Kenya 2022 Support ya Uhuru Kenyatta kwa Raila ilikuwa ni chenga ya mwili au?

Kenya 2022 Support ya Uhuru Kenyatta kwa Raila ilikuwa ni chenga ya mwili au?

Kenya 2022 General Election
Habari wana Jf ,hivi ile support ya Uhuru kwa laila ni siasa ,chenga ya mwili kwa raila ?

kulingana na historia na siasa za Kenya Uhuru alikuwa tayari Raila kuwa Mjaluo wa kwanza kuingia Ikulu au chenga tu ?
Alikusudia hivyo ila matarajio yake hayakutimia yamebackfire. Kilichofanya asifanikiwe katika azma yake hiyo ni ukomavu wa wakikuyu kwani wana uwezo wa kupembua mambo ndio maana walitupilia mbali msimamo wake. Ingekuwa huku kwetu Tanzania ambako watu wanaabudu watu badala ya kufikiria hoja critically Ruto angeshindwa.

Kenyatta atakuwa anajuta kwa uamuzi aliouchukua wa kusaliti Ruto mtu aliyemuweka kwenye urais mwaka 2012.

Wakikuyu wamemfuta machozi Ruto kwa kusalitiwa na Kenyatta.
 
Alikusudia hivyo ila matarajio yake hayakutimia yamebackfire. Kilichofanya asifanikiwe katika azma yake hiyo ni uko.mavu wa wakikuyu kwani wana uwezo wa kupembua mamb ndio maana walitupilia mbali msimamo wake. Ingekuwa huku kwetu Tanzania ambako watu wanaabudu watu badala ya kufikiria hoja critically eRuto angeshindwa.

Kenyatta atakuwa anajuta kwa uamuzi aliouchukua wa ku.saliti Ruto mtu aliyemuweka kwenye urais mwaka 2012.

Wakikuyu wanemfuta .machozi Ruto kwa kusalitiwa na Kenyatta.
Kuna vitu huvielewi wewe kuhusu ukabila uliopo Kenya
 
Mzee angefia Ikulu yule wacha apumzike tu

Kikwete pia anatukanwa bongo Ila ukweli jamaa ana ushawishi Sana kimataifa

Toka amekuja Kenya wapo kwenye vikao vya siri tu kuwajenga kisakolojia wagombea upande wa Rails mpaka mission imefanikiwa.

Wajaluo hawatakuja kutawala Kenya mpaka mwisho wa Dunia.
 
Mzee angefia Ikulu yule watcha apumzike tu

Kikwete pia anatukanwa bongo Ila ukweli jamaa ana ushawishi Sana kimataifa

Toka amekuja kenya wapo kwenye vikao vya siri tu kuwajenga kisakolojia wagombea upande wa Rails mpaka mission imefanikiwa.

Wajaluo hawatakuja kutawala kenya mpaka mwisho wa Dunia.
Mzee kazungukwa sana
 
Kwenye siasa hakuna maadui wala marafiki wa kudumu.

Himaya ya familia ya Kenyatta na marafiki zake wafaidika wa mfumo lazima sasa waendane na aliye ktk madaraka .

Hivyo muungano wa Azimio la Umoja lazima kuna watakaotoka kwenda Kenya kwanza kuunga juhudi kwa kufuatana na mazingira na tamaduni za mifumo ya kisiasa na kijamii ktk bara la Afrika .

STORI YA MWINDAJI ALIYEONGOZANA NA MBWA 'MTIIFU' MWITUNI

Mzee Lee Njiru alisema katika stori zake za hekima za mazingira ya kiAfrika mbele ya televisheni tajwa kuwa mwindaji aliyeenda porini akiongozana na mbwa wake mtiifu ni lazima mwindaji awe makini.

Mzee Lee Njiru anaendelea kuwa kwani porini utakuwa pekee yako pamoja na mbwa, mbweha na mbwa mwitu.

Sasa hawa wanyama watatu ambao ni binamu mbwa kwa kila namna yaani mbwa, mbweha na mbwamwitu wakiamua kukugeuka huko porini wakati upo nao pekee yako utapona ?

MZEE LEE NJIRU : STATE HOUSE SECRETS



Maneno hayo ya Mzee Lee Njiru nikiyachukua na kuyaweka katika mazingira ya leo 15 Agosti 2022 Sasa hapa Rt. Hon. baba Raila Amolo Odinga ingawa alikuwa yupo na Uhuru Kenyatta katika Azimio la Umoja Home - Azimio La Umoja lakini wenye mwitu wa mamlaka ni waliopo ofisini kwa sasa ktk mazingira ya kiafrika ya siasa yaani rais Uhuru Kenyatta na rais mtarajiwa mteule makamu wa rais William Ruto. Sasa hapo nani ni nani kama binamu walio katika mwitu ?

AZIMIO LA UMOJA
17 May 2022 — Kenyan Azimio La Umoja presidential candidate Raila Odinga, announced Monday he had chosen lawyer and former Justice minister Martha Karua
1660585490524.png

Rt.Hon. Raila Amolo Odinga with running-mate Martha Karua ( File Photo)
 
Raila angeshinda story ingekuwa nyingine. Hata hivyo mjaluo kuwa Rais Kenya haiwezekani.
 
Habari wana Jf ,hivi ile support ya Uhuru kwa laila ni siasa ,chenga ya mwili kwa raila ?

kulingana na historia na siasa za Kenya Uhuru alikuwa tayari Raila kuwa Mjaluo wa kwanza kuingia Ikulu au chenga tu ?
Siasa na michezo yake...
 
hiyo ni mipango ya mda mrefu kabla ya kampeni wote watatu wanajua Uhuru,Raila na Ruto, Uhuru hana ugomvi wowote na makamu wake ila movie wameiandaa mda mrefu kuwapumbaza wananchi
Sawa afisa habari wa Ikulu ya Kenya.
 
Kweli magwiji wa siasa za Kenya mmoja toka Mount Kenya na mwingine toka Rift Valley wameweza kuwapiga chenga wale wa kutoka Nyanza.

Magwiji wa Mlima Kenya / Mount Kenya na Bonde la Ufa/Rift Valley wana kila sababu za kushirikiana kisiasa kwa manufaa yao kwa jinsi zilivyo siasa za Kenya .

TOKA MAKTABA :

Ruto Adai Kumiliki Kura Za Eneo La Mlima Kenya​

Na STEVE NJUGUNA

NAIBU Rais William Ruto amepuuzilia mbali juhudi za kiongozi wa ODM Raila Odinga kupenya Mlima Kenya.


Dkt Ruto alisema kuwa tayari anamiliki eneo hilo lililo na wapiga kura wengi.

Dkt Ruto ameonekana kuwa kwenye njia panda kisiasa akijitahidi kudumisha ushawishi wake Mlima Kenya wakati huu ambapo Bw Odinga amezindua kampeni kali eneo hilo.

“Kuna watu wamejua leo ati kuna mlima na sasa wameanza kutafuta google map ili waanze kupanda mlima. Ningetaka kuwaambia kuwa mimi ndiye mwenye mlima,” alisema.

“Walipokuwa kwingineko, nilizuru mara kadhaa eneo hili, tukajenga barabara Mlima Kenya na kuanzisha miradi mingine ya maendeleo. Ninawakaribisha mlimani lakini wanapokuja acha wajue kwamba kuna wenyeji kwa mlima,” alisema Naibu Rais katika Shule ya Msingi ya Nyahururu DEB, Kaunti ya Laikipia.

Wakati huo huo, Dkt Ruto pamoja na wabunge wanaoegemea kambi yake walipuuzilia mbali mkutano uliofanyika kati ya kiongozi wa ODM na viongozi wa kibiashara kutoka eneo la Mlima Kenya.

“Kuna watu wanaoandaa mikutano Nairobi kupanga jinsi ya kuja kuuza mtu ambaye amegundua leo kwamba kuna mlima unaopatikana mahali fulani. Msiruhusu watu wengine wanaoandaa mikutano Nairobi kuja kuwafanyia uamuzi kuhusu ni nani atakayekuwa rais wenu mpya,” alisema.

Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua alisema hawatampa nafasi Bw Odinga kuwashinda katika kinyang’anyiro cha urais.

“Vuguvugu la walalahoi haliwezi kuzimwa. Naibu Rais amekuwa sehemu ya jamii ya Mlima Kenya kwa miaka mingi sasa na katika muda huo, amegeuka kipenzi cha watu,” alisema. Source : Ruto adai kumiliki kura za eneo la Mlima Kenya – Taifa Leo


TOKA MAKTABA :

Ruto Abuni Mkakati Wa Kuangusha Raila Mlima Kenya​

Na JAMES MURIMI

WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya, wameamua kuingia vijijini kumpigia debe ili kuimarisha umaarufu wake eneo hilo kabla ya uchaguzi mkuu ujao.


Wakizungumza katika hoteli ya Abadare Cottage, Kaunti ya Laikipia baada ya mkutano wa kuweka mikakati ya kampeni na kutetea maslahi ya eneo hilo katika chama cha United Democratic Alliance (UDA), wabunge hao walisema watapeleka mipango ya kiuchumi ya Dkt Ruto mashinani ili kupata maoni ya wakazi.

Viongozi hao walisema kwamba chama cha UDA hakitaungana na vyama vingine kabla ya uchaguzi mkuu ujao mbali kumpigia debe Dkt Ruto na kushirikiana na vingine vilivyo na ajenda kama yake.

‘Yeyote anayezungumza lugha ya watu wa kawaida si adui wetu lakini ni ndugu. Lakini mazungumzo yoyote yatakuwa kupitia UDA,’ alisema Seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki. Wabunge hao walikanusha kwamba mkutano huo ulijadili suala la mgombea mwenza wa Dkt Ruto kutoka eneo la Mlima Kenya.

Mwakilishi Mwanamke wa Nyandarua, Faith Gitau alisema baada ya mazungumzo na wataalamu, zaidi ya wabunge 50 waliamua kuunga ajenda ya Dkt Ruto kuhusu eneo lao.

“Tutawasilisha ajenda hiyo kwa wakazi kwenye mikutano katika vijiji, vituo vya kibiashara na masoko miongoni mwa maeneo mengine,” akasema.

Hata hivyo mbinu hii inalenga kukabili juhudi za washirika wa Rais Uhuru Kenya kumpigia debe kiongozi wa ODM Raila Odinga katika eneo hilo.

“Tunataka kupata maoni ya watu, idhini na uungwaji mkono,” alisema Bw Gitau. Seneta Kindiki alisema wakazi wameamua kutumia UDA kwa sababu ya mfumo wake wa kuinua uchumi.

“Tunaalika Wakenya kuungana nasi katika safari hii ya kujenga Kenya iliyo na umoja na ustawi,” alisema Profesa Kindiki.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo ni Susan Kihika, John Muchiri, Geoffrey King’ang’i, Rigathi Gachagua, Charity Kathambi, Rahab Mukami, John Mutunga, Jayne Kihara, Patrick Munene, Ndindi Nyoro, Benjamin Gathiru, George Kariuki, Michael Muchira na Githua Wamacukuru. Source : Ruto abuni mkakati wa kuangusha Raila Mlima Kenya – Taifa Leo




TOKA MAKTABA :

Kenyan prime minister Raila Odinga discusses the International Criminal Court's charges against Kenyan officials.






Read more :

www.dailymaverick.co.za
The great escape: How Kenyatta and Ruto beat the ICC

7 Apr 2016 — In a stroke of pragmatic genius, Kenyatta and Ruto — realising their fates were now inextricably linked — joined forces to contest the 2013 ......



READ MORE :
Luis Moreno Ocampo, prosecutor for the International Criminal Court, named six top Kenyans

Announcing the names of the “most responsible” – William Ruto, Uhuru Kenyatta, Henry Kosgey, Hussein Ali, Joshua Arap Sang, and Francis Muthaura – the ICC’s prosecutor, Luis Moreno Ocampo, said that he expected the accused to cooperate fully with the ICC court ...... International Criminal Court prosecutor Ocampo names six top Kenyans for post-election violence trial
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Wakenya wamechezewa filamu.

Kuna matukio yalikuwa wazi kabisa.

Yaani Rais anampiga shoti Makamu wake live naye akiwemo.

Ushaona wapi hii.
 
TOKA MAKTABA :

4 September 2021

Raila anyenyekea wazito Mlima Kenya


Raila Anyenyekea Wazito Mlima Kenya​

Na CHARLES WASONGA
KIONGOZI wa ODM, Raila Odinga, sasa ameanza kuwinda mabwanyenye wenye ushawishi Mlima Kenya katika juhudi zake za kujipenyeza kisiasa katika eneo hilo ambalo limekuwa kizingiti kwa azma yake ya kuingia Ikulu.


Katika juhudi za kufanikisha azima yake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, Bw Odinga anaonekana kuwalenga wafanyabiashara wakubwa wa eneo hilo wampigie debe.

Bw Odinga amefanya mikutano ya mashauriano na wanachama wa Wakfu wa Mlima Kenya (MKF) , katika kile kinachoonekana kama sehemu ya mbinu yake mpya ya kupata uungwaji mkono kutoka eneo hilo lenye zaidi ya wapiga ikura milioni tano.

Mnamo Alhamisi, alikutana na viongozi na wasomi kutoka kaunti ya Meru kupitia juhudi za mabwenyenye hao. Katika mikutano kadhaa ambayo amefanya na wafanyabiashara mashuhuri wa eneo hilo, waziri mkuu huyo wa zamani amekuwa akifafanua jinsi serikali yake italinda maslahi yao na ya wakazi wa eneo pana la Mlima Kenya.

Mnamo Agosti 13 Bw Odinga alikutana na wafanyabiashara na wanasiasa kutoka eneo hilo nyumbani kwa mfanyabiashara tajiri Nginyo Kariuki eneo la Limuru. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ambapo siasa zilishamiri ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara katika Benki ya Equity, Polycarp Igathe na aliyekuwa Mbunge wa Gatanga, Peter Kenneth.

Katika mkutano huo, Bw Odinga alifafanua jinsi sera yake ya uchumi itafaidi wakazi wa Mlima Kenya.

Bw Odinga pia amezuru kaunti ya Murang’a mara mbili mwezi huo ambapo alipata mapokezi kutoka kwa miongoni mwa wengine, mfanyabiashara mashuhuri S. K Macharia.
Mnamo Alhmisi, kiongozi huyo wa ODM alirusha chambo tena katika eneo la Mlima Kenya Magharibi ambapo alifanya mkutano na wafanyabiashara na wataalamu kutoka jamii ya Ameru, katika Safari Park Hotel, Nairobi.
Mkutano huo ulipangwa na MKF, ishara kwamba wanachama wa wakfu huo wenye uhusiano wa karibu na Rais Uhuru Kenyatta, wanaunga mkono azma ya Bw Odinga ya kuingia Ikulu 2022.

Wakfu huo, ambao wanachama wake pia ni wenye ushawishi mkubwa serikalini, ulipiga jeki kifedha, kampeni za Rais Kenyatta kuelekea uchaguzi mkuu wa 2017 .

Katika mkutano huo wa kupanga mikakati ya kisiasa, ujumbe kutoka jamii ya Ameru, uliongozwa na Gavana wa Meru, Kiraitu Murungi.

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Naibu Kiranja katika Bunge la Kitaifa Maoka Maore (Mbunge wa Igembe North), Jaji Mstaafu na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa iliyokuwa Tume ya Kupambana na Ufisadi Nchini (KACC) Aron Ringera na aliyekuwa Katibu katika Wizara ya Usalama Mutea Iringo.

Wengine walikuwa Mwenyekiti wa mradi wa Lapsset Titus Ibui, aliyekuwa Waziri Msaidizi wa Elimu, Kilemi Mwiria na kaimu Gavana wa Nairobi, Anne Kananu.

Viongozi hao waliapa kuvumisha azma ya urais ya Bw Odinga katika eneo hilo huku wakiyeyusha dhana kwamba kiongozi huyo wa ODM hawezi kukumbatiwa na wakazi wa Mlima Kenya kwa ujumla.
“Maneno machafu yalitumika kumsawiri Bw Odinga kama mtu hatari na asiyefaa kuwa rais miaka ya nyuma aliposhindana na Rais mstaafu Mwai Kibaki na rais wa sasa Uhuru Kenyatta. Lakini wakati huu ambapo wawili hao hawagombei tena, hatuna budi kumuunga mkono kwa kusimama nasi tangu 2002,” Bw Murungi alinukuliwa akisema kwenye mkutano huo.
Kwa upande wake, Bw Odinga aliahidi kupiga jeki uzalishaji wa miraa, majani chai, kahawa, ufugaji ng’ombe wa maziwa miongoni mwa sekta zingine ambazo ni tegemeo la wakazi wa Mlima Kenya.

Mkutano huo umejiri siku chache baada ya wabunge kutoka eneo hilo wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kuungama peupe kuwa ni vigumu kushawishi wakazi wa eneo hilo kumuunga mkono Bw Odinga. Source : Raila anyenyekea wazito Mlima Kenya – Taifa Leo
 
15 August 2022
Bomas
Nairobi, Kenya

Wajackoyah, Ruto na Mwaure wakitaniana walipofika jengo la Bomas


Source : Nation
 
Wakenya wamechezewa filamu.

Kuna matukio yalikuwa wazi kabisa.

Yaani Rais anampiga shoti Makamu wake live naye akiwemo.

Ushaona wapi hii.
Hahahahaa
 

16 August 2022​

UHURU BETRAYED RAILA ?? Watch Ruto supporters busting Raila while celebrating Gachagua!

 
Back
Top Bottom