TAARIFA RASMI YA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA KWA VYOMBO VYA HABARI YA TAREHE 29 JULAI 2024
SURA YA NNE
MADHARA YA UTOAJI VIBALI KIHOLELA, KUSAMEHE KODI NA MABADILIKO YA SHERIA YA SEKTA YA SUKARI
1.0 Uamuzi wa kutoa vibali vya kuagiza sukari kiholela vya zaidi ya kiwango cha Gap Sugar inayohitajika na
marekebisho ya Sheria yaliyofanywa yatapelekea madhara yafuatayo:-
(i) Kusuasua kwa uzalishaji na kufungwa kwa viwanda vya sukari 7 vilivyoko nchini na taifa kutegemea sukari kutoka nje ya nchi, ambapo pia kutapelekea kuathiri viwanda vya pombe kali, viwanda vya chakula cha mifugo na viwanda vya mbolea nk. vinavyotegemea malighafi ya molasses na ethanol inayotoka kwenye viwanda vya sukari kama by-products.
(ii) Kuua soko la wakulima wa miwa zaidi ya 12,500 na hivyo mashamba ya miwa kufungwa na kilimo cha miwa kufa nchini mwetu, kipato cha wakulima cha zaidi ya Tsh Bilioni 105 walizokuwa wanapata wakulima kutokana na mauzo ya miwa kupotea na nchi yetu kunufaisha wakulima wa miwa wa nchi nyingine tunazoagiza sukari.
Madhara ya mlundikano wa sukari kutoka nje ya nchi kukamata soko la ndani yameanza kuonekana nimesikia maelezo ya Mkulima wa Miwa wa Mkamba Kilombero Ndugu Kasembo Ndola ambaye ameeleza kuwa bei ya miwa imeshuka kutoka Tsh. 161,500 mwaka 2023 hadi Tsh 48,000 kwa tani 1 mwaka 2024 sawa na anguko la 70% kwa maelezo kuwa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero hana soko la kuuza sukari kwa sababu sukari ya kutoka nje ya nchi imejaa sokoni.
.
(iii) Kuhamisha ajira za watanzania za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 125,000 na ajira zingine nyingi za watoa huduma, wasafirishaji kwenda nchi zingine tunazoagiza sukari. Haya yanafanyika katika kipindi ambacho taifa linatatizo kubwa la ukosefu wa ajira ambapo vijana wengi wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali na kubaki majumbani bila ajira.
(iv) Kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa sukari nchini, Nchi yetu inaweza kutumbukia kwenye janga kubwa la kukosekana kwa sukari endapo itatokea nchi tunazoagiza sukari kukumbwa na vita, machafuko na migogoro ya kisiasa au magonjwa kama ilivyokuwa Korona na Vita vya Urusi na Ukraine. Hivyo kwa utegemezi huo wa sukari wa kutoka nje ipo siku nchi yetu itakosa sukari kabisa na kuleta adha kubwa kwa watumiaji wa sukari nchini na kuathiri uchumi wa nchi.
(vi) Kupoteza uwekezaji wa zaidi ya Trilioni 3.5 uliofanyika kwa zaidi ya miaka 7, kama viwanda hivi 7 vitafungwa zaidi ya uwekezaji wa Tsh. Trilioni 3.5 utapotea. Lakini pia wakulima wa miwa, wafanyakazi na wenye viwanda kushindwa kulipa mikopo katika mabenki na hivyo kufilisika na benki kupata hasara lakini pia kutokuaminika katika taasisi za fedha ndani na nje ya nchi kwa kuwa kunaleta taswira mbaya kwa taasisi za fedha za ndani na za kimataifa kuwa sera za uwekezaji za nchi yetu hazitabiriki. Hivyo kazi ya upanuzi wa mashamba ya miwa kuzorota na ujenzi na upanuzi wa viwanda na mashamba kusimama.
(vii) Serikali kukosa mapato ya zaidi ya Bilioni 700 yanayopatikana kutokana na mnyororo wa uzalishaji wa sukari, uchumi imara ni ule ambao unaingiza na kulinda matumizi holela ya fedha za kigeni ambapo kama tungekuwa tunaagiza sukari kutoka nje ya nchi, molasses na ethanol tungekuwa tunatumia takribani Dola za Marekani Milioni 500 kila mwaka. Pia nchi yetu imetumia zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 300 kuagiza sukari ambayo haihitajiki jumla ya tani 310,000.
(viii) Wanafunzi wa vyuo kukosa maeneo ya kufanya mafunzo kwa vitendo, kukosekana technology transfer na kulifanya taifa letu likose vijana wabobezi kwenye tasnia ya uzalishaji sukari. (Sugar Experts)
2.0 Utoaji holela wa vibali vya sukari na Misamaha ya Kodi isiyo na tija na kulisababishia hasara taifa
Utoaji holela wa vibali na misamaha holela ya Kodi ya VAT na Ushuru wa Forodha katika kuingiza sukari kutoka nje ya nchi umesababishia hasara nchi kama ifuatavyo;-
(i) Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe, Bodi ya Sukari na TRA kwa pamoja wamelisababishia Taifa hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 580.
Pia misamaha ya Kodi ya VAT imehusisha sukari inayoagizwa kutoka nje lakini wazalishaji wa ndani wa sukari hawakupewa msamaha huo na hivyo kuwawia vigumu kushindana katika soko.
(ii) Kitendo cha Waziri wa Kilimo na Bodi ya Sukari kutoa vibali vya kuagiza na kuingiza sukari zaidi ya mahitaji kumekosesha soko makampuni ya viwanda vya ndani kushindwa kulipa kodi na hivyo kuipotezea Serikali mapato ya kodi ya Tsh. Bilioni 158 kati ya Tsh Bilioni 250 zinazokusanywa kila mwaka.
(iii) Matumizi holela ya Dola za Marekani takriban Milioni 300 sawa wa Tsh. Bilioni 800 kuagiza tani 310,000 za sukari zisizohitajika nchini.
Maamuzi yaliyofanywa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe, Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari, Prof. Kenneth Bengesi na Kamishna Mkuu wa TRA, kwa pamoja wamelisababishia hasara Taifa ya Tsh. Trilioni 1.54.
Kwa maoni yangu Mawaziri na Wakuu wa mashirika wametenda makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na kuingia kwenye makosa ya uhujumu uchumi wa nchi.
3.0 Misamaha ya kodi kutozingatia mahitaji muhimu katika nchi
Misamaha ya kodi inapotolewa kiholela hupunguza wigo wa makusanyo ya kodi, huchochea upendeleo na ubaguzi wa kundi fulani na kusababisha ushindani usio sawa wa biashara na utoaji huduma nchini ambapo mara nyingi husukumwa na rushwa na ufisadi.
Kufikia mwaka 2023 misamaha ya kodi imeongezeka na kufikia wastani wa Tsh Trilioni 2 kwa mwaka sawa na 1.3% ya pato la Taifa hii ni zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa kutoa misamaha isiyozidi 1% ya Pato la Taifa. Na pia ni kabla ya huu msamaha wa Tsh. Bilioni 580, Tanzania inakusanya kodi 12.5% tu ya pato la Taifa ikiachwa mbali na nchi za Rwanda na Kenya zinazokusanya kodi zaidi ya 15% ya Pato la Taifa.
Nchi yetu inaendelea kuwa na wigo mdogo wa kukusanya kodi na kushindwa kugharamia miradi ya maendeleo na uendeshaji wa nchi kwani kwa sehemu kubwa kodi kubaki inalipwa na watu wachache na nchi kuendelea kutegemea misaada na mikopo kutoka nje.
Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan tarehe 5 Julai 2024 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Kamishna wa TRA alionyesha kukerwa na utoaji holela wa misamaha ya kodi na kwamba amechoka kunyanyasika kuomba misaada na mikopo. Mheshimiwa Rais anakataza utoaji holela wa misamaha ya kodi lakini Mawaziri wake wanaendelea kutoa misamaha kiholela na isiyo na tija yoyote kwa umma kinyume cha sheria na Katiba ya nchi huku wananchi masikini wakiendelea kutozwa kodi na tozo kubwa katika huduma muhimu.
Wananchi kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiomba Serikali kusamehe gharama za matibabu kwa wagonjwa wa figo, gharama za matibabu ya marehemu na gharama za utunzaji wa miili ya marehemu, lakini misamaha hii imeshindikana kutolewa na Serikali kutokana na ufinyu wa mapato. Tunalipa mishahara midogo kwa wafanyakazi na wananchi kuendelea kutozwa tozo kubwa kwenye huduma muhimu.
Nchi yetu ina mahitaji makubwa ya fedha kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu kwa wananchi, kwa zaidi ya miaka 3 tunahangaika kupata mtaji wa MSD wa zaidi ya Bilioni Tsh 500 kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba bila mafanikio, tumefuta Bima ya Toto afya ambayo ilikuwa inagharimu Tsh Bilioni 40 tu kwa mwaka, zaidi ya vijiji 6,000 nchini havina zahanati na kupelekea watoto, akina mama wajawazito na wagonjwa wengine kupoteza maisha bila matibabu, vijana wa vyuo vikuu zaidi ya 100,000 kila mwaka hukosa mikopo na baadhi yao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na umasikini wa wazazi wao na taifa lao.
Leo Mawaziri hawa wanapata wapi ujasiri kutoa misamaha kirahisi na tena bila idhini ya Bunge, sababu inayotolewa eti wafanyabishara wa sukari waliomba kupewa msamaha huo na Serikali ikakubali, maamuzi ambayo yamelifanya Taifa kupoteza mapato na kuingia hasara kubwa inayofikia 6% ya mapato yote ya Tsh Trilioni 26 yanayokusanywa na TRA kwa mwaka.
Miradi mingi ya maendeleo inashindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha, hata bajeti iliyopitishwa ya mwaka 2024/2025 ina upungufu mkubwa wa fedha katika maeneo ya elimu, maji, afya na miundombinu muhimu.
Waziri wa Fedha kila leo amekuwa akikimbilia nje ya nchi kutafuta fedha za misaada na mikopo na kulibebesha taifa letu mzigo mkubwa wa madeni usiobebeka huku mapato ya ndani yakiwa yanatapanywa na kufujwa bila huruma kama inavyoonyeshwa kwenye Ripoti ya CAG na Ripoti ya FIU kila mwaka.
Vilevile kuna maeneo mengi yenye uvujishaji mkubwa wa mapato lakini hatua zimekuwa hazichukuliwi kwa wakati, mfano utaratibu wa kuchangia makasha kwa wafanyabishara wanaoingiza mizigo bandarini (Cargo Consolidation & De-consolidation) ambapo nyaraka zote huchapishwa kwa jina na TN Namba ya consolidator (Bill of lading, commercial invoice, parking lists, declaration forms, TPA documents, payment slips, etc) ambaye pia hudai marejesho ya Kodi ya VAT ya manunuzi (VAT imput Tax) katika madai ya marejesho ya VAT ya kila mwezi (VAT returns) hali inayopelekea wafanyabiashara kukosa taarifa sahihi za manunuzi na ulipaji kodi na hivyo hulazimika kulipa kodi kubwa au kukwepa kodi kwa kuuza bila risiti za EFD.
Consolidator katika kusafirisha mizigo mara nyingi amekuwa akitoza tozo kwa CBM badala ya thamani ya bidhaa hali inayoashiria kuwa kuna udanganyifu na ukwepaji mkubwa wa kodi.
Licha ya utaratibu huu kuikosesha Serikali mapato kwa kiwango kikubwa na kulalamikiwa na wafanyabishara wa Kariakoo na maeneo mengine kwa kuandamana, kugoma na kufunga biashara zao hadi tarehe 3 Julai 2024 Serikali ilipotangaza kurekebisha mfumo huo na kuruhusu kila mfanyabishara kupata nyaraka za manunuzi na malipo ya kodi, kudai VAT imput Tax ili wakiwa wanauza waweze kuwa na stakabadhi za madai (VAT Refunds) na wasilipe kodi kubwa hali ambayo itaiwezesha Serikali kukusanya kodi iliyokuwa inapotelea mifukoni mwa consolidators (Oppo Agencies Company Ltd) na mapato mengi yaliyopotea kwa wafanyabiashara kutokutoa risiti za EFD. Mfumo huu umekuwepo kwa zaidi ya miaka 5.
Utaratibu wa nyaraka kuchapishwa kwa jina na TN Namba ya Consolidator unakwenda kinyume na Kanuni ya 4 ya Kanuni ya The Tanzania Shipping Agencies (Cargo Consolidator and De-Consolidators Regulations) G.N Na. 337 of 2018 ambayo imeanisha majukumu ya Consolidator na utunzaji taarifa sahihi za walipa kodi nchini, Swali kubwa la kujiuliza, je huu utaratibu unaovuruga mfumo wa utunzaji wa taarifa sahihi za walipakodi na kuipotezea Serikali mapato uliruhusiwaje? Na kwanini marekebisho yamechukua muda mrefu kiasi hicho? Na hatua gani zimechukuliwa kwa wahusika? Eneo hili linapaswa kufanyiwa uchambuzi zaidi ili kubaini mapato yaliyopotea na kupendekeza hatua za kuchukua.