Kweli magwiji wa siasa za Kenya mmoja toka Mount Kenya na mwingine toka Rift Valley wameweza kuwapiga chenga wale wa kutoka Nyanza.
Magwiji wa Mlima Kenya / Mount Kenya na Bonde la Ufa/Rift Valley wana kila sababu za kushirikiana kisiasa kwa manufaa yao kwa jinsi zilivyo siasa za Kenya .
TOKA MAKTABA :
Ruto Adai Kumiliki Kura Za Eneo La Mlima Kenya
Na STEVE NJUGUNA
NAIBU Rais William Ruto amepuuzilia mbali juhudi za kiongozi wa ODM Raila Odinga kupenya Mlima Kenya.
Dkt Ruto alisema kuwa tayari anamiliki eneo hilo lililo na wapiga kura wengi.
Dkt Ruto ameonekana kuwa kwenye njia panda kisiasa akijitahidi kudumisha ushawishi wake Mlima Kenya wakati huu ambapo Bw Odinga amezindua kampeni kali eneo hilo.
“Kuna watu wamejua leo ati kuna mlima na sasa wameanza kutafuta google map ili waanze kupanda mlima. Ningetaka kuwaambia kuwa mimi ndiye mwenye mlima,” alisema.
“Walipokuwa kwingineko, nilizuru mara kadhaa eneo hili, tukajenga barabara Mlima Kenya na kuanzisha miradi mingine ya maendeleo. Ninawakaribisha mlimani lakini wanapokuja acha wajue kwamba kuna wenyeji kwa mlima,” alisema Naibu Rais katika Shule ya Msingi ya Nyahururu DEB, Kaunti ya Laikipia.
Wakati huo huo, Dkt Ruto pamoja na wabunge wanaoegemea kambi yake walipuuzilia mbali mkutano uliofanyika kati ya kiongozi wa ODM na viongozi wa kibiashara kutoka eneo la Mlima Kenya.
“Kuna watu wanaoandaa mikutano Nairobi kupanga jinsi ya kuja kuuza mtu ambaye amegundua leo kwamba kuna mlima unaopatikana mahali fulani. Msiruhusu watu wengine wanaoandaa mikutano Nairobi kuja kuwafanyia uamuzi kuhusu ni nani atakayekuwa rais wenu mpya,” alisema.
Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua alisema hawatampa nafasi Bw Odinga kuwashinda katika kinyang’anyiro cha urais.
“Vuguvugu la walalahoi haliwezi kuzimwa. Naibu Rais amekuwa sehemu ya jamii ya Mlima Kenya kwa miaka mingi sasa na katika muda huo, amegeuka kipenzi cha watu,” alisema. Source :
Ruto adai kumiliki kura za eneo la Mlima Kenya – Taifa Leo
TOKA MAKTABA :
Ruto Abuni Mkakati Wa Kuangusha Raila Mlima Kenya
Na JAMES MURIMI
WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya, wameamua kuingia vijijini kumpigia debe ili kuimarisha umaarufu wake eneo hilo kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Wakizungumza katika hoteli ya Abadare Cottage, Kaunti ya Laikipia baada ya mkutano wa kuweka mikakati ya kampeni na kutetea maslahi ya eneo hilo katika chama cha United Democratic Alliance (UDA), wabunge hao walisema watapeleka mipango ya kiuchumi ya Dkt Ruto mashinani ili kupata maoni ya wakazi.
Viongozi hao walisema kwamba chama cha UDA hakitaungana na vyama vingine kabla ya uchaguzi mkuu ujao mbali kumpigia debe Dkt Ruto na kushirikiana na vingine vilivyo na ajenda kama yake.
‘Yeyote anayezungumza lugha ya watu wa kawaida si adui wetu lakini ni ndugu. Lakini mazungumzo yoyote yatakuwa kupitia UDA,’ alisema Seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki. Wabunge hao walikanusha kwamba mkutano huo ulijadili suala la mgombea mwenza wa Dkt Ruto kutoka eneo la Mlima Kenya.
Mwakilishi Mwanamke wa Nyandarua, Faith Gitau alisema baada ya mazungumzo na wataalamu, zaidi ya wabunge 50 waliamua kuunga ajenda ya Dkt Ruto kuhusu eneo lao.
“Tutawasilisha ajenda hiyo kwa wakazi kwenye mikutano katika vijiji, vituo vya kibiashara na masoko miongoni mwa maeneo mengine,” akasema.
Hata hivyo mbinu hii inalenga kukabili juhudi za washirika wa Rais Uhuru Kenya kumpigia debe kiongozi wa ODM Raila Odinga katika eneo hilo.
“Tunataka kupata maoni ya watu, idhini na uungwaji mkono,” alisema Bw Gitau. Seneta Kindiki alisema wakazi wameamua kutumia UDA kwa sababu ya mfumo wake wa kuinua uchumi.
“Tunaalika Wakenya kuungana nasi katika safari hii ya kujenga Kenya iliyo na umoja na ustawi,” alisema Profesa Kindiki.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo ni Susan Kihika, John Muchiri, Geoffrey King’ang’i, Rigathi Gachagua, Charity Kathambi, Rahab Mukami, John Mutunga, Jayne Kihara, Patrick Munene, Ndindi Nyoro, Benjamin Gathiru, George Kariuki, Michael Muchira na Githua Wamacukuru. Source :
Ruto abuni mkakati wa kuangusha Raila Mlima Kenya – Taifa Leo
TOKA MAKTABA :
Kenyan prime minister Raila Odinga discusses the International Criminal Court's charges against Kenyan officials.
Read more :
www.dailymaverick.co.za
The great escape: How Kenyatta and Ruto beat the ICC
7 Apr 2016 — In a stroke of pragmatic genius, Kenyatta and Ruto — realising their fates were now inextricably linked — joined forces to contest the 2013 ......
READ MORE :
Luis Moreno Ocampo, prosecutor for the International Criminal Court, named six top Kenyans
Announcing the names of the “most responsible” –
William Ruto,
Uhuru Kenyatta,
Henry Kosgey,
Hussein Ali, Joshua Arap Sang, and
Francis Muthaura – the ICC’s prosecutor,
Luis Moreno Ocampo, said that he expected the accused to cooperate fully with the ICC court ......
International Criminal Court prosecutor Ocampo names six top Kenyans for post-election violence trial