Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Supu ya nyama.
Mahiiaji:
Safisha nyama weka kwenye jiko bila kutia maji. Tia binzari nyembamba, tangawizi, pilipili manga, kitunguu swaumu na chumvi.
Pika bila kutia maji igeuze nyama mpaka yote iwe rangi moja, acha kwenye jiko mpaka maji yakauke.
Ikishakuwa kavu tia maji ya kutosha kwa ajili ya kuivisha nyama. Acha ichemke mpaka iive vizuri.
Kata karoti tia kwenye supu, acha zichemke kwa dakika kama mbili halafu tia njegere na viazi.
Viazi vikishaiva onja kama kila kitu kiko sawa. Ukipenda weka na ndimu.
Tayari kwa kuliwa.
Waweza kula na chapati.
Mahiiaji:
- Nyama ya mifupa 1/2kg
- Carrots 2
- Viazi 2
- Njegere kiasi
- Kitunguu swaumu 1 tsp
- Tangawizi mbichi 1 tsp
- Pilipili manga 1tsp
- Bizari nyembamba 1tsp
- Chumvi kiasi