Supu ya Kuku na viazi mbatata

Supu ya Kuku na viazi mbatata

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
supu kuku viazii.jpg


Mahitaji

Nyama ya Kuku
Viazi/mbatata - 3
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe
Pilipili mbichi - 2
Nyanya ya kusaga - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - ½ kijiko cha chai
Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya zaytuni - 2 vijiko vya supu
Kotmiri (coriander freshi) - 1 msongo
Ndimu/siki - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika

Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
•Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.

•Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.

•Kisha tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.

•Tia nyanya, haldi, na maji kiasi.
Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.

•Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa na mkate au upendavyo.
 
Sijui na kuku wa kisasa (broiler) step zake ziko hivihivi.
 
Back
Top Bottom