kwetu nilishuhudia mwezi December mvua haikunyesha siku mbili tu mwezi mzima.
Mvua ilikuwa ikianza kunyesha usiku mnanaamka nayo nje kila mahali maji yanatembea tuliteseka sana. Mazao mengine yote yalisombwa na maji watu wakaponea kulima viazi na maharage ya kiangazi. Wakulima wengi walihamia kuvua kambale.
 
Serikali hii ya kijinga itapata kisingizio cha kutojenga barabara Kwa wakati kutokana na mvua.
Miradi yote ya barabara inaenda kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…