Supu ni mlo unaoweza kutumia kwa breakfast ama kama chakula cha jioni haswa kwa watu wanaozingatia uzito na ufanisi wa chakula mwilini.
Supu standard inatakiwa kuwa ni mlo uliokamilika, inaweza kuwa supu ya mbogamboga, sea food, ama nyama za kawaida Ila uwepo wa mbogamboga hâta kama ni supu ya nyama, mifupa kuku au samaki itamuwezesha mlaji kupata starehe ya harufu na ladha, virutubisho vinavyohitajika mwilini pamoja na île hali ya kukinai hivyo huta-crave mavyakula mengine mazito Ili uweze kujaza tumbo kama ambavyo wengi tunaona ni kawaida.
Hizi supu tunazokunywa uswazi maji yanaongezwa Mara tatu tatu kisa tuu tunakamulia ndimu ni mazoea tunayotakiwa kuyaacha kama kweli tunamini katika nafasi ya chakula kwenye ubora wa afya.