Vijana vipi? Ubunifu hakuna tena siku hizi?
Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mke wangu, ilikuwa hivi . . .
Nilimwalika yeye pamoja na marafiki zake na pia rafiki zangu wa karibu jumla tulikuwa kama 30. Wote walijua ni Birthday ya Mke wangu na walikuwa wanajumuika nasi tu. Tuliifanyia katika hoteli moja ya kitalii katikati ya jiji.
Baada ya kupata dinner ambayo ilikuwa ni buffet ya vyakula vya Kitanzania, hatimaye nilimwalika mke wangu kukata keki. Alipokuwa anakata keki, mara kisu kikawa kigumu, nikamwambia labda kuna kitu ajaribu kutoa. Alipotoa kulikuwa na kibox kidogo chenye saa ndogo nzuri ya kike ya dhahabu, alifurahi saana na kila moja alifurahi nasi.
Baada ya shamrashamra hizo, nilimwomba amalizie kukata keki, safari hii tena kisu kikakwama. Alipotoa kitu kigumu safari hii kulikuwa na kibox kidogo ambacho kimefungwa vema. alikitioa na kufungua ndani yake kulikuwa nana pete ya uchumba yenye vito vya Tanzanite na Diamond. Ni wazi kabisa alipigwa na mshangao huku machozi ya furaha yakimtoka . . . .
Kabla hajataharuki, kidume tayari nilikuwa nimeshachukua pete huku nikilalama "Will You Marry Me?" . . . . hakika kulikuwa na msisimko wa ajabu. Hakujivunga aliposema "YES MY BABY", mara nikamvisha ile pete. Baada ya hapo, tukaenda kufungua mziki huku ndugu, jamaa, marafiki na wapambe wetu wakituunga mkono . . .
Sister wangu moja aliniambia kuwa wakati BF wake anamvisha pete, walikuwa wawili canteen wanakunywa soda, kumbe kidume bwana shem, kaweka pete ndani ya glass kisha akamimina coca cola. Sister alipokuwa anamaliza kunywa soda akaona ile pete, kabla hajauliza, jamaa akamwomba "PLEASE MARRY ME"